Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Wakati hofu ya maambukizi ya Virusi vya Corona ikiendelea kushika kasi huku serikali ikifanya kila namna ili kupunguza kusambaa kwa Virusi vya Corona, ni vema serikali ikawaondoa wapiga debe kwenye stendi za magari ya abiria (waende likizo) kwani hawa ni watu hatari sana kusambaza ugonjwa huu kwani.

hukutana na abiria mbalimbali na pia wana tabia ya kugombania abiria hivyo huweza kupata maambukizo toka kwa abiria mmoja na kusambaza kwa abiria wengine.

Kwa pamoja tutokomeze kusambaa kwa Virusi vya Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
oya oya ukitutoa tutaacha kupiga debe tuanze kupiga roba.
Tahadhari: roba ya mbao huua haraka kuliko corona.
 
Nilifanikiwa kujitoa kuwa mwanachama wa COTWU walikuwa wananikata pesa kidhalimu kabisa bila msaada wowote na sitaki tena kuwasikia! nikipata msala bora kutafuta mwanasheria mtaani!
 
Uwe na AKILI PEVU WEWE.

TANGAZO LA MIKUTANO LILIKUWA KABLA YA TANGAZO LA KORONA.

UNAPIGIA CHAPUO JAMBO LA KIPUMBAVU.
 
Kwenye mabaa huko ndo shida watu wakishaweka vitu vyao sijui Kama watajumbuka tahadhari, maana wanakuwaga hawajali Kinga au usalama hata njia za miba wao hupita peku hii sehemu iangaliwe kwaumakini Sana, daladala zibebe abilia waliokaa tu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini ndugu

Ni mda sasa toka hili janga la kirusi cha Korona limekuwa linajadiliwa na kuzungumzwa hapa jamiiforums na sehemu mbalimbali. Hivi karibuni tumeshuhudia ndugu zetu wachache wamegundlika kuupata huu ugonjwa.

Lengo la hii post nikujaribu kukusanya mawazo kutoka kwa wadau hapa jamvini juu ya jinsi ya kukabili huu ugonjwa. Tuna watu mbalimbali hapa,wenye uwezo tofauti, nina imani hatutaweza kukosa mawazo mawili matatu ambayo serikali inaweza kufaidika kuhusu kudhibiti hili janga.


Ni vyema serikali kujua kwamba namna nchi za ulaya wanavyo pamana na kirusi inaweza hisifanye kazi hapa Tanzania kutokana na mazingira yetu. Kwahiyo, badala la ku-copy na ku-paste kutoka kwenye mataifa ya nje ni vyema kukaa chini na kuja na njia mbadala ambayo inatakuwa most effective kwa mazingira yetu ya Africa.

Nashukuru Serikali kwa kufanya uwamuzi wa kufunga shule. Lakini kwa sehemu kama Tanzania, sehemu zifuatavyo pia zinaweza kuwa ni hatarishi sana na kupelekea ugonjwa kusambaa kwa kasi sana.

1.Usafiri wa daladala

Kama tunavyo jua usafiri wetu ni washida na huwa watu wana banana sana. Kama ikatokea mtu mmoja ambaye anamaambukizi basi kuna hatari kubwa ya kusambaza kirusi kwa kasi.




2.Mkusanyiko Makanisani na misikitini

Pia hapa kuna uwezekano mkubwa wa watu kusambaza huu ugonjwa. Kuweka sanitiser milagongi mwa misikiti na makanisa haita saidia maana usimamizi wake utakuwa ni mgumu na watu watakuwa hatarini. Kuna makanisa na misikiti yenye msongamano mkubwa wa watu, ni vyema serikali kuangalia hili jambo.




3.Nawaomba wizara ya afya kutengeneza centre maalumu ambayo itatumika kupokea simu za watu ambazo watakuwa wanaisi wameambukizwa.Hii ni njia rahisi kuliko watu kujazana hapo mwimbili.Pili wizara mnatakiwa kutoa maelezo au kufundisha watu kwenye radio na television dalalili za huu ugonja. watu wanaweza kuchanganya na mafua, kupelekea kuzembea na kusambaza VIRUSI.

Nakaribisha wote kwenye mjadala.
 
Kwanza mpaka sasa hapa bongo ugonjwa una muda gani tangia umeingia?
Wangapi wameathirika? Umeuwa wangapi?

Ukipata takwimu za hayo maswali nadhani utajua kwa nini serikali inadilei, Huyu mdudu kwa hapa bongo kashindwa na yupo tena sana ila hana athari kama huko kwengine.ni jambo la kushkuru kwamba ugonjwa upo na umeenea sema umeshindwa kutuuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hizi sehemu asilia kubwa kunakuwa na makelele ya muziki mkubwa ambao unasababisha watu kutosikilizana mfano mhudumu anakusogelea kwenye shavu anakuuliza kwa sauti kubwa na mate yakikurukia unakunywa kinyaji gani?

Na wewe unamjibu kwa sauti kubwa castle lite ya baridi na mate yakimrukia mhudumu >> hapo kama mate yana corona virus yanakurukia mdomoni

option mbili
kuandika kwenye karatasi au muziki uwe na sauti ndogo
 
Tuendelee kumwomba Mungu, hali si shwari kabisa hasa nchi za wenzetu wa Kizungu, mambo hayaendi kabisa! Wamekosa majibu sahihi ya hili tatizo na wamechanganyikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaambiwa tuepuke mikusanyiko lakini nashangaa kuona makanisa na misikiti yanaanza kutoa miongozo tofauti mara kunawa wapi?

Ukisikiliza wataalamu wanasemaje kuhusu uambukizwaji wa ugonjwa huu, kuwa unakaa mda mfupi hewani lakini vijidudu vikituama chini vinakaa siku tatu.

Tukiendekeza hawa watu wa imani tukaona hatuwezi kuwaamrisha kufunga shughuli zao hizi tutaleta blaa kubwa.

Moja ya mikusanyiko hatarishi ni isshu za imani. unakuta watu wote kwenye mtaa au mji wanakusanyika katika nyumba chache, kutoka sehemu tofauti.

Sasa wakiingia humu watu ambao tayari wana ugonjwa uwezekano wa kusambaza ukoje? Kwangu naona ni mkubwa sana tena makanisa na misikiti inaweza kuwa kama kutawanya ugonjwa kwenye miji yetu.

Watu watanawa mikono lakini kama kuna mgonjwa akapiga chafya kanisani au msikitini je, yapo mambo mengi.

Sasa mkimpima mtu Jumatatu mkakuta ana Corona na akasema Jumapili alienda kanisani mtaanza kufuatilia watu wote waliokuwa wamesali kuwapima kama tulivyoona mnafunga hoteli, mnamtafuta dereva taksi n.k?

Tuwe serious na mambo haya
 
Tatizo umetoa maoni huku umevaa upagani.

Maoni ya kipagani pagani tu.

Ila kiukweli hali ya corona inavoambukizwa inatakiwa hata misikiti na maksnisa yafungwe kabisa watu wasali sala tano majumbani mwao.

Pengine serikali inaona haijafilia hatua hiyo.
Mungu hata nyumbani yupo ukisali anakusikia tu.

Wasaudia wameona isiwe tabu mara hii hakuna hijja kwa kuepuka corona.

Mtoa mada acha chuki binafsi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…