Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Huenda alikuwa hajazipata habari za Msukuma na yaliyojiri ziarani Asia, ulaya na America.
Na kama kazipata naona atamwondolea kazi na ulinzi kwani hii in dharau sasa juu ya vita ya ufisadi inayonadiwa kupiganwa huku wateule wakiendelea kuzipiga kuliko zamani.
Na kwa mtindo huu mahakama ya mafisadi haitompata hata mteja mmoja.
Hahaha, hii ni vita ya mafahari wawili.
 
Makonda hatumpingi ila tunamchana ukweli wa mambo ulivyo ,vita vya madawa ya kulevya hazikuwa za mkuu wa mkoa naomba nikukumbushe KITWANGA alivyotuambia kabla hajamwaga unga "hatuwezi kuwakata kuwataja ila tumeandaa mkakati wa kuzia madawa yasiingie nchini '
Pili kazi hii ilipaswa kufanywa na RAIS ,MAKAM NA WAZIRI MKUU kwa sababu majina ya mapapa wanayo ikulu yaliachwa na JMK

Ukitaka kuamini kila alichokifanya JK anzia kwenye issue ya reli SG na jiulize kwanini Magufuli amezikataa tirioni 17 ambazo wachina walikuwa tayari kutoa kama mkopo nafuu. Kiongozi usizungumzie issue ya madawa kwa utawala wa JK kama kweli una historia kidogo na ilo. Hivi raisi kufikia hatua ya kutolea mfano mkewe kuwa kama wanahisi anauza wamkamate haukuelewa maaana yake.

Vita ya madawa ni vya jeshi la Polisi na nguvu ya mkuu wa mkoa ni kubwa kwenye mkoa wake ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama kwenye mkoa wake.

Makonda anafanya kazi nzr sana lakini mnamvunja moyo sana. Ebu chukulia ungekuwa ni wewe utajisikiaje.

Huyo Kitwanga hachana nae maana kashifa zake zilikuwa wazi pengine madawa alikuwa anatafuta sababu tu.
 
Mwanzo nilimuunga mkono Mkono jamaa nikidhani hii vita ni for real, hata hivyo Hukumu ya Jana imethibitisha kuwa hao waliokamatwa ni insignificant, hawana impact yoyote katika biashara ya madawa!

Wema naona ameamua kumtunishia msuli wa kimamlaka!

Hii ni aibu!

Mkuu kumpeleka mtumiaji wa Madawa ya kulevya mahabusu unaenda kujaza mahabusu tu...hao watu wanahitaji msaada yaani wasaidiwe ili waache kutumia hayo Madawa.

Kuna wengine nilisikia ni wasambazaji katika hilo kundi sasa Sijui labda hawakukutikana na kitu hapo sijajua bado.

Ila kwa kweli mm naona hii kitu ni kiki tu za kisiasa zinatafutwa...hamna kitu hapa.

Tumekuwa tunasikia miaka na miaka kuwa wauza Unga nchi hii wanajulikana...sasa Sijui kigugumizi cha kuwashughulikia kinatoka Wapi tu???mpaka tunaanza kushughulika na watu Sijui wenye msokoto mmoja..
 
Hii 05:00 unamaanisha saa kumi na moja alfajiri ama? Nilivyofundishwa mimi ni kwamba masaa yanaandikwa kwa namna mbili. Either kwa kutumia mfumo wa masaa kumi na mbili yaani 05:00PM/AM ambayo ni saa kumi na moja alfajiri au saa kumi na moja jioni au kwa masaa 24 yaani 0500HRS ambayo humaanisha saa kumi na moja alfajiri. Wewe umemaanisha muda upi mkuu? Au ulitaka kumaanisha saa tano asubuhi?

Heshima yako bwana barafu
 
Ukitaka kuamini kila alichokifanya JK anzia kwenye issue ya reli SG na jiulize kwanini Magufuli amezikataa tirioni 17 ambazo wachina walikuwa tayari kutoa kama mkopo nafuu. Kiongozi usizungumzie issue ya madawa kwa utawala wa JK kama kweli una historia kidogo na ilo. Hivi raisi kufikia hatua ya kutolea mfano mkewe kuwa kama wanahisi anauza wamkamate haukuelewa maaana yake.

Vita ya madawa ni vya jeshi la Polisi na nguvu ya mkuu wa mkoa ni kubwa kwenye mkoa wake ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama kwenye mkoa wake.

Makonda anafanya kazi nzr sana lakini mnamvunja moyo sana. Ebu chukulia ungekuwa ni wewe utajisikiaje.

Huyo Kitwanga hachana nae maana kashifa zake zilikuwa wazi pengine madawa alikuwa anatafuta sababu tu.
Huyu huyu alituaminisha kuwa wauza shisha walitaka kumuhonga hajawachukulia hatua
 
Huyu huyu alituaminisha kuwa wauza shisha walitaka kumuhonga hajawachukulia hatua

Kwa kweli kwenye issue ya shisha nampongeza sana, kila maali palikuwa pamearibika shisha ilivutwa wazi kuliko hata sigara mkuu kwenye ili Makonda anasitaili pongezi. Pengine alitereza kusema walitaka kumuongo na akutwambia wamechukua hatua gani lakini mkuu napongeza sana bado issue ya massage kufanywa vyumba vya umalaya nalisubiri ili.
 
Mengi yamesemwa ni muda muafaka wa kusikiliza upande wa pili ya sarafu ili vita iendelee vyema
 
Kuna baadhi vyama mpaka leo havieleweki vinasimamia maslahi ya nani, kuna wawakilishi wao walikuwa wanapiga sana kelele juu ya madawa ya kulevya leo mtu anasimamia wao wanakuja juu kutetea hao wahusika kila siku mapovu yanawatoka juu ya mapapa wa madawa hamjui kuwa viongozi wenu pia ni wahusika wakuu wa madawa nani asiye urafiki wa Lowassa na Rostam, rostam na familia yake ni mmoja wa wahusika wakuu.
Je nani hajui kuhusu GWAJIMA ambaye ndiye alkua mlez wa CHADEMA nani hajui juu ya haya.

Naona humu tunashabikia tunapiga kelele juu ya kitu ambacho hatukijui, msifuate upepo nyie bendera.
Umejidhihirisha kuwa uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo mno! Endelea kuchezeshwa Lizombe! Na katika hili wewe ndiye bendera!
 
Mpaka sasa hivi tumegawanyika vibaya

Ccm (watakatifu) vs wapinzani (wasiotakiwa)

waliotumbuliwa Vs watumbuwaji

wazushi wakisiasa vs waathilika

kwa hali hii visasi havitakwepeka ni suala la muda.....na tukianza kulipizana visani laana itatuweka pabaya......

majuto nimjukuuu
.
b:2/#freemaxencemeloPanda hofu, vuna hasira. Kandamiza uhuru, pata ukimya. Hasira na ukimya zikichanganyika, zinanyesha laana za mababu.6:00 AM - 16 Dec 2016468468 Retweets576576 likes.

.
Maneno ya prof. Shivji haya.
Kikombe cha machukizo ya watawala kwa sasa ni kama kinaharakishwa kujaa.

Kuna baadhi vyama mpaka leo havieleweki vinasimamia maslahi ya nani, kuna wawakilishi wao walikuwa wanapiga sana kelele juu ya madawa ya kulevya leo mtu anasimamia wao wanakuja juu kutetea hao wahusika kila siku mapovu yanawatoka juu ya mapapa wa madawa hamjui kuwa viongozi wenu pia ni wahusika wakuu wa madawa nani asiye urafiki wa Lowassa na Rostam, rostam na familia yake ni mmoja wa wahusika wakuu.
Je nani hajui kuhusu GWAJIMA ambaye ndiye alkua mlez wa CHADEMA nani hajui juu ya haya.

Naona humu tunashabikia tunapiga kelele juu ya kitu ambacho hatukijui, msifuate upepo nyie bendera.
.
Kwa maana unataka kutuambia makonda kukamata wale vidagaa ni kupoteza lengo la hawa unaosema kila mtu anawafahamu?
 
Back
Top Bottom