Trump ana wakati mgumu sababu ameingizwa mkenge na Netanyahu kwa kuaminishwa kwamba operesheni ya kuchochea maandamano ndani ya Iran pamoja na kumuua Ayatollah Khameini pekee ingechangia kuuangusha utawala wa Iran kwa haraka sana kitu ambacho imekuwa kinyume.
Netanyahu alichangia kuanguka kwa utawala wa Syria chini ya Bashar. Baada ya kuwapiga Hamas na kumuua Nasrallah wa Hezbollah, Israel wakajua Iran haina nguvu na kumshawishi Trump aingie vitani
Vyombo vya usalama vya Marekani vilimuonya Trump kwamba mambo si rahisi kama anavyosema Netantahu
Tukianza na Lebanon, hali ni mbaya kwa Israel wanaumizwa na Hezbollah. Technology ya Hezbollah inaharibu vifaru na magari ya deraya achilia mbali kuua askari.
Israel imelazimika kurudi nyuma na kuachia hata miji yake. Haisemwi wazi lakini ukweli Israel ina wakati mgumu
Kumuua Nasrallah hakujasaidia kitu kwasababu Walebanon wanaamini katika Utaifa kama walivyo Wapalestina
Kimya cha Hezbollah kilimpa kichwa Netanyahu kwamba wakijua viongozi taasisi zinadhoofika.
Kosa walilofanya Iran ni kumuua Khamenei aliyekuwa a moderate katika maamuzi ikiwemo kutotaka Nuke kama silaha. Kifo cha Khamenei kimewaunganisha Wairan kwasababu wanaona kama shambulio la Dini
Marekani imepoteza kambi 16. Image za Radar system zinaonyesha kufutwa Radar kubwa 4 kati ya 8 zilizopo Duniani. Ndege zote na drone za Marekani zinazoaminika zimetumika katika vita na kuvunja miundo mbinu
Jaribio la kutaka kupora Uraniun kule Isfahan limeshindwa, Navy imeshindwa kufanya lolote Hormuz , Marekani haina la kufanya Hormuz licha ya usadizi wa Mataifa makubwa .
Mataifa sasa yanaongea na Iran kuhusu meli zao na kuifanya kuwa mbabe wa Mashariki ya Kati
Marekani inataka mazungumzo na si vita. Israel inataka vita kwasababu anayetangulia ni Marekani kwa gharama na vifo. Kwenye mazungumzo Israel hayupo mezani anasubiri kuamriwa nini cha kufanya na Marekani
Trump anapata pressure ndani ya nchi, kavuruga JCPOA ya Obama sasa anatafuta ''JCPOA'' ile ile kwa gharama za damu na kodi za Wamarekani. Hapa ndipo alipokwama kwasababu hataki vita na hajapata mkataba.
Vita imeonyesha udhaifu mkubwa wa Marekani. Meli na Manowari iliyojivunia hazina maana kwa Technology ya sasa. Vitisho na makomboram Iran imesimamam ushahidi kwamba Marekani ina wakati mgumu kusimama na China, Russia ikiwa itatokea .