Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Vita dhidi ya Corona: Mikusanyiko ya watu isiyo lazima isitishwe, misongamano idhibitiwe ili kuepusha madhara makubwa zaidi

Mkuu nina muda mrefu huwa nikipita karibu na bar nashuhudia viti vikiwa tupu, labda utupiemo kapicha tuone huko palipo na mkusanyiko
 
Katika kupambana na corona, Tanzania tumekuwa tofauti sana na wenzetu kiasi kwamba unajiuliza kama ile dhana ya dunia ni kijiji ina-apply katika nchi yetu.

Tumekuwa very selective katika kuamua ni aina gani ya mikusanyiko ipigwe marufuku na ipi iachwe wakati ukweli unabaki mikusanyiko ni mikusanyiko bila kujali nature ya mikusanyiko hiyo.

Kwa mfano,tunajidanganya sana kwa kujifanya wacha Mungu kwa kutozuia mikusanyiko katika nyumba za ibada kwa imani eti tusioogope huu ugonjwa mpaka tukashindwa kwenda kumuomba Mungu wakati unaweza kumuomba Mungu hata nyumbani kwako na akakusikiliza hasa katika kipindi hiki cha hili janga.

Sasa, wakati tumeacha kudhibiti baadhi ya mikusanyiko huku idadi ya wagonjwa ikiongezeka,ni jambo la kushangaza kuona tumeshindwa hata kuzuia mikusanyiko kwenye mabaa ambapo watu wanajazana na huku wakinywa kwa pamoja katika meza moja kanakwamba hatuna tishio la corona.

Kwa hakika tunashangaza sana, ila muda si mrefu tutavuna tunachopanda kama Taifa.
Labda wanataka kupunguza watu. Corona haina chama wala dini.
 
Nyie waajiriwa acheni mambo yenu bwana tumewachoka, kila siku mnalazimisha lockdown, lockdown.
Zaidi ya robo tatu ya watanzania hawana saving ya kuwawezesha kuishi hata siku 3 tu.
Sasa mnapolazimisha baadhi ya shughuli zisitishwe sijui mnataka watanzania wenzenu tuishi vipi.
 
Kakorona kenyewe kako hivi
IMG_20200410_192126.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nianze maneno Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar zubeir" Kuokoa nafsi za mwengi zisiangamie ni kutekeleza Amri na maagizo ya wataalamu na viongizi wetu. Na atakayepinga amri atasababisha kufa na atadhikwa dhambi. Pia ameshauri waumini wenye matatizo ya kiafya na wazee , wabaki majumbani. kwasababu zaidi ya 50% watanzania wengi wazee na wana matatizo kiafya . Tunaomba serikali itoe tamko kufunga mara moja nyumba za ibada . Mfano DAR KAWE
 
Watu wasali majumbani mwao na Sadaka watume kwa Mpesa ili viongozi wa dini wasije kufa kwa njaa
 
Hapa maandiko yanasema tunaangamia kwa kukosa maarifa . Covid-.19. Inashambazwa kutokana na mikusanyiko ya watu. Lakini baadhi ya viongozi wa dini wamekosa uzalenzo wamejali mapato fedha kuliko uhai wa watu.
 
viongozi wa dini ni wabishi sana, mf gwajima hata ukimpelekea jwtz bado atatoka tu kwenda kanisani, serikali ina kazi kubwa!
 
Bado najiuliza, tuzuie mikusanyiko kwa siku ngapi?

Baada ya kuzuia mikusanyiko kwa hizo siku ndo itakuwa nn?

Mikusanyiko ya sokoni vp?
Mikusanyiko ya machinga vp?

Mikusanyiko mabarabarani vp?

Hizi pesa zinakinga?

Nzi je?
 
Hapa maandiko yanasema tunaangamia kwa kukosa maarifa . Covid-.19. Inashambazwa kutokana na mikusanyiko ya watu. Lakini baadhi ya viongozi wa dini wamekosa uzalenzo wamejali mapato fedha kuliko uhai wa watu.
Hapana mkuu, mamlaka ikitamka, Kesho tu hutaona Ibada zikiendelea, makanisa na miskiti itafungwa,

Vinginevyo unawaonea tu hao viongozi wa Dini, au la unachuki nao
 
Kwani Viongozi wetu .wanasubiri mpaka serikali isitishe hawawezu kujiongeza.tu
 
Back
Top Bottom