Habarini ndugu
Ni mda sasa toka hili janga la kirusi cha Korona limekuwa linajadiliwa na kuzungumzwa hapa jamiiforums na sehemu mbalimbali. Hivi karibuni tumeshuhudia ndugu zetu wachache wamegundlika kuupata huu ugonjwa.
Lengo la hii post nikujaribu kukusanya mawazo kutoka kwa wadau hapa jamvini juu ya jinsi ya kukabili huu ugonjwa. Tuna watu mbalimbali hapa,wenye uwezo tofauti, nina imani hatutaweza kukosa mawazo mawili matatu ambayo serikali inaweza kufaidika kuhusu kudhibiti hili janga.
Ni vyema serikali kujua kwamba namna nchi za ulaya wanavyo pamana na kirusi inaweza hisifanye kazi hapa Tanzania kutokana na mazingira yetu. Kwahiyo, badala la ku-copy na ku-paste kutoka kwenye mataifa ya nje ni vyema kukaa chini na kuja na njia mbadala ambayo inatakuwa most effective kwa mazingira yetu ya Africa.
Nashukuru Serikali kwa kufanya uwamuzi wa kufunga shule. Lakini kwa sehemu kama Tanzania, sehemu zifuatavyo pia zinaweza kuwa ni hatarishi sana na kupelekea ugonjwa kusambaa kwa kasi sana.
1.Usafiri wa daladala
Kama tunavyo jua usafiri wetu ni washida na huwa watu wana banana sana. Kama ikatokea mtu mmoja ambaye anamaambukizi basi kuna hatari kubwa ya kusambaza kirusi kwa kasi.
2.Mkusanyiko Makanisani na misikitini
Pia hapa kuna uwezekano mkubwa wa watu kusambaza huu ugonjwa. Kuweka sanitiser milagongi mwa misikiti na makanisa haita saidia maana usimamizi wake utakuwa ni mgumu na watu watakuwa hatarini. Kuna makanisa na misikiti yenye msongamano mkubwa wa watu, ni vyema serikali kuangalia hili jambo.
3.Nawaomba wizara ya afya kutengeneza centre maalumu ambayo itatumika kupokea simu za watu ambazo watakuwa wanaisi wameambukizwa.Hii ni njia rahisi kuliko watu kujazana hapo mwimbili.Pili wizara mnatakiwa kutoa maelezo au kufundisha watu kwenye radio na television dalalili za huu ugonja. watu wanaweza kuchanganya na mafua, kupelekea kuzembea na kusambaza VIRUSI.
Nakaribisha wote kwenye mjadala.