Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Vita dhidi ya Dawa za Kulevya awamu ya Pili: RC Makonda awataja Mbowe, Manji, Gwajima, Idd Azzan...

Kuna kila dalili na harufu isiyo ya kawaida ya watanzania kuyumbishwa. Watanzania wamesahaulishwa mambo yote na kugeukia 'filamu itiayo hamu' ya madawa ya kulevya chini ya muongozaji Makonda. Watanzania wamehamishwa kwenye mambo yote, hata yale ya karibu yao.

Kulikuwa na suala la mikutano ya kisiasa,mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, viwanda, Sheria ya Makosa ya Mtandao na ile iwahusuyo Wanahabari; mfumuko wa bei na matokeo mabovu ya kidato cha nne. Yote hayo yamesahaulishwa, ni madawa ya kulevya tu.

Makonda amejivika u-IGP,u-DCI,Uwaziri na Uhakimu. Ameota mapembe,analidharau hata Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anatamba kwa kuwabamba watanzania kwakuwa wanamfuatilia. Makonda anapaswa 'kususiwa' na kudhibitiwa. Ni kwakuwa hashauriki wala haambiliki kwasasa.

Madawa ya kulevya ni jambo baya. Vita yake ni muhimu na inahitajika bila kuchoka. Lakini, aina ya vita ya kupambana na madawa ya kulevya si hii ya Makonda. Madawa huingizwa,kusafirishwa,kuuzwa na kutumiwa sirini. Iweje vita yake iwe hadharani. Kutajataja watu ni kuwachafua na kuwashtua.

Makonda, kama atang'ang'ania aina hii ya kupambana na madawa ya kulevya, anapaswa kuachwa mwenyewe. Wengine tuendelee na mambo mengine ya kitaifa. Haiwezekani wote tusombwe na 'harakati za kuigiza' na zenye kuelekea kwenye giza. Haiwezekani.

Mwafaaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Kajivika u-IGP, u-DCI, na Uwaziri na Uhakimu. Kama hao wote walikuwepo una maana madawa ya kulevya hayapo? au bado wanapambana "SIRINI"
 
Sasa umeanika sura yako halisi hadharani. Iwe unaishi Lumumba au Ufipa, sura yako halisi ndio hiyo ya sasa. Hufungi mtu kamba tena.
 
Ukiondoa rais na viongozi wa dini, nani mwingine ameonyesha dalili ya kumuunga mkono makonda zaidi ya kumkatisha tamaa, kila anaetajwa mnadai anachafuliwa, kama anachafuliwa basi watajeni hao ambao ni kweli wanauza ili kuepuka wengine kuchafuliwa.

vinginevyo, pigeni kimya na kujifanya mnajua sana taratibu. vijana wanazidi kuangamia, kila atakaempinga makonda bora atiwe ndani.
 
Umeandika kw kutumia beat ya mziki ya Darassa[emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Uko sahihi. Ni kutafuta popularity tu si kingine. Mbaya zaidi imeingizwa na siasa, ni kawaida kwa CCM.
 
Wanatumia nguvu kidogo sana kupambana na upinzani. Turudishe ukuta watumie nguvu nyingi mpaka wachoke.
 
Nafikiri Mh mkuu wa Mkoa alieleza mwanzoni kabisa sababu ya kutangaza hadharani naona wabezaji bado mnabeza bila kuja na njia mbadala,msikariri mambo ya sirisiri ndio nini?mbona mnataka kufanya hili jambo kama ni hot cake?wakati HAKUNA KINACHOSHINDIKANA CHINI YA JUA.
Kama hakuna kinachoshindikana waulizeni USA wanashindwaje msipende kujipa matumaini hewa,, kama unataka Kumaliza madawa malizeni dini na elekeeni kuomba misaada kwa ulluminat huenda mkafanikiwa. Fikra huru
 
Kama hakuna kinachoshindikana waulizeni USA wanashindwaje msipende kujipa matumaini hewa,, kama unataka Kumaliza madawa malizeni dini na elekeeni kuomba misaada kwa ulluminat huenda mkafanikiwa. Fikra huru
hii ni Tanzania unaizungumziaje USA???????
 
Ktk harakati zinazoendesha na mkuu wa mkoa wetu Paul Makonda ni wazi kuwa watanzania tumesimama ktk misingi ya vyama vyetu, dini zetu, team zetu na kuacha taifa likiangamia na madawa ya kulevya!

Wengi wetu tumekuwa tukipinga na kusema kuwa approach anayotumia mh sio sahihi!

Iwe sahihi isiwe sahihi sisi tuungane pamoja kutafuta hiyo sahihi kwani mabadiliko yanaanza na wewe tusiache vijana wetu wapoteze mustakabali wao kisa ushabiki wetu na mwisho tukumbuke kuwa ktk vita hii makonda akishindwa ndio tumefungulia geti la madawa dar na tz kwa ujumla.
 
Mwanzo nili support hii vita ya madawa ya kulevya nikijua uchunguzi na evidence wako nazo,baada ya watu kazaa kuitwa na kuhojiwa nakufikishwa sehemu husika kujibu mashitaka,ghafla nikasikia kuwa baada ya kuwaita watu team upelelezi ya makonda /siro ndo wakaenda majumbani kwa watuhumiwa na kuambulia kukamata misokoto ya bangi nikajua hapa makonda na siro ni mchezo wanacheza, kwa hiyo ni kazi ngumu sana kumshawishi mtu akakuelewa kuwa makonda/siro wanapambana na madawa ya kulevya kwa jinsi wanavyofanya.

Pili,ni kweli wananchi wengi wanahitaji mapapa watajwe, njia ya wananchi kutuma majina kwa makonda/polis/siro ni nzuri, hata watu wengine kuomba kinga na kuhakikishiwa usalama wao pia ni safi kabisa, lakini makonda/siro baada ya kupata haya majina ilitakiwa afanye sasa uchunguzi, aunde kikosi maalum cha kuwapeleleza hao watu ili wapate evidence, na jinsi hao watu wanavyofanya biashara hiyo nchini, upepelezi huo ungeoanisha ni jinsi gani hao watu wanavyoingiza madawa nchin, jinsi gani wanavyouza, nani yuko nyuma yao, wapekuliwe mawasiliano yao,kazi zao na flow ya pesa katika account zao, mpesa , safari zao za ndani na nje, hotel ambapo hupendelea kwenda kupumzika ndani na nje ya nchi, passport zao, je wanamiliki aina ngapi za passports, majina yao kamili wanayotumia nchini na nje ya nchi, utagundua mlolongo huu wote unahitaji budget ya kutosha, unahitaji wizara mbalimbali ziweze kufanya kazi kwa pamoja , baada ya hapo ndo waje na ushahidi wa kutosha na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Tatu, siasa na pengine chuki binafsi pia lazima litazamwe, isije ikatokea kila mwenye pesa ambae amepata pesa ni muuza dawa, wengine wanfanya biashara zao kihalali na wanapata pesa ,hivyo ukimtaja yule bila kuwa na uchunguzi wa kutosha unakosea na kupelekea vita hii kukosa uhalisia. Upande wa siasa hapa pia kuna shida, Tanzania kwa sasa imegawanyika ,isije ikatokea labda katika majina yote yanayotumwa na wananchi ya wauza unga mengi ni ya chama kimoja na wahusika -wapokeaji wa majina kwa kutaka kuleta uwiano ikabidi iweke jina la mtu wa chama kingine hapo tutakuwa tunapoteza muda na hii vita itakuwa ni ngumu kushinda, maana tutahama katika vita tuingie sasa katika vyama, ndo kinachotokea sasa hivi, ili kuepusha haya yote ni lazima basi tuunde team ichunguze tena ya watalaam wetu waje na vielelzo vya kutosha kiasi kwamba hata mtu ukimwambia kwamba vielelezo na evidence za kiongozi wa upinzani kuhusika na madawa ni hizi hapa, hawa wa chama hiki nao vielezo hivi hapa, hapo wananchi bila kujali itikadi zao wata support. Hii kukulu kakala ya sasa hivi sioni kama tukifauru, yaani ni kama sasa tumewapa kibari hao wahusika kufanya hiyo kazi kwa bidii.
 
Kuongea juu ya rais sio kutokumuheshimu,
nadhani ukiwa kiongozi ni vema ukajiandaa na mambo kama hayo.
Na wabunge pia kama viongozi wanatakiwa wajiandae na mambo kama hayo asiwe rais pekee wa kujiandaa
 
atakuwa mubashara azam tv[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji4]
 
Back
Top Bottom