Visa vyangu vya mapenzi: Harakati za kusaka mume

Visa vyangu vya mapenzi: Harakati za kusaka mume

Ila hii mada imechangamka ila tuna machungu sana za kuliwa nauli chenkov tuelewe tu
 
🤣🤣🤣 Nini kimetokea?
Mawinga tuna hekaheka sana.!
Mshauri bi dada basi mi hapa kuna mteja kanivuruga akili mpk nataka kufanya maamuzi magumu, sijui nilete kisa changu mnishauri na mimi!!
We leta kisa chako mi sitashauri Mtu mpaka niwe na bima ya afya & mwanasheria
 
Kwanini wewe unadhani ana shida na wewe? Kwani wewe huna shida nae? Mimi nadhani jamaa yuko sahihi anapima je wewe uko tayari ku invest kwenye hilo penzi.. kwa kujitolea ticket tu? ila wewe unaona yeye ana shida.. huyu achana nae atakuumbua huyo.
Jamaa jinsi anavyomfikiria manzi ni tofauti na manzi anavyojifikiria na anavyomfirikia jamaa.

Ukimsoma vizuri utamuelewa.
 
🤣🤣🤣 Nini kimetokea?
Mawinga tuna hekaheka sana.!
Mshauri bi dada basi mi hapa kuna mteja kanivuruga akili mpk nataka kufanya maamuzi magumu, sijui nilete kisa changu mnishauri na mimi!!
Nini kimetokea au nikuitie aposto😆
 
Jamani eeh, dada yenu niko singo na niko kwenye haraki za kutafuta mpenzi! Ninajiweza niko sawa kifedha na la hasha navutia kwa kudra za mwenyezi Mungu ila usumbufu naouona ni bab kubwa. Ntakuwa nahadithia hapa muwe mnanipa ushauri wa kumchagua. Wanaume hawa wote ni wabongo kasoro baadhi. Mpaka natamani kuhama mkoa mwingine kutafuta mwenza wa maisha ila sasa kazi hizi jamani doh

Mwanaume wa kwanza: Agel
Agel ni mkristo mzuri tu tulisoma wote chuo huko Dom ye akapata scholarship kwenda majuu akabaki huko,Agel hajawahi hata kuniongelesha tulivokuwa chuo ila tulikutana mtandaoni siku moja akaulizia niko vipi anaona mihangaiko yangu na anapenda sana navojishughukisha ( me nauza nguo na vitu vya ndani ) basi bwana ye anaishi majuu na ana cheo kweli kweli, kupewa cheo nchi za watu sio rahisi cv imeshiba, ni executive fortune 500 company huko yeye ni mambo ya first class na kuendeshwa na dereva, ana hadi chef wa kumpikia .

Katika majadiliano siku moja akaniambia me Chenko nakuelewa mwenzako. Nikashangaaa nikamuliza why? Akasema wewe mpambanaji nimekupenda sana na nimekuwa nakupenda toka chuo basi tu ulikua mkimya mnoo… basi mtoto nikaona yes nimepata fortune 500 husband.

Ila katika maongezi jamaa nikawa simuelew elewi, kwanza ni mkali mlalamisha usipopokea simu anaandika message ndefu barua, tuko masaa 10 nyuma sasa ni ngumu kweli mawasiliano me nimelala yeye ndo anaenda kazini, pili kila saa ananisifia uko vizuri sana kifedha nakuadmire sijawahi pata mwanamke alie kama mimi, kidogo sikupenda hii statement… halafu kila saa anataka nimwoneshe napokaaa nyumba nimpe tour eh jamani, (hata ye alitaka kunipa tour nyumba ake nkasema ya nini jamani siku ukiniliaka si ntapaona?), gari naloendesha anataka address ya nyumbani kwangu kabisa , halafu maongezi yake mhhh mara ananimiss anataka kuhug sijui hajaona mwanamke miezi 6 toka kaachwa dah hasa nikawa nakuwa uncomfortable.. (hatujaonana miaka 12) huko nikawa nakausha basi akanialika niende majuu tupate our first date angalau, mhh nikasita kidogo sababu sijawahi fika marekani na anaishi new york kabisa ila nikapiga moyo konde sababu ni mualiko wacha tuone , nikatafuta visa nikapata.. khaaa kaka si ananiambia nijilipie ticket? Ye atagharamia kila kitu cha malazi nikifika.

Huyu Agel sijamuelewa yani unanifuata wewe una hamu kuniona wewe unanitongoza wewe unanisumbua nije tuwe na first date wewe afu nijilipie ticket? Akaniambia im sure unaweza kulipia haina shida kwako, doh statement imenikata mbaya…Hela ninayo ila sina shida ya kwenda marekani saa hiii, ndo kwanza nina safari ya china mwezi ujao kuchukua mzigo. Kanidissapoint, nimwache au nimwambie tukutane dubai afu nimsikilizie?
Bonge la chai aisee halafu unatumia muda mrefu kuandika chai.
Eti New York na Tanzania ni tofauti ya masaa 12. Tanzania iko mbele masaa 7 tu. Hivi huwa mnaanzaje anzaje kutengeneza hizi status fake?😂😂😂
 
Sasa si unikumbushe, ujue dada ako bichwa langu lina mambo mengi bana.!
Naona una mambo mengi kama unga wa ngano.
Kuna kastori tuliongea labda umekasahau. Next time nitakukumbusha.
I don't want peace, i like problems.
 
Naona una mambo mengi kama unga wa ngano.
Kuna kastori tuliongea labda umekasahau. Next time nitakukumbusha.
I don't want peace, i like problems.
🤣🤣🤣 hapo kwenye “I don’t want peace” ndio penyewe sasa.!! Kuna mupya gani?
 
  • Kicheko
Reactions: 511
🤣🤣🤣 hapo kwenye “I don’t want peace” ndio penyewe sasa.!! Kuna mupya gani?
Acha leo watu wafurahie tu, sitaki kuondoa amani.
Kuna pdf 4 mpya na makaburi ya kufufua 8. Natafuta motel nzuri nikazindulie. Elewa neno motel
 
Back
Top Bottom