Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Wapi ulisikia mhalifu anatangaziwa Clouds tv/radio aende polisi
Wapi ulisikia mtu anaitwa mhalifu wakati hakuna uchunguzi,kidhibiti au ithabati yoyote
Huu ni uhuni mtupu
Anadhani anaweza kujijengea sifa kama marehemu Amina,matokeo anavuna aibu na dharau
 
Maandishi yako tu yanatia kinyaa, kuanzia sarufi mpaka fasihi.

Sio huko bungeni, hata huku nje kuna ambao tumeshaiona tofauti hiyo vita yenu na Wema Sepetu. Wabunge wenye mtazamo uliokomaa hawawezi kuungana na wewe ikiwa unaamini kwenye one man show. Mtu unayemchunguza unamtaarifu?

Mtu anatuhumiwa kwa mihadarati, unampa taarifa na kumwomba ajisalimishe. Ambaye ni mbunge, ana tuhuma za KAULI unatuma kikosi kikamkamate...tumia akili yako wewe, kati ya hawa wawili yupi hapaswi kupewa muda wa kujiandaa ili asipoteze ushahidi? Who is likely to run away, MP or Drug Dealer?
 
Bora Kikwete alikaa kimya kuhusu hii vita.

Sasa hivi huwezi kujua nani mpinzani nani chama tawala wote wameungana.
 
Hii ni vita dhidi ya wauzaji na wapingaji so ukimwona binaadam mwenye watoto na family yake ndg nk anapinga vita dhidi ya madawa jua huyo ni mhusika kwa namna moja au nyingine!.
 
Kipindi fulani tulipiga sana kelele kwamba wateule wa rais wapewe instruments ili kila mmoja aelewe majukumu yake na mipaka yake.Hili halikieleweka vyema matokeo yake limefanya wakuu wa mikoa kugeuka mawaziri.

Katika kipindi cha nusu mwaka hivi kumekuwa na matukio ya hovyo sana hapa jijini Dar Es Salaam ya kulitumia jeshi la polisi katika kutekeleza matamko mbalimbali ya muheshimiwa Mkuu wa Mkoa

Ikumbukwe kwamba jeshi la polisi lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambaye waziri wake ni Waziri Mwigulu Nchemba

Kitendo cha RC Makonda kutaka kulitumia jeshi la polisi kutekeleza matamko yake sio jambo zuri hata kidogo. Matukio ni mengi lakini mara nyingi sana Makonda ametoa maagizo kwa jeshi la polisi kufanya hiki na kile kana kwamba yeye ndiye waziri. Hii ni kutaka kuonyesha kuwa waziri Mwigulu ni waziri Uchwara jambo ambalo sio kweli.

Juzi juzi hapa alimshutumu Kamanda Sirro mbele ya hadhara kwamba anaonekana kuwabeba wauza Shisha......

Lakini pia hivi sasa kina hiki kinachoonekana vita dhidi ya madawa ya kulevya. Kiutendaji jambo hili linatakiwa kusimamiwa na waziri Mwigulu kwa kuwa anavyo vyombo vya kufanya uchunguzi na kuchukua hatua. Lakini ajabu Makonda kajimilikisha vita na kujiegeza ubavuni mwa rais Magufuli.......Huku waziri Mwigulu akiwa hana la kufanya

Jambo hili sio la kuchekewa kwani ipo siku RC atamtaka CDF aingize jeshi mtaani

Naunga mkono azimio la Bunge kuwa Ofis ya Rais awaandikie RC na DC watambue majukumu yake

Inawezekana sarakasi yote hii ni kwa sababu viongozi wa awamu hii hawakuapata semina elekezi?

RC Makonda kumpokonya madaraka Mwigulu haikubaliki
 
Lowasa kama anahusika aswekwe lupango tumechoka na wauza madawa et kisa wapinzan

Kwani wapinzani wangapi wameshatajwa hapo? Vipi kuhusu yule anayejulikana ambaye alisababisha JK asitoe yale majina aliyoletewa?
 
Na hii inathibitisha ile per cent 80 iliyotaka mfumo wa chama kimoja uendelee ilikuwa sahihi.Angalia leo hii ktk vita hii ya mihadarati upinzani umekufa ganzi.Tunawaona wanaccm tu wengine wakipigana vita hii na wengine wakikosoa kwa kupendekeza njia mbadala.Nimeshangaa hata mpambanaji wa upinzani anayeaminika KC Zitto Kabwe amepigwa ganzi!Kuna nini jamani huko upinzani?Nijuavyo mimi mlango wa ruzuku ya vyama ni mmoja tu Serikali, sasa kwa nini wapinzani mnashindwa kuiunga mkono ktk hivi vita.Hata kama kutajwa kwa KUB kumewakera yule ni binadam ana mambo yake binafsi.Mwisho niwapongeze sana ccm mmeonyesha ukomavu wa kisiasa na hasa Makonda, Nape na hata yule msukuma kwa kuwa wote mmekiri umuhimu wa vita hii.
Think Great in order to be a Great Thinker!!!!
 
Huwezi jua uchungu wa kuchafuliwa jina kaa kimya..sipendi wauza unga ila sipendi njia anayotumia makonda kwenye hii vita yake.
 
Swali jepesi, akitokea mtu akamtaja Makonda kuwa anahusika, je atakamatwa? Maana polisi are acting on tips from different sources? Kama hawawezi basi haya yote kuna watu wanalengwa!
Atajwe mara ngapi?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu nashindwa kuelewa nimuunge mkono mheshimiwa Makonda kwa asilimia ngapi maana anachokifanya sasa huko Dar ni jambo zuri lakini naona kama itapokuja kubainika kuna uonevu kwa baadhi ya watu itabadili taswira nzima ya azma yake njema jambo ambalo tayari lipo na limesha wagawa watu UPANDE mbili.

Mimi kama mpenda haki nikae upande upi ukizingatia na hali ilivyo sasa??
 
Hili movie ya makonda madawa ni ya kipuuzi na ita backfire kwake.

Kuwatuhumu watu na kuwaachia kwa kukosekana ushahidi haina maana bali atajiongezea maadui wengi wenye hali na mali.

Wahusika wangekamatwa na madawa kabla ya kuchafuliwa majina tungemuona konda shujaa.
 
Na hii inathibitisha ile per cent 80 iliyotaka mfumo wa chama kimoja uendelee ilikuwa sahihi.Angalia leo hii ktk vita hii ya mihadarati upinzani umekufa ganzi.Tunawaona wanaccm tu wengine wakipigana vita hii na wengine wakikosoa kwa kupendekeza njia mbadala.Nimeshangaa hata mpambanaji wa upinzani anayeaminika KC Zitto Kabwe amepigwa ganzi!Kuna nini jamani huko upinzani?Nijuavyo mimi mlango wa ruzuku ya vyama ni mmoja tu Serikali, sasa kwa nini wapinzani mnashindwa kuiunga mkono ktk hivi vita.Hata kama kutajwa kwa KUB kumewakera yule ni binadam ana mambo yake binafsi.Mwisho niwapongeze sana ccm mmeonyesha ukomavu wa kisiasa na hasa Makonda, Nape na hata yule msukuma kwa kuwa wote mmekiri umuhimu wa vita hii.
aisee ndani ya cm kuna vichwa sana..daah.. yani upinzani wa kweli upo ndani ya ccm na watu wanaongea kweli ..yani waongeaji wazuri kuliko hata hao wa upinzani
 
Kipindi fulani tulipiga sana kelele kwamba wateule wa rais wapewe instruments ili kila mmoja aelewe majukumu yake na mipaka yake.Hili halikieleweka vyema matokeo yake limefanya wakuu wa mikoa kugeuka mawaziri.

Katika kipindi cha nusu mwaka hivi kumekuwa na matukio ya hovyo sana hapa jijini Dar Es Salaam ya kulitumia jeshi la polisi katika kutekeleza matamko mbalimbali ya muheshimiwa Mkuu wa Mkoa

Ikumbukwe kwamba jeshi la polisi lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ambaye waziri wake ni Waziri Mwigulu Nchemba

Kitendo cha RC Makonda kutaka kulitumia jeshi la polisi kutekeleza matamko yake sio jambo zuri hata kidogo. Matukio ni mengi lakini mara nyingi sana Makonda ametoa maagizo kwa jeshi la polisi kufanya hiki na kile kana kwamba yeye ndiye waziri. Hii ni kutaka kuonyesha kuwa waziri Mwigulu ni waziri Uchwara jambo ambalo sio kweli.

Juzi juzi hapa alimshutumu Kamanda Sirro mbele ya hadhara kwamba anaonekana kuwabeba wauza Shisha......

Lakini pia hivi sasa kina hiki kinachoonekana vita dhidi ya madawa ya kulevya. Kiutendaji jambo hili linatakiwa kusimamiwa na waziri Mwigulu kwa kuwa anavyo vyombo vya kufanya uchunguzi na kuchukua hatua. Lakini ajabu Makonda kajimilikisha vita na kujiegeza ubavuni mwa rais Magufuli.......Huku waziri Mwigulu akiwa hana la kufanya

Jambo hili sio la kuchekewa kwani ipo siku RC atamtaka CDF aingize jeshi mtaani

Naunga mkono azimio la Bunge kuwa Ofis ya Rais awaandikie RC na DC watambue majukumu yake

RC Makonda kumpokonya madaraka Mwigulu haikubaliki

Kwani ww ndiye uliyewateua ?. Hizi ni sawa na kelele za branding na za yule mchekeshaji.
Amir jeshi Mkuu kashatoa tamko, na km huna za kujiongeza kujua nani hasa yupo behind muvu nzima basi tulia mnyolewe vizuri !!

Mlikuwa wapi siku zote au wakati ule au mliona priority ni kuzusha ugaidi, na kuwapiga watu mabomu na kuhangaikia mambo ya Yanga tuuu badala hata ya panya road ??
 
Kuna kila dalili na harufu isiyo ya kawaida ya watanzania kuyumbishwa. Watanzania wamesahaulishwa mambo yote na kugeukia 'filamu itiayo hamu' ya madawa ya kulevya chini ya muongozaji Makonda. Watanzania wamehamishwa kwenye mambo yote, hata yale ya karibu yao.

Kulikuwa na suala la mikutano ya kisiasa,mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, viwanda, Sheria ya Makosa ya Mtandao na ile iwahusuyo Wanahabari; mfumuko wa bei na matokeo mabovu ya kidato cha nne. Yote hayo yamesahaulishwa, ni madawa ya kulevya tu.

Makonda amejivika u-IGP,u-DCI,Uwaziri na Uhakimu. Ameota mapembe,analidharau hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatamba kwa kuwabamba watanzania kwakuwa wanamfuatilia. Makonda anapaswa 'kususiwa' na kudhibitiwa. Ni kwakuwa hashauriki wala haambiliki kwasasa.

Madawa ya kulevya ni jambo baya. Vita yake ni muhimu na inahitajika bila kuchoka. Lakini, aina ya vita ya kupambana na madawa ya kulevya si hii ya Makonda. Madawa huingizwa,kusafirishwa,kuuzwa na kutumiwa sirini. Iweje vita yake iwe hadharani? Kutajataja watu ni kuwachafua na kuwashtua.

Makonda, kama atang'ang'ania aina hii ya kupambana na madawa ya kulevya, anapaswa kuachwa mwenyewe. Wengine tuendelee na mambo mengine ya kitaifa. Haiwezekani wote tusombwe na 'harakati za kuigiza' na zenye kuelekea kwenye giza. Haiwezekani.

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Ila amefanikiwa sana. Lile suala la mkoa wa darisalama kuwa "kinara" kwa "kufelisha" limekosa nguvu kabisa, halisikiki tena si uraini wala bungeni!

Kuna mtu alikuwa anasema ati hata ile singo ya Darassa ('muziki') nayo chalii!😀😀😀
 
Kuna kila dalili na harufu isiyo ya kawaida ya watanzania kuyumbishwa. Watanzania wamesahaulishwa mambo yote na kugeukia 'filamu itiayo hamu' ya madawa ya kulevya chini ya muongozaji Makonda. Watanzania wamehamishwa kwenye mambo yote, hata yale ya karibu yao.

Kulikuwa na suala la mikutano ya kisiasa,mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, viwanda, Sheria ya Makosa ya Mtandao na ile iwahusuyo Wanahabari; mfumuko wa bei na matokeo mabovu ya kidato cha nne. Yote hayo yamesahaulishwa, ni madawa ya kulevya tu.

Makonda amejivika u-IGP,u-DCI,Uwaziri na Uhakimu. Ameota mapembe,analidharau hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatamba kwa kuwabamba watanzania kwakuwa wanamfuatilia. Makonda anapaswa 'kususiwa' na kudhibitiwa. Ni kwakuwa hashauriki wala haambiliki kwasasa.

Madawa ya kulevya ni jambo baya. Vita yake ni muhimu na inahitajika bila kuchoka. Lakini, aina ya vita ya kupambana na madawa ya kulevya si hii ya Makonda. Madawa huingizwa,kusafirishwa,kuuzwa na kutumiwa sirini. Iweje vita yake iwe hadharani. Kutajataja watu ni kuwachafua na kuwashtua.

Makonda, kama atang'ang'ania aina hii ya kupambana na madawa ya kulevya, anapaswa kuachwa mwenyewe. Wengine tuendelee na mambo mengine ya kitaifa. Haiwezekani wote tusombwe na 'harakati za kuigiza' na zenye kuelekea kwenye giza. Haiwezekani.

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Nafikiri Mh mkuu wa Mkoa alieleza mwanzoni kabisa sababu ya kutangaza hadharani naona wabezaji bado mnabeza bila kuja na njia mbadala,msikariri mambo ya sirisiri ndio nini?mbona mnataka kufanya hili jambo kama ni hot cake?wakati HAKUNA KINACHOSHINDIKANA CHINI YA JUA.
 
Back
Top Bottom