Jankoliko,
Ieleweke nimesema hii ni tetesi tu.
Huyu dada alijua tangia ulaya kuwa ni muathirika. Kwa akili za kawaida alitakiwa ajisalimishe kwa matibabu kwenye hospitali za huko Ulaya ambazo zina vifaa tiba na utalaamu mkubwa kuliko hizi za kwetu bongo. Ndiyo maana tetesi zinasema alikuwa katumwa (kalipwa pesa nyingi) ili aje kuleta maangamizi nchini kwetu, yeye akiwa raia wa Tanzania tusingalimshuku sana.
Baada ya kuvuka vizingiti vya pale KIA angaliweza kabisa kuendelea kuusambaza huo ugonjwa kwa kujichanganya hususani kwenye mikusanyiko ya watu kama kwenye masoko, super markets, mikutano ya kisiasa ya hadhara, kukutana na watu maarufu wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa na kadhalika. Na angaliweza kufanya hivyo kwa siku nyingi tu maana afya yake ilikuwa nzuri. Na kama afya yake ingeanza kuteteleka baadaye angaliweza kurudi Ubeligiji kwa matibabu mazuri zaidi.
Hakufanya hivyo bali alienda kujifungia hotelini (self quaranteen) na kesho yake kujisalimisha hospitalini. Kitendo hiki ndicho ninakiita uzalendo ulimurudia.
Unaona hata kwa kufanya huo uzalendo ndani ya siku moja tu maelfu ya watu inawezekana alishawaambukiza. Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu hasa husambazwa haraka na mikono kugusa vitu mbali mbali. Virusi hivi huweza kuishi kwa siku nne kwenye maeneo (surfaces) zilizoguswa na mwenye virusi hivyo. Kwa mfano vitasa vya magari aliyoyagusa (ya huyo dreva na ya hao wakina Gumbo walioenda kumuchukua hapo hotelini), maeneo aliyogusa akiwa hotelini na hospitalini n.k.
lazima yaliendelea kuguswa na mikono ya watu mbali mbali na baadaye nao kwenda kugusa maeneo mengine nakadhalika. It spreads like fire. Kitendo cha kupeleka msafara mkubwa uliotumwa na mkuu wa mkoa kwenda kumchukua muathirika ni kitendo cha kulaaniwa. Daktari aliyemshauri mkuu wa mkoa kufanya hivyo anapaswa kuwajibishwa. Kitendo hiko kimechangia kusambaza virusi hivyo.