Kwenye hili sasa serikali itafanya nini, kupiga marufuku hizo pombe au kushauri vijana kunywa kiasi?
Sent from my SM-A105F using
JamiiForums mobile app
Mkuu huwezi kukataza watu wasinywe lakini mimi binafsi sijawahi kuona faida yoyote zaidi ya kijana kuzidi kupotea.
Nilisema too much is harmful, serikali hii haiwezi katakaza sababu wanajali pesa zaidi.
Kuna bro wangu mmoja sahiv ni bodaboda wa posta alikuwa anatumiaga sana.
Huyu bro mtaani nilipokulia kipindi nipo mdogo alishanichapa, lakini akawa ananiona naenda kusalimia wazazi safi.
Siku moja nikajisikia kuongea naye na amenizidi kiumri sana.
Nikamuambia kaka Mimi nakuheshimu sana lakini hizi pombe unazokunywa mpaka sasa na umri unazidi kwenda zimekupa faida gani? Kama huna kipato na nguvu huna utapata wapi hizi pesa?
Yule bro niliongea nae akaniambia mdogo wangu sijawahi kuambiwa haya maneno mimi naahidi kuacha.
Nilimsaidia bro kupata mkataba wa pikipiki sababu wengi hawakumumini na process za kupata Leseni.
Mpaka Leo bro ananishukuru, nafikiri vijana wanahitaji uhamasishaji zaidi.
Lakini kama utajaribu kufanya hivi bado utaumizwa tu sababu ni biashara za wakubwa.