Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Hapa hakuna kitu. Ni maigizo tu. Anatuma message kwa wale mapapa kuwa wawe waangalifu huku watumiaji wachache wakitolewa kafara
 
Boss wake juzi amemsifia tena amemtaka atembee KIFUA MBELE, hiyo Idara itamdhibiti vipi unadhani??
Huenda alikuwa hajazipata habari za Msukuma na yaliyojiri ziarani Asia, ulaya na America.
Na kama kazipata naona atamwondolea kazi na ulinzi kwani hii in dharau sasa juu ya vita ya ufisadi inayonadiwa kupiganwa huku wateule wakiendelea kuzipiga kuliko zamani.
Na kwa mtindo huu mahakama ya mafisadi haitompata hata mteja mmoja.
 
Akomae, vita dhidi ya madawa ya kulevya ni kali sana.

Ndio maana hao akina MSUKUMA wamenyanyuka juu yake baada ya kuona maslahi yao yameguswa!
Sasa hivi tumeanza kuona mwanga sasa. Bavicha walikuwa wanakupoteza mzee
 
Hii vita inahitaji approach mpya ,matatizo ya madawa ya kulevya yapo kabla Makonda hajawa RC lakini hizo agency hazijawahi kufanya lolote na polisi wanaifahamu hii biashara vizuri na ni washiriki wakubwa kwenye hii biashara ndio maana umeona ile list waliokamatwa kuna polisi wengi.Hii vita inakuwa one man show sababu wafanyabiashara na vigogo wa idara za serikali ni wadau wa hii biashara.Hata Duterte anafanya one man show na amepata upinzani mkubwa sana lakini ameendelea kuwaua na wengi wamekimbia na hata wale waliokuwa wanataka kuingia kwenye biashara wanajua mambo yamebadilika. Vile vile madawa ya kulevya yanaingilia na kutokea DSM na pia ndio kuna watumiaji wakubwa

Makonda anapata upinzani kwa mambo mengine aliyofanya huko nyuma lakini kwa hili yuko sawa,kelele zake zinasababisha matatizo mengi yanazidi kujulikana
 
Anaipenda clouds kwasabubu
1..ndio wanamuandikia na kumuandalia mipango
2..ndio aliwahi kusema wana akili kuliko staff wa office yake
3..Pele yy km mtangazaji

NB Luna vijana pale kawanunulia hadi magari
1.yule wanamuita muuza magazeti kapewa Benz Mercedes
2..kuna mpiga picha wa video pale kampa rav 4

Kifupi wale clouds ndio wajanja wake
 
UKAWA wanasapoti wauza mihadarati!!? Siamini! Hizi siasa zitaichafua nchi
 
Umeonge kitu kikubwa sana Mkuu kama walioko polisi wote waliitwa kuhojiwa wakabaki huko mpk Leo na kwake iwe hivyo kupitia tuhuma zinazomkabili
 
Umemwelewa vizuri tu ila ujuaji wako
 
Makonda hatumpingi ila tunamchana ukweli wa mambo ulivyo ,vita vya madawa ya kulevya hazikuwa za mkuu wa mkoa naomba nikukumbushe KITWANGA alivyotuambia kabla hajamwaga unga "hatuwezi kuwakata kuwataja ila tumeandaa mkakati wa kuzia madawa yasiingie nchini '
Pili kazi hii ilipaswa kufanywa na RAIS ,MAKAM NA WAZIRI MKUU kwa sababu majina ya mapapa wanayo ikulu yaliachwa na JMK
 
Kwanini asiende TBC ?? Tunakolipia kodi zetu .
Huko MAWINGU kuna nini si nimeskia nao wako kwenye ile list au atawasafisha kwenye tuhuma
Why mawingu ?
Kazi ya serikali inafanyikia kwenye vyombo binafsi dah na mbana matumizi analiona hilo ujinga wa kijinga kwenye ujinga waambiane wajinga wenzao sisi tunajua kilichonyuma ya kinachosemwa
 
Makonda anawafungulia milango GSM kuwa wamiliki wakuu wa biashara ya madawa ya kulevya. Hii dhana inaleta maana.
 
Thanks for info mkuu hatukuwahi kujua hayo uliyoyataja yalitokea na yakafanikiwa.
 
Mmh,acha kuropoka jamaa yangu,wameumbuana so far ni ccm wenyewe,tumemsikia waziri wa michezo,tumemsikia mbunge wa ulanga tumemsikia mbunge wa geita vijijini wote hawa ni makada wa ccm,hata hao uliowataja ni ccm kitambo.
 
Nasema tena Adili na Akina wema na chid Ila Hao wengine Tutabaki kuwasikia tuuu

Mizizi yao ni mikubwa
 
Umesahau bosi wao kusaga anakula na kuuza unga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…