Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Visa na Mikasa vya kusaka kwangu Utajiri toka Kigoma mpaka Kongo

Taa mkuu hapa duniani tunatofautiana kila MTU ana lengo gani.
Nimeshatafuna kila aina ya k ila sijaonaga faida mkuu. Yaani huwa nasemaga nikimpata huyu BASI nitakuwa nitakuwa je ila mkuu nikshakula hakuna kitu Nakuona mie ni yule yule Wa Jana na hata Leo.
Yaani kiufupi sijawahi pataga faida yake
Kama wala kwa kutafuta kitu huwezi ona faida yake, mi nakula kama kiburudisho, yaani hakuna nnachokitafuta zaidi ya burudani naenjoi sana kula K mkuu.
 
PART I

Katika harakati za kutafuta maisha kuna mengi sana ambayo wanaume tunapitia. Leo ntawaelezea visa na mikasa ambayo nlipitia toka nimemaliza kidato cha nne mwaka 1995. Mambo haya yametokea nikiyaona na pia nikihusika.

Mimi ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto 7. Nikiwa na dada watano na mdogo wa kiume mmoja.

Nakumbuka mwaka 1995 mara baada ya kumaliza masomo nikawa home mara nyingi na vijana wenzangu.mpaka matokeo yametoka nlikuwa na division 2 hivyo nlipaswa niendelee na masomo.

Mzee hakuwa ametaka niendelee na masomo kwa kuwa hakuwa na pesa na pia mama alikuwa akiumwa mara kwa mara hivyo ikawa tunauza ng'ombe na mawese ili mama atibiwe.tukiwa na mahangaiko hayo mdogo wangu wa nne naye alishikwa na ugonjwa wa ajabu sana.

Akawa kama ana mashetani yakimpanda anatoka jasho jingi sana huku akitetemeka. Kipindi hicho anaishi Ujiji kwa Bamdogo. Ikabidi aletwe home kuja kuugua. Hapo ikabidi aitwe ustaadhi ayasikilize na kuyatuliza.tulihangaika sana. Dada zangu kuumwa umwa chanzo kilikuwa hao dada zangu kiukweli walikuwa warembo sana. Kila mtu pale kijijini aliwapenda. Wazee wengi walitamani kuoa kwetu.

Baba yangu alioa mwanamke wa mpakani na Burundi.alikuwa mzuri sana.

Pale alipokuwa anaishi sister Mzee mmoja alitaka mwoa huyu dada kama mke wa nne kipindi hicho mdogo tu.mzee alikataa. Kumbe yule mzee akamrushia majini ili yamsumbue asiolewe. Kwa hiyo ikawa shughuli hasa pale home.

Mama anaumwa sister anaumwa. Mi naendaje shule? Hali ile iliniumiza sana.nikatamani ngesoma ili niwaondoe wazee pale kijijini na akili nlikuwa nayo sana.shuleni ni wawili tu ambao tulipata division 2 wengine wote walipata 3,4 na 0.

Basi baada ya kuhangaika sana kutafuta pesa ili nikasome tulishauriana na jamaa zangu wengine wawili.

Hawa walikuwa nao wanataka pesa wamechoka maisha ya umaskini. Ahmed na Abdul. Ahmed yeye alikuwa ameishia darasa la saba akaamua kuwa mvuvi.

Jamaa alikuwa angalau anapata pata vijicent kidogo lakini hakuridhika.kila mara alikuwa ananipa mikasa ya ziwa tanganyika kwa mambo ya ushirikina.

Akisimulia jinsi ambavyo kuna siku ilikuwa wavuvi wenzie wamtoe kafara ili wapate samaki wengi.(hiki kisa ntakisimulia siku moja) Ahmed alikuwa akinikataza kupenda kupanda mitumbwi ya watu. Alinambia jinsi ambavyo kuna shangazi yake mtoto wake alianza umwa ghafla baada ya kupakizwa kwenye mtumbwi uliokuwa umepark ufukweni. Ikaja onekana yule mtoto aliguswa na misukule kwenye mtumbwi. Yule mtoto alianza kuumwa ghafla na kutokwa na udenda.walimuwahi kwa mganga ndo kupona kwake.

Basi Ahmed akawa anasisitiza sana kuwa tuvuke tuingie kongo kuna pesa nyingi sana.binafsi nlikuwa nasita maana sikuwa mzuri sana ziwani.nilikuwa na woga sababu nlishawi mezwa na mamba nikiwa mdogo lakini mzee alimng'amua kuwa alikuwa mzee jirani(mzee luyaga) akamkemea. Yule mamba alinitapika mzima kabisa.nikawa mwoga sana wa maji.

Basi tulishauriana sana baadaye tukaamua jioni moja tuondoke twende kongo.

Basi nyumbani mimi nliwaaga kuwa kuna tajiri mmoja kaomba nimsindikize kasulu kuna mambo anataka nimsaidie.mzee alihoji sana lakini akaniruhusu.

Siku hiyo ilikuwa jioni giza limeingia. Tukapanda boat tukiwa wengi kidogo kila mtu akiwa kimya.

Tulikutana na misuko suko mingi sana ziwani.nakumbuka kuna sehemu tulifika ile boat ikazima.halafu ikawa inazunguka pale pale yaani kama mtu anaizungusha hivi. Wakati huo inazunguka kwa kasi inatengeneza kama shimo kwenda chini.wale waongozaji walikuwa watatu.walipambana sana wakinyunyizia dawa n.k mwishowe wakakubaliana kuwa pale lazima tuache mtu mmoja.

Sikuelewa maana yake mpaka Ahmed alipofafanua.kuwa hatutoki pale mpaka tumtose mtu mmoja. Wakati natafakari mle ndani tupo kama 10 hivi wale jamaa wakawa kama wanashauriana jambo ila kwa kunong'onezana. Wakaanza kuuliza kila mtu aliondokaje.mimi nikajikuta nasema nliaga kuwa naenda kongo ktk wale watu mmoja akasema ye alitoroka tu hamna anayejua yupo wapi.

Wakati huo bado tunazungushwa pale pale na kuna shimo kuelekea chini ya maji kama unavyoona kimbunga.wale jamaa wakashauriana.ghafla wakamkamata yule jamaa na kumtupia kwenye maji pale shimoni. Alipogusa tu maji ni kama alivutwa chini halafu kikatokea kitu kama moshi mweusi ukamnyonya/mpokea kumshusha chini. Kukawa kimya.

Ziwa likawa limetulia sana.hapo mimi moyo unadunda sana.wale jamaa wakasema mmeona kilichotokea.tukatikisa vichwa. Wakasema hakijatokea kitu na tulivyo ndivyo tulivyotoka nchi kavu.hakuna mtu kuongelea hilo jambo kwa mtu yeyote.

Nlitetemeka sana.nilikuja shtuka tumefika ukingoni.walikuja kama migambo hivi pale pembezoni mwa maji.wakaongea na wale jamaa watatu wakapewa mshiko wakatwambia tutawanyike haraka sana wao wanaenda kusini sisi twende magharibi.

Safari ikaanza tukiongozwa na ahmad.ahmad alitutembeza sana kama masaa matatu mpaka tulipofika sehemu tukakuta kuna nyumba mbavu za mbwa na watu wanaota moto.akauliza kama tunaweza fika kwa mzee Shangai.wale jamaa wakatutizama kwa mshangao sana na kugundua tumetoka kigoma.wakahoji sana why tunataka enda mwona huyo mzee. Ahmed alisema tu kuwa kuna mwenzetu ana shida ndo tumemsindikiza.wakatuelekeza.

Ahmed alitaka tuendelee kutembea usiku huo huo. Tulitembea kama mwendo wa masaa 4. Tukifuata tu hiyo njia.mpaka kuja fika nyumba moja imezungukwa na miti.

Ile nyumba tuliifikia shida ikawa kuvuka kizingiti cha majani kwenda uwanja nyumba husika. Ilikuwa tunavuka tunakanyaga majani yametandikwa chini ila hatufiki kwenye nyumba.tulihangaika sana.hebu fikiria umbali wa kurusha jiwe kuanzia sijui saa tisa ile mpaka tunasikia jogoo hatuwezi fika hiyo sehemu. Alipowika jogoo tukagundua kumekuchwa sasa maana ilikuwa tunakaa baada ya muda tunajaribu tena.

Safari hii tukaweza vuka bila shida.tumefika karibu na mlango ahmed anaita babu, babu,babuu. Akatokea paka. Akaja akatuangalia...halafu akarudi ndani.baada ya dk moja akatokea mbabu flani hivi anatabasamu.

Akatukaribisha akitaka kwanza tujimwagie dawa miguuni.akatupa kila mtu kibuyu.tukaosha miguu. Akatwambia mmechoka laleni.

Mi nakumbuka nlikuja shtuka saa saba au nane hivi tukiwa tumelala kwenye ngozi kwenye kakibanda kengine nyuma ya nyumba.nlifikaje sikumbuki.

Tukajieleza sana.yule mzee akatwambia ngoja atueleze zaidi akatuambia tabia zetu na mambo mbalimbali ya ukweli.akamwambia Abduli wewe shida yako unapenda sana wasichana. Abdul alikataa kabisa kuwa si kweli.Mzee Shangai akawa anacheka tu.

Baadaye tumekaa akaja binti kutuletea chakula. Alikuwa binti mzuri sana.sana mzee hakutuambia kitu.basi tumemaliza kura mzee akatwambia yule binti atatupeleka kutembea shambani tuchume matunda.

Kiufupi tulimwambia mzee tunataka dawa ya utajiri.alituhoji sana hasa akisema tatizo la Abdul ni mademu.tukae naye siku tatu tufikirie kama bado tunataka dawa atatupeleka sehemu kama tumebadili mawazo ataturuhusu turudi.

Tuliona kama anatuchelewesha sana.ila hatukuwa na namna. Basi yule bint mzuri akawa anatupeleka kwenye matunda.

Abduli alishaonekana kumtaka yule demu.hivyo akawa amekaa mbele kabisa ana mdadisi dadisi bint. Mwishowe akaanza mwimbisha.yule bint alikataa sana.

Abdul akamwimbisha sana bint akasema basi tukirudi sababu mzee shangai atatoka kwenda porini mpaka kesho yake basi wataonana.

Abdul alikuja tusimulia huku anafuraha sana. Akidai anaenda kumla yule binti jioni mtoni.

Tulimtaka sana aachane na hizo issue baadaye akaanza sema ni wivu tu unatusumbua.

Kweli. Jioni mzee akaaga kuwa anaenda porini kuna watu anaenda kutana nao wanajeshi waasi.atatuacha na yule bint.

Baada kama ya kutoka masaa mawili abduli akatoka na yule bint.baadaye tumekaa chini ya mti tunaota moto abdul alirudi anapiga kelele sana

Kumuuliza tatizo nini akatujibu haoni sehemu zake za siri.mimi na Ahmed tulicheka sana tukijua jamaa anatudanganya .hapo Abdul aliangua kilio kikatushtua. Kweli Ahmed akaenda papasa.jamaa hakuwa na Ub**. Kabisa. Abdul akazidisha kulia.

Wakati tunatafakari hayo yule bint akarudi mbio naye.akaingia ndani. Abdul akawa anamwambia amwite babu shangai.bint anasema tusubiri kesho.ktk hali ya kuhangaika Ahmed akaenda mletea maji ya kunywa Abdul.

Hapo nlishindwa jizuia kucheka kuwa anamleteaje maji ya kunywa wakati jamaa hatoweza kojoa? Abduli akazidi kulia sana.nadhani akakumbuka akinywa maji hatoweza kojoa.

Nikawaza jamaa atakuwa anajisaidia kama kuku vyote vinatokea kwa nyuma.nikajikuta nacheka mpaka machozi yananitoka.

Abduli siku hiyo alikesha. Asubuhi sana akaja mzee Shangai.akaelezwa hali ile.alicheka sana.akasema Abdul tatizo lako wewe unapenda sana wanawake. Huyo ni mke wangu mi nlitaka nikuone tu je kweli ulivyokuwa unakataa.akampaka masizi kichwani. Akampiga mgongoni Abdul akalala. Alikuja amka anashika mashine.imerudi. Alifurahi sana aisee akaanza ruka ruka. Ndi kutueleza kweli alitaka kumla yule binti ila ndo akagundua yupo flat.

Na pia usiku alienda kukojoa haja ndogo ikatokea nyuma maji mengi sana. Tulijikuta tunacheka sana.

Baada ya siku tatu mzee akatwambia sasa muda umefika kama tupo tayari jioni tutaondoka wote.

Nakumbuka tulibeba maji tu kwenye vibuyu. Tulitembea sana tukipanda milima na kushuka,vijito na mito hatimaye tukafika kwenye mti mkuuuubwa sana. Mzee akatwambia tumefika tutulie hapo atuelekeze mambo ambayo yanaenda tokea.....

Nitaendelea.
😀😁😂
 
PART III

Tulitembea hivi kwa muda mrefu mpaka tulipofika sehemu moja ghafla tukamulikwa na mwanga mkali sana usoni. Mbele na nyuma yetu walisimama watu kama 7-10 wakiwa wameshika silaha mbalimbali. Wakitusemesha kwa lugha ambayo hatukuwa tunafahamu.

Abdul alikuwa wa kwanza kupiga magoti na kunyoosha mikono juu. Ahmed alinyoosha mkono mmoja mwingine ameshikilia mfuko wake.

Mimi nlinyoosha mikono yote na kupiga magoti.jamaa walikuja wakatufunika usoni na vitambaa vichafu maana vilikuwa na harufu wakaturushia kwenye gari na kuondoka nasi.

Hatukujua tunaenda wapi but ulikuwa mwendo kama wa nusu saa hivi kwa gari mwishoni tukashushwa na kuongozwa huku tukiwa tuna vitambaa usoni mikono imefungwa nyuma.

Tukapelekwa kama kwenye chumba hivi kukandamizwa mabegani kutuelekeza tukae. Tulikaa tukiwa hatujui ni wapi tupo na kwa nini tumekamatwa.

Wale jamaa walikuwa wakiongea lugha ambayo mimi siifahamu lakini nlihisi ni lugha mojawapo ya kikongo.

Baadhi ya maneno machache yalikuwa kama yanaeleweka sikuwa mzuri sana kwenye lugha ya kwetu sababu udogoni nlilelewa na padre toka darasa la 1 mpaka la 7 mpaka alipokuja hamishwa yule padre ndo nikarudi home. Ni padre ambaye alinipenda sana na alikuwa anaamini mimi nina akili sana.

Lakini ilitosha kuelewa kuwa walikuwa wanabishana jambo. Ahmed alikuwa na ujasiri akasema anaomba maji ya kunywa kwa kiswahili.wale jamaa wakanyamaza.wakakaa kama sekunde kadhaa halafu wakaoitana nje.

Wakarudi na bwana mmoja ambaye alikuwa anaweza ongea kiswahili kibovu.akatuuliza sisi ni akina nani. Tukataja majina yetu.

Wakatutandika sana kwa viboko.muda wote huo hatuoni.mikono imefungwa nyuma.wakatuuliza tena "nyinyi ni nani?" Tukajibu majina yetu wakatutandika viboko mgongoni.

Wakatuchukua na kutupeleka nje. Kipindi hicho kulikuwa na baridi kiasi wakatuweka tupige magoti kwenye kuni.

Miguu iliuma sana kisha wakawa wanatumwagia maji halafu wanapiga kiboko.unapatwa na maumivu na ganzi.yale maji yalikuwa yamewekwa chumvi kali sana.

Tulikuwa tunawashwa ila hatuwezi jikuna.muda huo tunalia tu.

Wakaturudisha tena kwenye chumba. Tukakaa mpaka kukauka.wakatumwagia upupu mgongoni na kwenye makalio.

Tuliteseka sana. Maana hatukuweza jikuna sababu mikono imefungwa.tukaanza kugara gara chini tukijikuna walati huo huo tukutonesha vidonda vibichi vya viboko.

Usiku ule hatukulala.tulikuwa uchi kabisa nguo zetu wameziweka pembeni.

Tulikuwa tunasubiri watuambie hatima ya mfuko wa Ahmed maana kumbuka ulikuwa wa ngozi pia una kitu ndani. Hawakusema lolote.

Mimi nlizimia. Sijui wenzangu. Nlikuja shtuka nimemwagiwa maji saa 12-2 asubuh. Tumelazwa kwenye kuni.tukatolewa vitambaa usoni.mbele yetu alikuwa bwana mmoja mweusi mwenye macho mekundu sana.

Akatutaka tujieleze alizungumza kiswahili kibovu.ila tulimwelewa.tukamweleza kuwa ni watanzania na tumetoka kwa mganga kupata dawa ya utajili.

Jamaa alicheka sana...akasema tunafikiri yeye "mujinga" dawa gani huko ipo? Tukamweleza akasema tukae halafu tuje mwambia tena sisi ni akina nani.

Hakutuamini. Wakafungua mfuko wa ahmed wakaona tu shati yake na kaptula.wakawa wanaushangaa mkoba wa ngozi.

Wakatuchukua na kutupeleka kwenye jiwe kutuanika. Tulikaa juani jua kali sana tukiumia kwa lile jua na vidonda.inzi wakitusumbua sana na wakati mwingine wanakuja ndege kama kunguru wanataka kutudonoa.tulishalia mpaka sauti zikawa hazitoki.

Abdul alikuwa anakoroma tu.midomo imekauka mimi machozi hayatoki nimeshikwa na kiu sana.

Mpaka mchana kama saa saba au nane hivi alikuja. Bwana ammoja akatuangalia then akaita wenzie wakaja tuchukua wakituburuza kwenda tena room.tulikuwa tumechoka na tumeumia mpaka miili imekufa ganzi.

Wale jamaa walikuja mbele yetu na sinia wameweka paja la mtoto mdogo limechemshwa. Wakitaka tule.sikuamini nikidhani ni vitisho.wote tuligoma.wakatuachia hapo wakaondoka.jioni wakarudi wakakuta hatujala. Wakaondoka.

Njaa,kiu, maumivu vilikuwa vimetushika sana. Usiku ukafika. Tukiwa kwenye maumivu makali.mara tunasikia nao wana piga kelele wakiiimba na kutiana mori.

Ikafika asubuhi tumedhoofu ile nyama ipo bado kwenye sinia.hatukula.

Mchana wakatukuta tumelala hata kukaa hatuwezi tena. Akaja mtu mmoja kama mzee hivi akawa anatuangalia huku tumejilalia very weak.

Akamchukua Abdul akaondoka naye.ukapita muda mle ndani hatuelewi wameenda mfanya nini abdul.akarudi analia sana kidole kimoja mkono wa kushoto kimepondwa kimekuwa kama nyama tu inaning'inia.analia sauti imekauka. Wakaja nikamata na mimi nilizimia.

Nlikuja shtuka wote tumekaa kwenye majani halafu kuna yule mzee anaongea na Ahmed kwa kiswahili kibovu. Ahmed akasimulia tena sababu ya sisi kuwa kule.wakaondoka wakatuacha mle ndani na walinzi.

Baada ya kama saa zima hivi wakaja tena na wengine.wakatuchukua na kutupakiza kwenye gari. Wakatufunika machoni. Abdul walimwagia unga wa njano kile kidonda wakamfunga na matambala.tukatembea nao mwendo mrefu sana mpaka kuja fika karibu na ziwa...nlianza sikia harufu ya ziwa.nikahisi wanaenda kututupa ziwani. Hofu ilinijaa sana.

Baadaye wakatushusha na kutufungua kamba.wakatupa nguo zetu. Haraka sana Ahmed akakamata mfuko wake na kuchungulia ndani. Tukamwona akitabasamu. Hatukumwelewa.mimi nlimuuliza unatabasamu nini katika hali hii.akacheka akasema tushukuru tu tumepona.

Tulikaa pale pembezon ya ziwa tukanywa maji na kuanza hangaika tutakula nini.siku 2 hatujala.

Tukaanza tembea kwa maumivu sana pembezon mwa mto kutafuta wenyeji. Tulitembea sana mpaka kuja kuta kijiji kimoja ambacho wenyeji walitukaribisha.nakunbuka alikuwa mzee mmoja na mke wake na watoto watatu.mzee alifahamu kiswahili kidogo ila mtoto wake alikuwa anakielewa.tukawaelezea.wakasema tusiingie ndani mwao. Watatuandalia sehemu nje tule then tusubiri wavuvi wakitoka watatupeleka sehemu ambayo tutapata mitumbwi ya kwenda kigoma.

Tulikula tukalala huku mimi nikiota ndoto mbaya sana. Mama alikuwa anaumwa sana lakini alikuwa ananililia mimi nikiwa nimesimama pembeni yake.

Nlishtuka nikipiga kelele na kuanza kukimbia kuelekea ziwani.wenzangu walishtuka sana...kunikimbiza hawawezi walikuwa dhaifu.kijana mmoja wa yule mzee alinikimbiza akanipiga mtama.nilianguka akanikalia juu.nlikuwa kama chizi.

Wanasema wenzangu kuwa nlikuwa napiga kelelel kuwa mama anisamehe. Yule mzee alikuja akanipaka mafuta kichwani na mengine akaninywesha.akanishika masikio akawa akiongea maneno yake flani.nikapoa.

Jioni saa 12 wakaja wavuvi.yule mzee akawaelekeza. Tukapanda kwenye mitumbwi na kuanza kuondoka. Mfukoni hatukuwa na kitu. Yule mzee kule porini tulimwachia pesa kila mtu 2000 akasema hiyo inatosha. Wale waasi walikagua na kuchukua kila kitu mifukoni.

Kwenye ile mitumbwi tulibebwa hatuna kitu.yule mzee alituombea na kusema wale jamaa wangetufaulisha kwa wavuvi wa Kigoma humo Ziwani.

Tulitembea usiku wavuvi wakivua na kutega nyavu zao. Wakaenda mpaka sehemu moja wanasema kuna kinu.ni jiwe kubwa sana.wakasema tusubiri hapo. kama baada ya masaa matatu ukatokea mtumbwi mwingine wakaongea nao na kutuambia tuhamie humo.

Tukiwa mle kwenye mtumbwi ahmed na mkoba wake tu kwapani hauachi mvuvi mmoja akamtizama na kumuuliza "utayaweza masharti yake? Hatukumwelewa.

Wakatupa ugali na dagaa tukala tukajilaza.mwili ulikuwa umechoka, unauma, akili haipo sawa. Nikiwaza matukio yote sielewi hasa nini kilikuwa kinatokea. Wakati flani hudhani it was a dream. Lakini haikuwa ndoto.

Nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua wenzangu walipatwa na nini kule ndani ya mti. Tulifika Kigoma....

Itaendelea.....
Huu ni mkasa wa maisha wa kushangaza niliowahi kuusoma humu jf... Umefunika hadi ule wa jamaa alieenda msumbiji akapewa lupatu dawa ya uchawi. More than a horror movie
 
Usituchangishe bukubuku mdau tupo uchumi wa kati
 
Mamba anameza maji tu vingine lazima avitafune tafune kwanza au avipukutishe viwe vidogo aweze kuvimeza... so kama ni Mtoto lazima amvunje kichwa kwa kukibastisha... hapo Chizi kweli Maalifa sema hadithi njoo uongo njoo utamu kolea
sayansi yako inakuambia hivyo, uswahilini haiko hivyo: mtu afichwa na mamba masaa 24, kisha anamrudisha mwenyewe pwani. Hii ni Ukara na kigoma tu, dont try at home
 
Tafadhali usitafute utajiri kwa kumtesa binadamu! Jitese mwenyewe hata nyakati za mwisho Mungu atakusamehe. Kivipi? Kutokuvaa viatu maishani hata chooni ni pekupeku, kutokulala ndani ya nyumba ya gharama, kutokuwa na mtoto maishani, na mengi kulingana na sangoma wako. Watu hawataki kujitesa ila "kutesa " .
 
nisaidie hiyo ya kujitesa
 
Back
Top Bottom