Naomba serikali isibague aina ya mikusanyiko ya kupigwa marufuku. Mimi nashauri mikusanyiko yote ikiwemo ya kidini iwe misikitini, makanisani, semina, uinjilisti, ya kukanyaga mafuta, ya kula keki, ndoa na mahaubiri ipigwe marufuku. Rais naye ashauriwe awe mfano kwa hili anazunguka na kukaa na makundi ya watu huku ameshika mike ni hatari kwake pia tena unakuta hana mask anaongea live kavu kavu.
Nina imani pia CHADEMA watasitisha azma yao ya kufanya mikutano ya kisiasa kuanzia mwezi wa nne. Mabasi ya mwendo kasi nayo yapakie abiria level seat utaratibu wa kupark mabasi wakati abiria wamejazana vituoni uachwe kwani unasababisha msongano vituoni na ndani ya mabasi yenyewe. Kama hawezi bora watu washauriwe kutembea kwa miguu au watumie baiskeli