Ndege ya Wing of Zion iliondoka Nevatim, na kuzua uvumi wa mapigano mapya.
Ripoti za Iran zinadai Tehran imepokea taarifa za kijasusi kuhusu shambulio la kushtukiza la Marekani na Israel baada ya Siku ya Uhuru.
Rais wa Iran asema nchi hiyo haitaachana na haki zake za nyuklia licha ya shinikizo kutoka kwa Trump.
Hapo awali Viongozi wa Iran walikubaliana na Marekani kusitisha vita kwa matakwa kadhaa ya pande zote mbili kushughulikiwa
Upande wa Iran
Walitaka Marekani Aondoe meli pale Hormuz Kwakuwa Marekani aliweka vizuizi kwa meli zote za kwenda na kutoka Iran na kuzuia bandari zote za Iran ambapo lilikuwa shinikizo la kuifanya Iran iache mlango wa Hormuz free kwa ajili ya meli zingine kupita ukanda ule,
Baada ya Iran kuona watakosa mapato Kwakuwa ndo chanzo kikuu cha mapato wakakubali kuachia, Baada ya kuachia Lakin Marekani meli zake zikaendelea kusalia pale Mpaka Iran atekeleze makubaliano mengine Ambapo Iran wakaona ni kama mtego wakazuia njia upya !!
Pia Iran walikuwa wamekubali kutorutubisha Tena urani kwa miaka mitano na kukabidhi mabaki kwa Marekani , jambo ambalo baadae viongozi wa juu wa Iran wakaona kama wakionekana wamekubali hilo ni kama kusalitiana juu ya misimamo Hiyo! Nalo wamelifikiria upya na kuona bora wasikubali
Iran ilikuwa imeshinikiza kulipwa gharama za vita na pia kusema Marekani ashinikize Israel iache kushambulia Lebanon ambapo, Israell ni kama walisita maana hilo lilionekana ni makubaliano ya Iran na Marekani wala si Israel,
Pia Marekani ilikuwa Imeshunikiza kuwa Irani iache kuvifadhili Vikundi vya magaidi kama Hamas na Hezbollah
Britanicca