Marejeo ya nyuma
Hali inayoendelea Mashariki ya Kati. Hoja zilizojadiliwa na maswali yatokanayo.
1. Kwamba, Iran inapigana na USA, UK, EU , UAE na Arab World Australia na Israel na waliojificha
Kabla ya vita, Saud Arabia na Kuwaiti walidai kutotoa ardhi kwa mashambulizi.
Ukweli kwamba kambi za Marekani zinapanga mipango yao ndani ya nchi hizo, huo ni usaidizi
Iran haikushambulia majirani , inashambulia maeneo ya masilahi ya US na Israel. Masilahi ni kambi za kijeshi na maeneo yanayotumika kijeshi kama Balozi. Shambulio la Iran kwa Ufaransa (Iraq) lilenga kambi zinazotoa usaidizi
2. Iran haipigani vita kushinda bali ku survive kwasababu inapigana na mataifa makubwa kiuchumi, na Kiteknolojia. Hadi siku 21 Iran ikiwa imesimama tena ikitoa masharti ya kusitisha vita ni jambo linaloshtua dunia
3. Hii si vita ya dini lakini dini inatumika. USA wamevamia Venezuela, wametaka Greenland, wamezodoa Canada na wanaelekea Cuba. Nchi zote ni za Kikristo kwa wingi wa waumini. Ikiwa dini ni kigezo basi zisingeshambulia
US na Israel zimeweka kambi Kuwait, Qatar, UAE, Saud Arabia, Oman n.k. Hizo ni nchi za ''Kiislam'' ili kumshambulia Iran ambaye ni Nchi ya Kiislam. Ingalikuwa vita ni ya dini hilo lisingetokea
Hata hivyo dini inatumiwa na USA/ Israel kuwagawa Waarabu na Waajemi. Kwa mfano, kuita Islamic republic regime nadictator wa IRGC (Islamic revolutionary Guard council) wanaingiza neno Islam kujenga miongoni mwa nchi za Magharibi kwamba wanapigana na ''Ugaidi''
Utasikia wakisema , Iran ina sponsor magaidi wa Hezebollah na Hamas. Lengo ni kuunganisha Iran na Ugaidi.
Ikiwa ku support makundi (Proxies) kama Houthi, Hezbollah na Hamas ni ugaidi, mbona Israel imemsaidia Jailani wa Syria ambaye ni Gaidi wa Aqaeda katika orodha ya CIA kumuondoa Assad!
Je, kuweka kambi za kijeshi UAE, Cyprus, Saud , Qatar hizo siyo proxies za US na Israel kumshambulia Iran?
3. Je suala ni mafuta? US walipovamia Venezuela suala la rasilimali ya mafuta lina ukweli ingawa si wote.
Venezuela ina utajiri wa mafuta na mshirika wa Russia, China, Iran na Cuba. US kuvamia ni njia ya kukata mirija ya mafuta kwenda China! ili kudhoofisha uchumi. Iran kama Venezuela ni wasaidizi wa China kwa mafuta. Kutawala Iran ni kudhoofisha China kiuchumi
4. Je, Israel inataka kujitanua? Hili lina ukweli ingawa si wote. Israel ina ndoto ya ''great Israel'' ikichukua nchi za mashriki ya Kati. Wapalestina wanaondolewa maeneo yao . Vita inaendelea Lebanon kuchukua Lebanon kusini. Syria ilishapoteza Golan na eneo la Magharibi. Jordan naye ni muathirika tu. Nchi inayoonekana kikwazo ni Iran
Iran ni kikwazo kwasababu ya uwezo wake kielimu ukilinganisha na nchi zote za mashariki ya Kati.
Kwa mfano, Iran naongoza katika eneo la Sayansi za anga na hata za kilimo na madawa. Dunia inashuhudia baada ya miaka 40 ya vikwazo vya uchumi, Iran imesimama kidedea siyo na Israel bali mataifa zaidi ya 15.
Israel iliona hatari hiyo ndiyo maana ilisingizia suala la Nuclear
Israel ilijua ikiwa Iran itapata uwezo wa Nuclear , haitaweza kusihambulia tena. Ni kama vile North Korea haiguswi, Pakistan au India. Shinikizo ni kumpiga na Iran ili kumdhoofisha na kutawala Iran kwa remote wala si Nuclear.
Ni nani anatoa vibali vya nchi kuwa na Nuclear?
Iran ilisaini mkataba wa non proliferation, Israel haikusiani.Israel ina Nuclear , Iran haina.
Ushahidi umetolewa na Mwisrael aliyehusika na utengeneza, Modechai Vanunu.
Leo tumeona Dimona ikshambuliwa baada ya Israel kushambulia kinu cha Natanz Iran.
Hali ipoje? Tutafafanua