Vita Mashariki ya Kati. US-Israel-Washirika dhidi ya Waajemi (Iran)

Vita Mashariki ya Kati. US-Israel-Washirika dhidi ya Waajemi (Iran)

Charles na Itikadi kali
Kama tulivyoeleza, Charles wa Wasafi anaposema Iran ina itikadi kali ana maanisha ''ugaidi''.
Kinyume chake hakuna maelezo ya maana itikadi kali ni kitu gani

Kuna dhana kwamba Iran ina sponsor vikundi vya kigaidi mashariki ya kati. Vkundi hivyo ni Houthi , Hezbollah na Hamas. Makundi hayo yameitwa ya kigaidi na Marekani na washirika na wengi huamini bila chembe ya fikra.

Tukitazama maana ya Ugaidi kwanini Iran inashutumiwa kusaidia makundi hayo?

Kwanza, Hamas haijawahi kushambulia eneo jingine nje ya Gaza. Hamas ni kundi lililofadhiliwa na Israel ili kuvuruga kundi la Fatah linalotawala West Bank. Miaka mingi Israel imetoa pesa kwa Hamas hadi Oktoba 07.
In fact miezi michache kabla ya shambulio pesa zilihamishwa kupitia Qatar kufikia Hamas

Kundi la Hezbollah ni matokeo ya Israel kujitanua eneo la Lebanon kusini, ndio mwanzo wa kuundwa Hezbollah. Hakuna siku Hezbollah imepigana nje ya kusini la Lebanon

Houth: Hawa ni washirika wa Iran kwa imani , nao kama Iran ni watetezi wa Palestina. Vita yao ipo Yemen .
Houthi hawajawahi kushambulia nchi nyingine zaidi ya Saud Arabia inayowashambulia.

Kwa kuangalihayo, ni vipi watu waseme ni ya kigaidi au itikadi kali kama anavyosema Charles wa Wasafi FM?

Tuangazie Iran: Tangu vita na Iraq iliyotamati mwaka 1984 Iran haijashambulia Taifa jingine lolote hadi majuzi iliposhambuliwa na Israel na Marekani. Iran inashambulia majirani kwasababu mashambulizi dhidi yake yanatokea nchi hizo. Ushahidi upo hadi leo ambapo askari wa Marekani wameuawa Bahrain na Kuwait.

Ikiwa Israel ina haki ya kujilinda, kwanini Iran isiwe na haki kama hiyo.

Tuangazie Israel: Imeshambulia nchi nyingine mara nyingi mashariki ya kati. Mwaka jana peke yake, Israel ilipiga nchi 7 ikiwemo shambulizi kwa nchi kama Qatar wakati wa usuluhishi.

Israel imesaidia kundi la Kigaidi la Syaria kiliongozwa na Gaidi katika orodha ya CIA kuwa Rais wa Syria.

Jana, Iran imeshambulia milima wanayoishi Kurdi wanaofadhaliwa na Israel na Marekani kushambulia Iran.
Moto uliunguza maghala ya Silaha. Rais Trump alikiri kwamba kundi la Kurdi lilipewa silaha likauza badala ya kutumia katika mashambulizi nchini Iran na Iraq maeneo ya Shia

Rais Trump amesema kwamba Marekani kwa kushirikiana na Israel walituma watu wao ndani ya Iran kuleta machafuko ili kuangusha utawala wa Khamenei.

Israel inaunga mkono waasi wa Somaliland, nchi pekee Duniani inayowatambua Wasomali hao

Israel ilitumia Passport za nchi za Magharibi kumuua kiongozi wa Hamas Hotelini UAE

Israel na Marekani zikamuua Qassam Soleiman wa Iran akiwa nchini Iraq

Marekani imevamia Venezuela na sasa inataka kuvamia Cuba.

Orodha inaendelea

Swali kwa Bwana Charles Williams wa Waasafi, ni nani mwenye itikadi kali ? Iran au Marekani / Israel?
 
Vita ya Mashiriki ya kati inaelekea kubaya
Iran yawataka Raia wa Israel kuondoka. Netanyahu aimbia Iran silaha chini au kutana na kifo


Ni Piga nikupige ya Marekani na Iran baada ya kupoa siku 5. Iran inazivuruga kambi za kijeshi za Marekani.
Iran inabadili mwelekeo, inawinda Askari za Marekani baada ya taarifa kwamba Marekani inakabiliwa na upungu wa silaha za kuzuia makombora. Vifo vya askari wa Marekani vimeongeza shinikizo la ndani ya Marekani

Marekani ina lengo la kuvunja madaraja, na miundo mbinu ya nishati na usafirishaji kuihujumu Iran kiuchumi.
Licha ya mabomu kwa siku 14 mfululizo, Iran inajibu na kuanzisha mashambulizi, si kulipa kisasi.

Rais Trump anatamani kumaliza suala la Mashriki ya Kati. Mtihani ni Israel inayotoka vita iendelee.
Inaelezwa kwamba kuna mpango wa kushambulia milima yenye kuhifadhi Uranium ya Iran.
Waziri mkuu Netanyahu alikuwa Washington na hiyo ikiwa agenda

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema wangeshambulia maeneo ya nishati ya Iran lakini wanazuiwa na Marekani kwa kuchelea kwamba vita itaenea zaaidi. Zaidi ya hilo, Israel inaelewa kwamba haina uwezo wa kuzuia makombora ya Iran!!! Kambi za Marekani zinazotoa kinga ya anga zimeharibiwa

Iran imeshambulia miundo mbinu ya majirani wanaoweka kambi za Marekani kama Kuwait, Bahrain, UAE, Qatar n.k. na kufungwa kwa mlango wa Hormuz hali ya mafuta ni mbaya duniani, Marekani akilaumiwa

Ikiwa Israel itashambulia maeneo ya nishati , Iran itajibu kwa nchi za kiarabu zisizoridhishwa na ulinzi wa Marekani kama ilivyo waahidi. Wananchi wanataka Marekani iondoe kambi katika nchi zao

Majuzi, Waziri Mkuu Netanyahu alitemebelea kinu cha Nuclear cha Dimona kilichopigwa na Iran mwaka jana. BB akasema ikiwa Iran itatenda tena Israel itajibu vikali. Hii inaonyesha ukubwa wa shambulio la Iran.

Siku moja baadaye Iran ikawataka Raia wa Israel waondoke nchini humo kwa usalama wao.
Jana, Netanyahu kasema Wairan waweke silaha chini au wakabiliane na kifo

Kuna tafsiri kadhaa! Moja, Israel inatambua ulinzi wa anga haupo na uwezekano wa kupigwa tena ni mkubwa.Kambi za Marekani zenye radar za kuilinda Israel zimefumuliwa.

Pili, Netanyahu ima anafikiri kupiga miundo mbinu ya mafuta , Madaraja, Hospitali na mashule tena au anafikiria kutumia Nuclear. Kwa hali ilivyo vita vimeielemea Israel na inafikiria option nyingine ikiwemo Nuclear

Kauli ya kwamba Israel ita surprise Iran imetishia ! kinachoonekana ni matumizi ya Nuclear iwe popote pale Iran au katika milima inayohifadhi Uranium. Hata hivyo majibu ya Iran yanaweza kuwa mabaya kuliko inavyokadiriwa
 
Iran yaishika Marekani pabaya, Trump akataa ombi la ku 'nuke' Iran

Baada ya mashambulizi ya siku 14 mfululizo ya majeshi ya Marekani, Iran ilijibu kwa mashambulizi 2 yaliyovuruga kambi za Marekani mashariki ya kati na kupelekea vifo na majeruhi. Hilo limeilazimu Marekani kusitisha mashambulizi kwa muda kuepuka uharibifu kutokan na majibu.

Mpango wa kushambulia miundo mbinu ya Iran ulisitishwa dakika za mwisho kwa ombi la Saud Arabia na UAE . Nchi hizo ziliahidiwa na Iran kwamba ikishambuliwa itazishambulia.

Ni dhahiri, Iran inaposema inatenda. Nchi za Mashariki ya kati hazina shaka kuhusu Iran kama Super power.

Iran imeshikilia kivuko cha Hormuz na Marekani imezuia kwa upande mwingine. Bei za mafuta zinapanda na kuongeza gharama za uzalishaji kutokana na ''inflation''.

Lawama hizo anabeba Rais Trump aliyeanzisha vita akidhani Iran ni sawa na Venezuela.
Kwasasa Trump anatafuta pa kutokea, anaomba mazungumzo. Iran inaonyesha kiburi cha masharti mezani

Israel inasema itaendelea kuishambulia Iran bila ruhusa ya Marekani. Gazeti la Wall street journal linaripoti kwamba Israel ilimshauri Trump atumie silaha za 'Nuclear'' kufumua milima inayosadikiwa kuhifadhi Uraniun.

Rais Trump anasemekana kukataa akijuakinachoendelea sasa ni matokeo ya kuingizwa mkenge na Israel.

Wazo la ''Nuke'' linaeleza kwamba, maji ni marefu kwa Israel. Kwamba, ilidhani inapigana na Wanamgambo wa Hezbollah ambao pia wanawapa tabu au kudhani ni Gaza wanapopiga mabomu kwa ndege.

Zile tambo za Israel kurusha ndege zikiwa na Wanawake hazionekani tena kwasababu hata kwenye meza ya mazungumzo Israel haipo. Tunazidi kupata majibu ya maswali ya siku nyingi ikiwa Israel ni super power kweli.

Nchi za Kiarabu zimejisalimisha tayari. Kuna mkataba wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Saud Arabia, Turkey na Pakistan. Kwamba mmoja akishambuliwa wote wameshambuliwa.

Jambo hilo linahusu mambo mawili, kwanza, kukabiliana na tishio la Iran na pili tishio la Israel kutumia Nuclear. Pakistan ina Nuclear kama Israel hivyo kutoa kinga kwa washirika wake.

InawezekanaMarekani na Israel zinajipanga kwa shambulio la kushtukiza kwasababu kila zinapozidiwa huomba ''pause'' zijikusanye. Kwanini Iran inaruhusu hali hiyo? Ni mkakati wa vita wa kuto toa siri na silaha muhimu za kukabiliana na adui pindi atakaporejea. Mathalani kambi za Marekani zimeunguzwa, kuna haja gani ya kupiga vibanda vingine kwa kujua satelite za Marekani zitaonyesha wapi mashambulizi yanapotokea!

Vita si silaha tu, ni akili pia
 
SS LINCOLN NA ADHA YA IRAN
Mtakumbuka vIran ilidai kuipiga Manowari ya SS Gerald Ford. Habari zilikanushwa kwa madai kwamba uharibifu ulisababishwa na hitilafu ya umeme chumba cha kusafishia nguo (Laundry).

Baadaye ilibainika kwamba drone za Iran zilipiga meli hiyo na kuhitaji matengenezo ya zaidi ya mwaka na nusu.

Habari za wiki hii ni kuhusu hali mbaya ndani ya Manowari ya SS Lincoln ikieleza askari wanavyotamani kujirusha wafe kutokana na hali mbaya. Kuna tukio la askari kuokolewa baada ya kujirusha majini.
Habari zinatolewa na askari ndani ya Manowari na ndugu zkieleza foleni za kahawa, upungufu wa toilet paper n.k.

Wengi wanadhani ni uzembe wa Serikali ya Trump kutopeleka mahitaji (supplies). Ukweli ni kwamba madhara ya mashambulizi ya Iran yanajitokeza.

Iran ilijipanga kwa vita ya muda mrefu ikielewa nguvu za Marekani na Israel zipo katika vita ya mara moja kwa kutumia nguvu nyingi. Kama mtakumbuka Iran ilianza kupiga majirani wanaohifadhi ''assets'' za Marekani.
Wengi hawakuelewa ni kwanini lakini sasa wataelewa

Iran ilipiga bandari ya Oman, nchi ambayo ni mshirika wake katika usuluhishi. Bandari ilikuwa ni kwa kupokea mizigo ya Marekani inayokwenda vituo mbali mbali mashariki ya kati. Iran ikapiga kambi ya 5th fleet HQ Bahrain kituo kikuu cha wanamaji wa Marekani mashairki ya kati

Kabla ya hayo Iran ilipiga radar muhimu za Marekani mashariki ya kati ili kuzuia majibu na kupeleka kiwewe.
Marekani na Israel zikabadili mwelekeo wa kutumia ndege zikawa zinatuma makombora ya Toma Hawk.

Kilichofanywa na Iran ilikuwa kuvunja miundo mbinu (Logistics infrastructure) za Marekani kukata supplies. Madhara ni Manowari kutokuwa na supplies achilia mbali upungufu wa makombora ya kujikinga dhidi ya Iran

Mapigo ya Marekani kwa siku 14 mfululizo yalilenga kuilazimisha Iran kusalim amri lakini Iran ilikuwa na plan yake

Shambulio moja dhidi ya King Faisal camp kule Jordan lilisababisha vifo na majeruhi wa Marekani.
Ndio kambi ya mwisho kabla ya Israel na hivyo Israel iliachwa bila ulinzi wa Marekani.

Hizo ndizo sababu Marekani kusimamisha vita kwa muda ili kujiweka sawa kwababu hali ya vita imewaelemea

Mpango wa Marekani na Israel ni kupata wapi Uranium zilipo walipue na kukimbia wakitangaza lengo limetimia ili kuepuka vipigo wa Waajemi.

Marekani na Israel zinaitambua Iran kama Super power kwasababu licha ya vikwazo vya miaka 40 bado Waajemi wamesimama wenyewe kidete dhidi ya Marekani na wala si Irael. Laiti ingalikuwa Israel peke yake vita ingakuwa imekwisha miezi mitano iliypita!
 
VIKWAZO VYA UCHUMI KWA IRAN

Rais Trump ametangaza vikwazo vikali vya uchumi dhidi ya Iran akiviita ''economic D-Day''.
D-Day ni siku ya vita kuu ya pili majeshi ya washirika yalipopambana na Ujerumani kule Ufaransa
Waziri Mkuu Netanyah naye kaitaka Marekani iongoze vikwazo vya uchumi zaidi dhidi ya Iran

Ukali wa vikwazo hivyo tofauti na vile vya miaka 46 ambavyo pia vilikuwa vikali ni kuonya nchi nyingine zifanye biashara na Iran. Trump ametishia kwamba nchi itakayobainika itawekewa vikwazo na Marekani.

Kwa maneno mengine, Trump anaomba msaada wa Dunia kuimaliza Iran kwasababu vikwazo vya miaka 46 havijafanya kazi, mashambulizi ya anga hayajafanya kazi, makombora kutoka Baharini hayajafanya kazi

Yote hayo ni pamoja na usaidizi wa Israel, UK, Ufaransa, Australia na nchi za Kiarabu.
Hakuna Taifa linalotamani kupeleka askari wake baada ya kambi zaidi ya 16 za Marekani kufutwa kabisa mashariki ya kati na Israel kupokea kipigo kilichoilazimisha kuunda sheria ya kutopiga picha miji ya nchi hiyo

Vikwazo vinavyosemwa vimekataliwa na Urusi na China ambao ni washirika wakubwa wa Iran kibishara.
Marekani ililenga nchi za UAE, Pakistan , China na Urusi ili kuidhoofisha Iran kiuchumi licha ya miaka 46 ya hali hiyo

Hii ina maana moja, Iran amefanikiwa ! kivuko cha Hormuz kipo mikononi mwao na Marekani hawana la kufanya.

Tunazungumzia Marekani kwasababu Israel iliyoanzisha vita haiwezi kusimama na Iran peke yake na katika hatua ya sasa hakuna mjadala unaoihusisha kwasababu hakuna sababu

Vyombo vya magharibi havielezi nini kinaendelea kwasababu mahususi, ni vya propaganda ambavyo wamiliki wake ni Wazayuni. Mfano, Iran inamiliki eneo la Kurdistan kule Iraq. Mpango wa Marekani na Israel kushambulia ardhini kutokea Kurdi umefeli, kambi za Wakurdi zimebomelewa , Marekani wameondoa vifaa

Vita ya Iran na Marekani imetoa mafunzo mengi hasa kwa wapuuzi wa dini. Kuna wanaoamini kwamba bila kuipigania Israel hata kwa maovu ni kuukana Ukristo jambo lisilo la kweli. Ukristo hauna uhusiano na Zionism.

Vile vile wapo wanaodhani Iran ipiganiwe kwasababu ni Waislam! ni wapuuzi, wanaoandaa mazingira ya Iran kupigwa ni Waislam wa Saud Arabia, UAE, Oman, Kuwait na Bahrain wakitoa ardhi zao zitumike

Upuuzi wa imani umepelekea hata wenye ufahamu kama akina Makalala wa The citizen kutumbukia ndani. Ukimsikiliza Mwanahistoria Mzee Said hai ni hiyo hiyo!

Vita inayopiganwa Iran ni ya masilahi ya Nchi za Magharibi kutokana na utajiri na nafasi ya Iran mashariki ya kati.
Ni vita ya Hegemony! ambayo Iran ameonyesha kuwa msumbufu

Ukweli upo wazi, Iran ni super power middle east si Israel kama alivyoandika Makalala kwa miaka mingi! akiwataka Waarabu wakubaliane na matakwa ya Israel na Wapalestina waache vita! yaani ardhi yao ichukuliwe tu.
Hoja zake ni kuhusu Israel kama msingi wa Imani yake na si hali ya mambo! tunasubiri makala zake!
 
Hali mashariki ya Kati ni tata zaidi
Houthi waongeza changamoto mashariki ya Kati


Baada ya ukimya wa wiki kadhaa , Marekani ilishambulia meli 4 za Iran zilizojaribu kupita lango la Hormuz
Iran ikajibu mapigo katika kambi za Marekani katika nchi za Kiarabu na kubwa zaidi nchini Jordan

Vifaa vya kijeshi vya Marekani zikiwemo ndege viliharibiwa na makombora ya kuzuia yakitumika mengi

Tukio la kushangaza ni Iran kuiteka nyambizi ya drone ya Marekani iliyokuwa ikifanya doria eneo la Hormuz
Nyambizi ilitekwa bila uharibifu kwa maana Iran iliingilia mawasiliano na kuiamru ielekee upande wao.
Kuiteka ikiwa nzima ina maana moja, watafanya ''reverse engineering' ili kubaini ilitengenezwaje

Marekani imesema nyambizi ni ya Teknolojia ya zamani bila taarifa muhimu lakini laiti isingekuwa , isingeweza kuwekwa Hormuz kwa majaribio. Na zaidi Teknolojia ya zamani itakuwa na mwendelezo wa generation za sasa.

Hii si mara ya kwanza kwa Iran kutumia Teknolojia kunasa vifaa vya Marekani. Wakati wa Rais Obama Iran iliteremsha drone ya ghali ya Marekani kwa kuingilia mifumo ya mawasiliano.

Gharama za utekaji wa vifaa ni kuruhusu mahasimu kama China, Korea kasakazini au Urusi kupata Tecknolojia za Marekani na kuzidurusu '' reverse engineering' kwa kiwango cha juu zaidi.

Houthi wateka miji muhimu Yemen
Wakati vita ikirindima, Wahouthi wa Yemen wameteka mji katika mlango wa bahari ya Sham (Red sea) uitwao Mocha na kisiwa karibu na lango la Bab el Mandeb. Houthi sasa wana udhibiti wa lango la bahari ya Sham na Iran ikidhibiti lango la Hormuz, maeneo muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Houthi kwa namna ya mkakati wamesema meli zinaruhusiwa kupita isipokuwa za Saud Arabia, ili dunia isiwageukie kwasababu ya adha ya mafuta wakati huo huo wakiitesa Saud Arabia

Saud Arabia imesaidia serikali ya Yemen dhidi ya Houthi marafiki wa Iran. Houthi sasa wanashambulia Saud Arabia kwa kutumia vifaa vya kijeshi vya Marekani. Marekani imekataa ombi la kuwasaidia

Kwa Marekani kuna sababu za kutoshiriki vita hivyo kwa kuzingatia hali mbaya wanayokabiliana nayo Iran

Presha inaongezeka kwa Rais Trump baada ya vifaa kutekwa na Houthi. Ukweli, ni vifaa vilivyotengenezwa Marekani na kununuliwa na Saud Arabia. Kwa macho ya Wananchi ni vifaa vya jeshi la Marekani na wanaona Jeshi kudhalilika kwa kupigwa na wavaa makobazi. Hilo tu linampa Trump presha

Presha ya pili ni kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani baada ya lango la Bab el mandeb kudhitiwa na Houthi na kulipuliwa bomba la mafuta kutoka Saud kwenda Bahari ya Sham.

Dunia inaingia gharama kwasababu ya Marekani na Trump hapendi kulaumiwa au kuonekana ameshindwa.
Iran inafaidika sana na hali hiyo kwa kuiweka Marekani katika ''tatizo la kiuchumi'' si ndani bali Duniani

Israel na Houthi
Kwa upande wa Israel, kutekwa kwa mji wa Mocha na udhibiti wa mlango wa Bab el Mandeb ni pigo.
Kumbuka, Houthi kwa msaada wa Iran wamewahi kuwashambulia Israel.

Kuna wakati Israel iliua baraza lote la Mawaziri la Houthi na kiongozi wao lakini leo wamesimama wima.

Houthi ni sehemu ya Axis of resistance inayohusisha Iran, Hezbollah, Hamas na Houthi
Israel ilitambua Somaliland eneo linalopakana na Bahari ya Sham kwa maana kwamba ni Bab el Mandeb upande wa pili takribani KM 24 kuvuka bahari.

Israel ilitambua Somaliland ili ipate access ya ushirika kuwadhibiti
Houthi wanadhibiti mji wa Mocha unaotazamana na Somaliland ukitenganishwa na Bab el Mandeb
Ikiwa Israel itatumia Somaliland kudhibiti Houthi, vita itakuwa kati ya Houthi na Somaliland

Swali linabaki ikiwa Pakistan na Turkiye zinaweza kuwasaidia Saud Arabia kufuatia mkataba wa Mecca unaojulikana kama Mecca accord unaosema attack on one is an attack on all!

Kwa pande wa vita ya Iran, Marekani inalazimika zaidi kumaliza vita isiendelee kuadhirika na pili kutokuwa sababu ya bei za mafuta kupanda duniani.

Tayari Trump ameanza kuzungumzia ''mazungumzo'' kwamba Iran wanataka ingawa tunajua anajaribu kuomba. Iran wamekataa wakisema zile point 10 za mkataba wa awali zifuatwe vingienvyo ni vita tu!
 
Houthi washambulia Saud Arabia, hali yazidi kuwa tete mashariki ya Kati

Wiki iliyopita Iran na Qatar waliitisha mkutano wa nchi za Gulf kujadili mustakabali wa mashariki ya Kati ikiwa ni pamoja na kivuko cha Hormuz . Dakika za mwisho za maandalizi Saud Arabia ikakataa, kikao kikaahirishwa

Nyuma ya pazia Saud Arabia, Marekani na nchi za Gulf zilikuwa na kikao na Marekani chini ya Trump.
Mpango ulipangwa wakati wa kikao cha baraza kuu la umoja wa mataifa kama zile ''side meetings'' za kawaida

Mtakumbuka Iran imeshambulia kambi za Marekani kaunzia Jordan, Saud Arabia, UAE n.k..
Iran ilifanya makusudi ikijua kiburi cha nchi za Kiarabuna Israel ni uwepo wa kambi za Marekani.

Majuzi tu kambi muhimu zilifumuliwa na kuiacha Marekani ikiwa haina kambi bali kukimbiza vifaa kuficha

Matakumbuka pia wakati wa mazishi ya kiongozi wa Iran Ali Khamenei ndege ya Iran ikiwa na abairia ilizuiliwa kutua Yemen baada ya Saud Arabia kubomoa uwanja wa ndege, ikatua uwanja mwingine.

Taarifa zinasema 'abiria' walikuwa makamanda wa Iran kikosi cha IRGC kwenda kwa kutoa msaada kwa Houthi.
Wiki iliyopita dereya na vifaa vilivyotumiwa na Saud Arabia vilitekelezwa baada ya Houthi kushambulia vikali.

Houthi kwa taarifa tu ni jina la ukoo wa mwanzilishi wa kundi aliyeitwa Hussein Badrredin Al Houthi aliyeuawa 2004. Lengo la Houthi lilikuwa kulinda jamii ya Zaydi dhidi ya serikali ya Sunni iliyoungwa mkono na Saud Arabia.

Houthi ni ''Washia nusu'' wakiungwa mkono na Iran. Kundi hilo jina lake halisi ni Ansar Allah likosomwa (Ansar-allah) likimaanisha '' supporter of Allah'' au waliojitweza kwa mwenyezi mungu.

Kinachotekea sasa ni mashambulizi katika miji ya Saud Arabia kwasababu hakuna ulinzi wa Marekani.
Iran inatumia nafasi hiyo kwasababu kikao ilichotaka kilikataliwa na Waarabu ili kuwa na muafaka na Marekani.
Iran inamuonyesha Saud Arabia na nchi za Gulf kwamba Marekani hana usaidizi tena kwao

Watu wanaojiuliza Houthi wanapata wapi nguvu waelewe Iran ilipofumua kambi za Marekani ilikuwa na sababu.

Israel ina hofu kwasababu hakuna ngome iliyobaki. Kambi zilizokuwa zinailinda kule Jordan na Arab zimepigwa.

Waziri mkuu Netanyah anasema Israel ndio mlinzi wa UKRITO na iungwe mkono.
Hii ni kauli ya hofu ikionyesha wazi Israel ina hofu hadi kuahidi kwamba ikishambuliwa itatumia Nuclear.

Hii si vita ya dini kwasababu Israel ilikuwa na kambi Saud Arabia, UAE, Jordan n.k. hoja ya dini inatoka wapi?

Ni mchezo huo huo unaotumiwa na Saud Arabia wakisingizia Houthi wamepiga eneo takatifu la MECCA.

Houthi hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanaamini katika Kaaba na miji mitakatifu. Saudi inacheza karata ili Waislam waungane dhidi ya Houthi. Hata hivyo Saud imefeli kwasababu dunia ya sasa ukweli upo kiganjani.

Kwanini Marekani imeitosa Saud Arabia?

Itaendelea
 
Back
Top Bottom