Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Mkuu nina muda mrefu huwa nikipita karibu na bar nashuhudia viti vikiwa tupu, labda utupiemo kapicha tuone huko palipo na mkusanyiko
 
Labda wanataka kupunguza watu. Corona haina chama wala dini.
 
Nyie waajiriwa acheni mambo yenu bwana tumewachoka, kila siku mnalazimisha lockdown, lockdown.
Zaidi ya robo tatu ya watanzania hawana saving ya kuwawezesha kuishi hata siku 3 tu.
Sasa mnapolazimisha baadhi ya shughuli zisitishwe sijui mnataka watanzania wenzenu tuishi vipi.
 
Nianze maneno Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar zubeir" Kuokoa nafsi za mwengi zisiangamie ni kutekeleza Amri na maagizo ya wataalamu na viongizi wetu. Na atakayepinga amri atasababisha kufa na atadhikwa dhambi. Pia ameshauri waumini wenye matatizo ya kiafya na wazee , wabaki majumbani. kwasababu zaidi ya 50% watanzania wengi wazee na wana matatizo kiafya . Tunaomba serikali itoe tamko kufunga mara moja nyumba za ibada . Mfano DAR KAWE
 
Watu wasali majumbani mwao na Sadaka watume kwa Mpesa ili viongozi wa dini wasije kufa kwa njaa
 
Hapa maandiko yanasema tunaangamia kwa kukosa maarifa . Covid-.19. Inashambazwa kutokana na mikusanyiko ya watu. Lakini baadhi ya viongozi wa dini wamekosa uzalenzo wamejali mapato fedha kuliko uhai wa watu.
 
Huwa naona tunakosea sana kuwacheka waliokuwa wafuasi wa Kibwetere.
 
viongozi wa dini ni wabishi sana, mf gwajima hata ukimpelekea jwtz bado atatoka tu kwenda kanisani, serikali ina kazi kubwa!
 
Bado najiuliza, tuzuie mikusanyiko kwa siku ngapi?

Baada ya kuzuia mikusanyiko kwa hizo siku ndo itakuwa nn?

Mikusanyiko ya sokoni vp?
Mikusanyiko ya machinga vp?

Mikusanyiko mabarabarani vp?

Hizi pesa zinakinga?

Nzi je?
 
Hapa maandiko yanasema tunaangamia kwa kukosa maarifa . Covid-.19. Inashambazwa kutokana na mikusanyiko ya watu. Lakini baadhi ya viongozi wa dini wamekosa uzalenzo wamejali mapato fedha kuliko uhai wa watu.
Hapana mkuu, mamlaka ikitamka, Kesho tu hutaona Ibada zikiendelea, makanisa na miskiti itafungwa,

Vinginevyo unawaonea tu hao viongozi wa Dini, au la unachuki nao
 
Kwani Viongozi wetu .wanasubiri mpaka serikali isitishe hawawezu kujiongeza.tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…