Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Mkuu hizii ni battalion 4, bro wangu alikuwepo uwa nashangaa Nyerere kipindi anawapokea wanajeshi waliorudi alisema "tumepoteza vijana wetu 379" na Mkapa kwenye mbook wake karudia kosa hili kwa makusudi. Tulipoteza askari zaidi ya 5000, na raia zaidi ya 2500 miezi mitatu ya kwanza ya vita baada ya kutekwa kwa eneo la Kakunyu, Kabwobya na Minziro wanajeshi wetu walivofka Mutukula walilipa kisasi cha staili ile ya kyaka (ya raia na wanajeshi waliokufa) yaan "Masacre" au "mfekane" kwa hiyo Mutukula kuna raia zaidi ya 3000 waliuliwa (na Watanzania wakiwemo) yaan dah hii vitaa kuna mengi tunafichwa huyu jamaa ameamua kuwa muwazii lakini nae hajasema ukwelii

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu 7500? Hivi 1979 kulikua na watu wangapi Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Mayunga hakuwa na mambo yanayotia shaka wakati wa vita? Yaani yasiyokuwa ya kawaida?
teh!! teh!! teh !!teh !! Hiyo siyo kweli kabisa; sikuwa frontline lakini stori hizo ni za kupikwa tu. Mayunga alikuwa askari mkomavu, shujaa, mwenye kujiamini sana na alikuwa anajua sana kuongoza vita. Watu wakaanza kumtungia stori za ajabu ajabu ambazo hazina ukweli wowote. Mara baada ya vita kuna watu waliwahi kusema kuwa Mayunga alipigana vita ya Biafra akaja na uchawi wa Nigeria, mambo ambayo siyo kweli kabisa. teh!! teh!! teh !!teh !! teh!! teh!! teh !!teh !!

Usinivunje mbavu kwa kicheko.
 
Idd
Sijachanganyikiwa kwani Idd Amin hakuzuka tu akavamia. Kosa ni la Nyerere kumkumbatia rafiki yake Obote . Mambo ya Uganda angaliwaachilia Waganda na ghasia zao . Mbona hakuivamia Kenya wala Sudan wala Kongo ??

Niliandika kabla hawa wapinzani wa Uganda walikuwa wakiingia Uganda kutokea Tanzania na kufanya vitendo vya Ugaidi .


Idd Amini alikua mshenzi tena alijiamini kupitiliza tofauti na uwezo wake
 
Idd


Idd Amini alikua mshenzi tena alijiamini kupitiliza tofauti na uwezo wake
Ukibishana na gavana utapata tabu sana kwani jiandae kusikia uwongo, uzushi na na hata ukweli mradi tu uwe ni wa kupambanisha ukristo na Uislamu na uwe unamponda Nyerere. Sasa kam wewe unataka ukweli, basi unaweza kupata maumivu ya kichwa
 
Vita siyo maandamano,kila mbinu inayoweza kukusaidia unaitumia
Ni kweli. jeshi la Tanzania lilikuwa linajua vita sana. Nimetoka kwenye system muda mrefu sana kwa hiyo sijui sasa jeshi letu likoje, lakini jamaa wale walikuwa wanajua kupigana. Kuna watu hawajui kuwa tulisaidid Zimbabwe kumwondoa Smith na vile vile Musumbiji kumwondoa Mreno. ndiyo maana tuna medal za Operation Safisha Msumbiji, na nishani ya Zimbabwe. Kwa hiyo wao kuingia pale vitani ilikuwa ni kama kutoka chumba kimoja cha ofisi na kuingia chumba kingine kwenye jengo hilo hilo
 
Watoto wa 2000 wanapojaribu kuzaliwa 1960

Mdogo wangu vita haikuwa ya ulazima wakati Nduli Iddi Amini Dada alivamia Mkoa wa Kagera kwa madai ya kwamba ile ni sehemu ya uganda lazima aichukue.

Kwa hiyo mwl. JKN angewaachia..!?
Ndivyo wanavyofundishwa kwenye vijiwe vya kahawa eti Idd Amin alikuwa mtu mwema sana, na hakuwa na kosa lote...alionewa tu. Wamekubali kuwa wajinga
 
Mkuu Kichuguu shukrani kwa kumbukumbu nzuri post #12 na #14,watoto wadogo wanajazwa ujinga na story za kuunga unga kutoka kwa watu ambao hata hawajui bunduki inashikwaje.

Mimi ni kizazi baada ya hii vita early 80s but siwezi kukaa kubishana eti “walikufa watu wengi sana” nani asiyejuwa vita ni kifo?huyo mzazi mwenyewe anamruhusu mwanae kwenda jeshini kichwani akijua muda wowote ataletewa badge yake kwamba mwanao kumbukumbu yake hii hapa kuwaje tukatae watu kufa,je hao Uganda ndo walipoteza watu wachache sana?vita tulishinda hatukushinda hiyo ndo habari ila kwamba watu walikufa wangapi siyo habari waliifia nchi na wanaenziwa.
Watoto wadogo wanaboa,vita ni ushindi kuhusu vifo lazima mfe..vietnam walipoteza askari wengi sana ila walifanikiwa kumpiga marekani.walishinda
 
Alitaifisha shule na hospitali zote za wakristu kusudi watu wa dini zote wasome na wapate matibabu bure. Dini za kikristo zilikuwa na mahosptiali na mashule mengi sana kuliko serikali.
Hata mimi nashangazwa kumconnect Nyerere na udini haswa mission ya kuua uislam.Nachojua Idd amini alikuwa brain washed na mifumo ya dini ya kiislam na ndiyo maana alikuwa karibu sana na Libya na inasadikika Iddi Amini alikuwa swala tano na ndiyo sababu ya yeye kusaidiwa na Libya kwenda kujificha Uarabuni huko alipofia.
 
Kweli nimeonana naye ila kuna sehemu anachapia sana!!!!
Asante sana kwa kutupigania frontline. Kaka yangu naye alikuwa active duty nadhani sijui 319KJ au kitu kama hicho sikumbuki tena; yeye alikwenda mpaka Arua. Alirudi nyumbani na Radio Cassete kubwa sana ya double deck. Mimi nilikuwa makao makuu ya brigade tu nikiwa napokea taarifa na kuzipeleka kwa makamanda kwa hiyo baada ya vita sikuwa na radio cassete kubwa kama ile; nilibaki na 277 dudu proof yangu. Ni kwa vile muda umekwenda sana na nimeshapitia sehemu tofauti za maisha ila sisi watu COMM tulikuwa tunapata taarifa nyingi sana kuhusu mambo yaliyokuwa yakiendelea kwenye theater.
 
Hapa kuna maswali mengi nitajitahidi kujibu moja moja kama ifuatavy:

(1) Wakati wa mapambano kulijitokeza vikundi vingi vya kumpinga Amini hivyo Mwalimu akwashauri waungane ndipo wakawa na ule Mkutano wa Moshi. PK hakuwa mwanajeshi wakati huo na alikuwa raia wa kawaida mkimbizi huko Uganda. Tanzania ilipita Rwanda wakati wa Hyabarimana, na siyo kuwa walitusaidia bali tulipita mpakani na wala hawakujua kuwa jeshi letu lilikuwa limepita huko. M7 naye alikuwa na kikundi chake ambavyo vyote viliunganishwa kuwa kundi moja kubwa likiongozwa na Yusuf Lule. Wakati huo M7 naye alikuwa anaishi tanzania kama mkimbizi.
(2) Mkutano wa Moshi haukuwa wa kuhalalisha waasi wa Obote, kama nilivyosema hapo uliunganisha vikundi vyote vilivyojitokeza kumpinga Amini. Wakati huo Nyerere alishaona kuwa Amin ataanguka na hakutaka aache ombwe la uongozi wala Tanzania iitawale Uganda, hivyo alikuwa anawaandaa waganda wajitawale wenyewe baada ya Amini kuangushwa.
(3)Ni kweli Nyerere alikuwa anamshabiia Obote kutokana na historia ya kuelewana kwa muda mrefu, kwa bahati mbaya nadhani hakujua kuwa waganda walikuwa hawamtaki kabisa. Kwa hiyo wakati Obote anshinda uchaguzi wa kwanza baada ya vita waganda walipinga vikali matokeo yale, na ndiyo iliyoletelza M7 aanazishe jeshi lake la msitunii. Ndippo aliaandikisha wanyarwand wengi wakimbiiz akina Fred Rwigyemn an Paulo Kagame.
(4) makubalino ya Mogadishu yaliratibiwa na Siad Barre na Tanzania ilimhusisha Samwel Malecela wakati akiwa wazir wa mambo ya nje. Makubalinao yalifanyika baada ya kikundi cha Obote kuwa kimejaribu kuingia Uganda muda mfupi baada ya mapinduzi kikitokea Tanzania na kikapigwa vibaya na askari wa Amin; kwa hiyo makubaliano yakawa yanazuia kushambuliana. Makubaliano yale yalikosa thamani baada ya Amini kuvamia Tanzania na kuchukua lile eneo la kagera; alikuwa anadai kuwa mpaka halali ulikuwa ni mto Kagera. Alifanya hivyo bila kuchokozwa.
(5) Afrika ya Mashariki ilianguka kutokana na shinikizo la Charles Njojo kwa Kenyata; hakukuwa na uhusiano kabisa na vita ile wala mfarakano wa Nyerere na Amini. Nyerere aliwahi kukutana na Amin mara nyingi sana, siku moja walikutania Mwanza. Mpaka leo ukimsikia Njonjo ana miaka zaidi ya 100 bado hataki shirikisho. Siku moja nilimsikia akihojiwa na Jeff Koinange na bado akasisistiza kuitaka Kenya ijitoe kwenye Jumuia.
View attachment 1479970
Mkuu asante sana kwa maandiko yako humu, nakushauri jitahidi auandike hata kwa mtazamo wako tu juu ya vita ya Kagera. Hii itasaidia kutuepusha na wapotoshaji na "wafia dini" walioradhi kuandika upupu wowote kumtetea mtu wa dini kama yao
 
Ni kweli. jeshi la Tanzania lilikuwa linajua vita sana. Nimetoka kwenye system muda mrefu sana kwa hiyo sijui sasa jeshi letu likoje, lakini jamaa wale walikuwa wanajua kupigana. Kuna watu hawajui kuwa tulisaidid Zimbabwe kumwondoa Smith na vile vile Musumbiji kumwondoa Mreno. ndiyo maana tuna medal za Operation Safisha Msumbiji, na nishani ya Zimbabwe. Kwa hiyo wao kuingia pale vitani ilikuwa ni kama kutoka chumba kimoja cha ofisi na kuingia chumba kingine kwenye jengo hilo hilo
Wengi hawajui,niliishi kikosi cha mafinga miaka 4 nilijifunza mengi ambayo sikuwa nayajua
 
Nyerere huyu mnaemuita mdini amae alikuwa anaratibu mfumo Ukristo(ukatoriki) ndo huyo huyo aliweka kamfumo kasiko rasmi kwenye katiba kwenye kupokezana urais kati ya hizi dini mbili kuu hapa nchini.
WAISLAM WAKATI MWINGINE MJITAHIDI KUFICHA UJINGA WENU ILI JAMII IWAHESHIMU

Kifungu kipi hicho , hivi lini Rais alitoka Kwa akina Gwajima ??
 
Back
Top Bottom