Mwanzo nili support hii vita ya madawa ya kulevya nikijua uchunguzi na evidence wako nazo,baada ya watu kazaa kuitwa na kuhojiwa nakufikishwa sehemu husika kujibu mashitaka,ghafla nikasikia kuwa baada ya kuwaita watu team upelelezi ya makonda /siro ndo wakaenda majumbani kwa watuhumiwa na kuambulia kukamata misokoto ya bangi nikajua hapa makonda na siro ni mchezo wanacheza, kwa hiyo ni kazi ngumu sana kumshawishi mtu akakuelewa kuwa makonda/siro wanapambana na madawa ya kulevya kwa jinsi wanavyofanya.
Pili,ni kweli wananchi wengi wanahitaji mapapa watajwe, njia ya wananchi kutuma majina kwa makonda/polis/siro ni nzuri, hata watu wengine kuomba kinga na kuhakikishiwa usalama wao pia ni safi kabisa, lakini makonda/siro baada ya kupata haya majina ilitakiwa afanye sasa uchunguzi, aunde kikosi maalum cha kuwapeleleza hao watu ili wapate evidence, na jinsi hao watu wanavyofanya biashara hiyo nchini, upepelezi huo ungeoanisha ni jinsi gani hao watu wanavyoingiza madawa nchin, jinsi gani wanavyouza, nani yuko nyuma yao, wapekuliwe mawasiliano yao,kazi zao na flow ya pesa katika account zao, mpesa , safari zao za ndani na nje, hotel ambapo hupendelea kwenda kupumzika ndani na nje ya nchi, passport zao, je wanamiliki aina ngapi za passports, majina yao kamili wanayotumia nchini na nje ya nchi, utagundua mlolongo huu wote unahitaji budget ya kutosha, unahitaji wizara mbalimbali ziweze kufanya kazi kwa pamoja , baada ya hapo ndo waje na ushahidi wa kutosha na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Tatu, siasa na pengine chuki binafsi pia lazima litazamwe, isije ikatokea kila mwenye pesa ambae amepata pesa ni muuza dawa, wengine wanfanya biashara zao kihalali na wanapata pesa ,hivyo ukimtaja yule bila kuwa na uchunguzi wa kutosha unakosea na kupelekea vita hii kukosa uhalisia. Upande wa siasa hapa pia kuna shida, Tanzania kwa sasa imegawanyika ,isije ikatokea labda katika majina yote yanayotumwa na wananchi ya wauza unga mengi ni ya chama kimoja na wahusika -wapokeaji wa majina kwa kutaka kuleta uwiano ikabidi iweke jina la mtu wa chama kingine hapo tutakuwa tunapoteza muda na hii vita itakuwa ni ngumu kushinda, maana tutahama katika vita tuingie sasa katika vyama, ndo kinachotokea sasa hivi, ili kuepusha haya yote ni lazima basi tuunde team ichunguze tena ya watalaam wetu waje na vielelzo vya kutosha kiasi kwamba hata mtu ukimwambia kwamba vielelezo na evidence za kiongozi wa upinzani kuhusika na madawa ni hizi hapa, hawa wa chama hiki nao vielezo hivi hapa, hapo wananchi bila kujali itikadi zao wata support. Hii kukulu kakala ya sasa hivi sioni kama tukifauru, yaani ni kama sasa tumewapa kibari hao wahusika kufanya hiyo kazi kwa bidii.