Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Wapi ulisikia mhalifu anatangaziwa Clouds tv/radio aende polisi
Wapi ulisikia mtu anaitwa mhalifu wakati hakuna uchunguzi,kidhibiti au ithabati yoyote
Huu ni uhuni mtupu
Anadhani anaweza kujijengea sifa kama marehemu Amina,matokeo anavuna aibu na dharau
 
Maandishi yako tu yanatia kinyaa, kuanzia sarufi mpaka fasihi.

Sio huko bungeni, hata huku nje kuna ambao tumeshaiona tofauti hiyo vita yenu na Wema Sepetu. Wabunge wenye mtazamo uliokomaa hawawezi kuungana na wewe ikiwa unaamini kwenye one man show. Mtu unayemchunguza unamtaarifu?

Mtu anatuhumiwa kwa mihadarati, unampa taarifa na kumwomba ajisalimishe. Ambaye ni mbunge, ana tuhuma za KAULI unatuma kikosi kikamkamate...tumia akili yako wewe, kati ya hawa wawili yupi hapaswi kupewa muda wa kujiandaa ili asipoteze ushahidi? Who is likely to run away, MP or Drug Dealer?
 
Bora Kikwete alikaa kimya kuhusu hii vita.

Sasa hivi huwezi kujua nani mpinzani nani chama tawala wote wameungana.
 
Hii ni vita dhidi ya wauzaji na wapingaji so ukimwona binaadam mwenye watoto na family yake ndg nk anapinga vita dhidi ya madawa jua huyo ni mhusika kwa namna moja au nyingine!.
 
 
Lowasa kama anahusika aswekwe lupango tumechoka na wauza madawa et kisa wapinzan



Kwani wapinzani wangapi wameshatajwa hapo? Vipi kuhusu yule anayejulikana ambaye alisababisha JK asitoe yale majina aliyoletewa?
 
Think Great in order to be a Great Thinker!!!!
 
Huwezi jua uchungu wa kuchafuliwa jina kaa kimya..sipendi wauza unga ila sipendi njia anayotumia makonda kwenye hii vita yake.
 
Swali jepesi, akitokea mtu akamtaja Makonda kuwa anahusika, je atakamatwa? Maana polisi are acting on tips from different sources? Kama hawawezi basi haya yote kuna watu wanalengwa!
Atajwe mara ngapi?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu nashindwa kuelewa nimuunge mkono mheshimiwa Makonda kwa asilimia ngapi maana anachokifanya sasa huko Dar ni jambo zuri lakini naona kama itapokuja kubainika kuna uonevu kwa baadhi ya watu itabadili taswira nzima ya azma yake njema jambo ambalo tayari lipo na limesha wagawa watu UPANDE mbili.

Mimi kama mpenda haki nikae upande upi ukizingatia na hali ilivyo sasa??
 
Hili movie ya makonda madawa ni ya kipuuzi na ita backfire kwake.

Kuwatuhumu watu na kuwaachia kwa kukosekana ushahidi haina maana bali atajiongezea maadui wengi wenye hali na mali.

Wahusika wangekamatwa na madawa kabla ya kuchafuliwa majina tungemuona konda shujaa.
 
aisee ndani ya cm kuna vichwa sana..daah.. yani upinzani wa kweli upo ndani ya ccm na watu wanaongea kweli ..yani waongeaji wazuri kuliko hata hao wa upinzani
 

Kwani ww ndiye uliyewateua ?. Hizi ni sawa na kelele za branding na za yule mchekeshaji.
Amir jeshi Mkuu kashatoa tamko, na km huna za kujiongeza kujua nani hasa yupo behind muvu nzima basi tulia mnyolewe vizuri !!

Mlikuwa wapi siku zote au wakati ule au mliona priority ni kuzusha ugaidi, na kuwapiga watu mabomu na kuhangaikia mambo ya Yanga tuuu badala hata ya panya road ??
 
Kuna kila dalili na harufu isiyo ya kawaida ya watanzania kuyumbishwa. Watanzania wamesahaulishwa mambo yote na kugeukia 'filamu itiayo hamu' ya madawa ya kulevya chini ya muongozaji Makonda. Watanzania wamehamishwa kwenye mambo yote, hata yale ya karibu yao.

Kulikuwa na suala la mikutano ya kisiasa,mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, viwanda, Sheria ya Makosa ya Mtandao na ile iwahusuyo Wanahabari; mfumuko wa bei na matokeo mabovu ya kidato cha nne. Yote hayo yamesahaulishwa, ni madawa ya kulevya tu.

Makonda amejivika u-IGP,u-DCI,Uwaziri na Uhakimu. Ameota mapembe,analidharau hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatamba kwa kuwabamba watanzania kwakuwa wanamfuatilia. Makonda anapaswa 'kususiwa' na kudhibitiwa. Ni kwakuwa hashauriki wala haambiliki kwasasa.

Madawa ya kulevya ni jambo baya. Vita yake ni muhimu na inahitajika bila kuchoka. Lakini, aina ya vita ya kupambana na madawa ya kulevya si hii ya Makonda. Madawa huingizwa,kusafirishwa,kuuzwa na kutumiwa sirini. Iweje vita yake iwe hadharani? Kutajataja watu ni kuwachafua na kuwashtua.

Makonda, kama atang'ang'ania aina hii ya kupambana na madawa ya kulevya, anapaswa kuachwa mwenyewe. Wengine tuendelee na mambo mengine ya kitaifa. Haiwezekani wote tusombwe na 'harakati za kuigiza' na zenye kuelekea kwenye giza. Haiwezekani.

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ila amefanikiwa sana. Lile suala la mkoa wa darisalama kuwa "kinara" kwa "kufelisha" limekosa nguvu kabisa, halisikiki tena si uraini wala bungeni!

Kuna mtu alikuwa anasema ati hata ile singo ya Darassa ('muziki') nayo chalii!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Nafikiri Mh mkuu wa Mkoa alieleza mwanzoni kabisa sababu ya kutangaza hadharani naona wabezaji bado mnabeza bila kuja na njia mbadala,msikariri mambo ya sirisiri ndio nini?mbona mnataka kufanya hili jambo kama ni hot cake?wakati HAKUNA KINACHOSHINDIKANA CHINI YA JUA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…