Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Watu 7500? Hivi 1979 kulikua na watu wangapi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Mayunga hakuwa na mambo yanayotia shaka wakati wa vita? Yaani yasiyokuwa ya kawaida?
teh!! teh!! teh !!teh !! Hiyo siyo kweli kabisa; sikuwa frontline lakini stori hizo ni za kupikwa tu. Mayunga alikuwa askari mkomavu, shujaa, mwenye kujiamini sana na alikuwa anajua sana kuongoza vita. Watu wakaanza kumtungia stori za ajabu ajabu ambazo hazina ukweli wowote. Mara baada ya vita kuna watu waliwahi kusema kuwa Mayunga alipigana vita ya Biafra akaja na uchawi wa Nigeria, mambo ambayo siyo kweli kabisa. teh!! teh!! teh !!teh !! teh!! teh!! teh !!teh !!

Usinivunje mbavu kwa kicheko.
 
Idd

Idd Amini alikua mshenzi tena alijiamini kupitiliza tofauti na uwezo wake
 
Idd


Idd Amini alikua mshenzi tena alijiamini kupitiliza tofauti na uwezo wake
Ukibishana na gavana utapata tabu sana kwani jiandae kusikia uwongo, uzushi na na hata ukweli mradi tu uwe ni wa kupambanisha ukristo na Uislamu na uwe unamponda Nyerere. Sasa kam wewe unataka ukweli, basi unaweza kupata maumivu ya kichwa
 
Vita siyo maandamano,kila mbinu inayoweza kukusaidia unaitumia
 
Vita siyo maandamano,kila mbinu inayoweza kukusaidia unaitumia
Ni kweli. jeshi la Tanzania lilikuwa linajua vita sana. Nimetoka kwenye system muda mrefu sana kwa hiyo sijui sasa jeshi letu likoje, lakini jamaa wale walikuwa wanajua kupigana. Kuna watu hawajui kuwa tulisaidid Zimbabwe kumwondoa Smith na vile vile Musumbiji kumwondoa Mreno. ndiyo maana tuna medal za Operation Safisha Msumbiji, na nishani ya Zimbabwe. Kwa hiyo wao kuingia pale vitani ilikuwa ni kama kutoka chumba kimoja cha ofisi na kuingia chumba kingine kwenye jengo hilo hilo
 
Watoto wa 2000 wanapojaribu kuzaliwa 1960

Mdogo wangu vita haikuwa ya ulazima wakati Nduli Iddi Amini Dada alivamia Mkoa wa Kagera kwa madai ya kwamba ile ni sehemu ya uganda lazima aichukue.

Kwa hiyo mwl. JKN angewaachia..!?
Ndivyo wanavyofundishwa kwenye vijiwe vya kahawa eti Idd Amin alikuwa mtu mwema sana, na hakuwa na kosa lote...alionewa tu. Wamekubali kuwa wajinga
 
Watoto wadogo wanaboa,vita ni ushindi kuhusu vifo lazima mfe..vietnam walipoteza askari wengi sana ila walifanikiwa kumpiga marekani.walishinda
 
Alitaifisha shule na hospitali zote za wakristu kusudi watu wa dini zote wasome na wapate matibabu bure. Dini za kikristo zilikuwa na mahosptiali na mashule mengi sana kuliko serikali.
Hata mimi nashangazwa kumconnect Nyerere na udini haswa mission ya kuua uislam.Nachojua Idd amini alikuwa brain washed na mifumo ya dini ya kiislam na ndiyo maana alikuwa karibu sana na Libya na inasadikika Iddi Amini alikuwa swala tano na ndiyo sababu ya yeye kusaidiwa na Libya kwenda kujificha Uarabuni huko alipofia.
 
Kweli nimeonana naye ila kuna sehemu anachapia sana!!!!
Asante sana kwa kutupigania frontline. Kaka yangu naye alikuwa active duty nadhani sijui 319KJ au kitu kama hicho sikumbuki tena; yeye alikwenda mpaka Arua. Alirudi nyumbani na Radio Cassete kubwa sana ya double deck. Mimi nilikuwa makao makuu ya brigade tu nikiwa napokea taarifa na kuzipeleka kwa makamanda kwa hiyo baada ya vita sikuwa na radio cassete kubwa kama ile; nilibaki na 277 dudu proof yangu. Ni kwa vile muda umekwenda sana na nimeshapitia sehemu tofauti za maisha ila sisi watu COMM tulikuwa tunapata taarifa nyingi sana kuhusu mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye theater.
 
Mkuu asante sana kwa maandiko yako humu, nakushauri jitahidi auandike hata kwa mtazamo wako tu juu ya vita ya Kagera. Hii itasaidia kutuepusha na wapotoshaji na "wafia dini" walioradhi kuandika upupu wowote kumtetea mtu wa dini kama yao
 
Wengi hawajui,niliishi kikosi cha mafinga miaka 4 nilijifunza mengi ambayo sikuwa nayajua
 

Kifungu kipi hicho , hivi lini Rais alitoka Kwa akina Gwajima ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…