Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Hivi ndiyo viuziuzi, badae atakuja MTU nauzi tukataze besdei mwingime mabasi mwingine mama ntilie mwingine....
Ushaambiwa epuka mikutano ya watu wengi sasa iwe harusi au maziko jiongeze mwenyewe!!
 
Habari wanaJf ,

Nadhani wengi mtakubaliana na mimi ya kuwa kkoo na maeneo ya karume sokoni ndio kitovu cha shughuli nyingi jijini Daresalaam.

Na bahati nzuri mahitaji yanayopatikana kkoo sio ya lazima sana kwamba watu wakikosa watakufa.

Ule muingiliano wa watu pale sokoni waTz,wakongo,wachina ni rahisi sana kwa watu kutoka nje ya pale kuokota maambukizi na kuyapeleka mtaani.

Ukifunga pale unapunguza maambukizi Daresalam nzima..idadi ya watu pale ni zaidi ya shule 1000 zilizofungwa,mbaya zaidi kuna raia wa kigeni.

Ni mawazo tu,Mc usiogope kivuli..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba serikali isibague aina ya mikusanyiko ya kupigwa marufuku. Mimi nashauri mikusanyiko yote ikiwemo ya kidini iwe misikitini, makanisani, semina, uinjilisti, ya kukanyaga mafuta, ya kula keki, ndoa na mahaubiri ipigwe marufuku. Rais naye ashauriwe awe mfano kwa hili anazunguka na kukaa na makundi ya watu huku ameshika mike ni hatari kwake pia tena unakuta hana mask anaongea live kavu kavu.

Nina imani pia CHADEMA watasitisha azma yao ya kufanya mikutano ya kisiasa kuanzia mwezi wa nne. Mabasi ya mwendo kasi nayo yapakie abiria level seat utaratibu wa kupark mabasi wakati abiria wamejazana vituoni uachwe kwani unasababisha msongano vituoni na ndani ya mabasi yenyewe. Kama hawezi bora watu washauriwe kutembea kwa miguu au watumie baiskeli
 
Jankoliko,
Nimekuelewa na ninakubaliana na wewe. Mzalendo wa kweli asingekubali kufanya kitendo hichi kwa nchi yake hata kama ni kwa malipo ya mapesa kiasi gani. Mzalendo wa kweli angalikuwa tayari kufa kuliko kuifanyia nchi yake unyama wa aina hii.

Mzalendo wa kweli angalibakia na kutibiwa huko huko Ubelgiji alikoupatia ugonjwa huo. Ona sasa ametuingiza kwenye taharuki kubwa sana ambayo tutaendelea nayo kwa muda mrefu na wengine tutapoteza maisha yetu. Atakapopona asiachwe hivi hivi. Sheria ifuate mkondo wake, katuletea corona kwa makusudi.
 
Mikusanyiko ya Ibada ifanyike kwenye viwanja na watu waachiane nafasi ya Mita kumi kila baada ya mtu, huduma ya wenye Imani inahitajika zaidi Kwa sasa kuliko Wakati mwingine wowote Kwa taifa
 
Aisee kufa kufaana, namuona Anko Magu akijiandaa kuahirisha sherehe za Mei Mosi kisa Corona. Halafu sijui mishahara itakuwaje ?

Naona wafanyakazi wakipigwa goli la nne na sijui akili zitawaingiaa? Ila hii korona itakuwa ndio fimbo yao nawaambia. Ni kama watumishi hewa ilivyokuwa fimbo kwa watu ambao hawajaajiriwa kutopata ajira.

Sasa jipangeni mi sio mwanasiasa wala mtabiri ila namaono ya mbaali nawasihi wafanyakazi wajipange kununa kwa mara nyinginee kwani naona Mkuu kashapata pakuchomokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafsiri yake ni nini.

Tunahofia corona sehemu za kuabudia zinafungwa..

Je ni kwamba usalama wa afya hauzingatiwi sehemu za kuabudia?

Pia.
Tunajumuika sehemu za kuabudu kumuomba mwenyezi Mungu lakini Leo corona inatufanya tuogope kukusanyika kwa vile si salama.

Je ni corona tu tuogope katika kukusanyika au Pasi na Corona mengine mungu atatuponya?

Au sasa tuseme hakuna haja ya kujumuika pamoja sehemu za kuabudu kisa corona?
 
Nitoe pongezi zangu kwa Wizara ya Afya na Serikali ya Tanzania kwa jinsi ambavyo wanaendelea na Mapambano ili kuwakinga Watanzania dhidi ya Corona.
Wasiwasi wangu ni Wataalamu wa Afya hasa Madaktari na Wauguzi wengi huenda wakatumia loopholes ya kutozuia likizo wakaomba Likizo wakapewa huko Vituoni na kutuacha tukitaabika bila msaada na kuwarejesha kazini itakuwa gharama mara mbili. Hivyo kwa busara Mhe.Waziri ungehairisha likizo zao kwa miezi kadhaa ili kadhia hiii ipite.
Ni mtazamo wa kizalendo tuu maana huenda Wataalamu wasio na Uzalendo washaanza Excuse kibao hukoooo ili kujilinda.
 
Mnh Jaman wauguzi na madaktar nao ni binadamu sio mashine zile kusema hazichoki.
Nitoe pongezi zangu kwa Wizara ya Afya na Serikali ya Tanzania kwa jinsi ambavyo wanaendelea na Mapambano ili kuwakinga Watanzania dhidi ya Corona.
Wasiwasi wangu ni Wataalamu wa Afya hasa Madaktari na Wauguzi wengi huenda wakatumia loopholes ya kutozuia likizo wakaomba Likizo wakapewa huko Vituoni na kutuacha tukitaabika bila msaada na kuwarejesha kazini itakuwa gharama mara mbili. Hivyo kwa busara Mhe.Waziri ungehairisha likizo zao kwa miezi kadhaa ili kadhia hiii ipite.
Ni mtazamo wa kizalendo tuu maana huenda Wataalamu wasio na Uzalendo washaanza Excuse kibao hukoooo ili kujilinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri lakini miluzi imekuwa mingi mno.
Tuwape nafasi kidigo wafanya mahamuzi wafanye kazi bila shinikizo toka kwetu.
 
Jankoliko,
Wagonjwa wameingia Ulaya kutoka Wuhan China wangeshindwa vipi kuingia Tanzania?. Mtu anapata virusi leo anaanza kuugua baada ya wiki mbili, utamgunduaje pale uwanja wa ndege akiwa kavaa vizuri na ana afya njema?.

Cha muhimu sio malalamiko bali ni kuikubali hali na kupambana nayo.
 
Jioni hii nikiwa na mshikaji wangu tumepita eneo moja Ilala, jamaa alienda kumuona ndugu yetu mmoja, cha ajabu nimeshangaa kukuta wanafunzi wa mitihani ya NBAA wakiwa wengi madarasani wakiendelea na masomo.

Nilipomuuliza mmoja wao akasema wao hawahusiki na katazo la serikali na hawajaambiwa wasiende darasani na waalimu wao.

Kuhakikisha nikampigia kijana wangu mmoja anasoma hiyo mitihani kumuuliza, akaniambia ni kweli wao hawajakatazwa na wanakutana kusoma kama kawaida na hata yeye akawa na wasiwasi kwa sababu madarasa hua yanakua na wanafunzi wengi sana.

Akaniambia bodi imewaambia wamiliki wa vituo vya tuition wawaambie wanafunzi wao kua mitihani iko pale pale waendelee na masomo kama kawaida.

Nafikiri baadhi wa watanzania bado wana masihala na hili gonjwa. Ndio maana unaweza kushangaa hatujafunga mipaka kwa sababu unakuta wanaotoa maamuzi ndio kama hawa, wanaojali pesa ila sio maisha ya watanzania.
 
Jamani nilikuwa nawaza kwa huyu mgeni - corona Virus- ingekuwa ni busara wenye mabasi ya mwendo kasi waongeze mabasi ili kuepusha msongamano katika mabasi yetu ya mwendo kasi.

Tusisubiri kuwa na wagonjwa wengi ndo tuzinduke. Ikiwezekana hata zile Coasta zinazopaki pale Morroco - Open university zipewe vibali maalumu zifanye kazi hata kwa nauli ya book kama mwendo kasi ili yasije kutukuta kama wenzetu wa Italy waliopuuzia sasa watu wote wamefungiwa hawatoki nje.
 
Back
Top Bottom