Leo nimeingia Supermarket nikachukua Mkate Mkubwa na Maji,
Ajabu tangu nachagua bidhaa kwenye Shelf kuna Mzee mmoja alikuwa ananifuata nyuma mpaka nikaogopa,
nikaenda kaunta kwa Cashier bado ananifuata nyuma!,
Nikarudi kwenye Shelf kuchukua Soda bado Mzee yupo! Duh!
MZEE : Sory kijana kama nimekutisha, unafanana sana na Mwanangu aliyefariki juzi na kuzikwa Makaburi ya Kinondoni,
MIMI: kwa hiyo mzee unataka kusema nini?
MZEE : bahati mbaya Mwanangu amefariki bila hata kusema bai, naomba unisaidie kitu kimoja, wakati naondoka nikikupa Mgongo walau useme BAI BABA! Ili nijisikie kama niliagwa na Marehemu Mwanangu jamani!, nisaidie (akatokwa machozi)
MIMI: hilo tu? Usijali Mzee!.
Kisha Mzee yule akachukua bidhaa zake mafurushi kibao mpaka pale kaunta akahesabiwa vitu vyake akabeba na kunipa Mgongo ili nitimize alichoomba.
MIMI : Bai baba!
MZEE: Bai Mwanangu Mpenzi, asante!!
Mzee yule alipoondoka nikaenda Kwa Cashier na kupigiwa hesabu
CASHIER : Kaka Unadaiwa Tsh 238,500/=
MIMI : kivipi? Yaani Mkate, Maji na Soda pesa yote hiyo? Acha Wizi wewe dada!!
CASHIER: wewe unadaiwa sh 8500 na Baba yako amesema unamlipia bili yake sh 230,000/
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Bai BABA!