Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Naona kama wewe unaquestion uwezo wa jeshi la Tanzania wakati huo, na unaelekea kuamini tu kuwa JWTZ walikuwa ni wanyonge. Leo hii sijui muundo wa JWTZ, lakini wakati wa Nyerere JWTZ ilikuwa ni pamoja na JTK, Polisi, Magereza, na Mgambo kama majeshi ya akiba. Kulikuwa na sera ya kuwa jukumu ulinzi wa taifa letu ni raia wote na kila askari katika eneo lolote alikuwa ni mlinzi wa taifa. Hicho kitabu ulichosoma inawezekana kilikuwa kinaripoti namba za wale active soldiers wa TPDF na kusahau kuwa TPDF ilikuwa na reserve soldiesr wengi sana; baada ya vita kuanza wale reserve soldiers wote walikuwa activated na jeshi kuonekana kubwa sana. Katika yote ya Nyerere nadhani sifa yake kubwa ni ile ya kujenga mioyo ya uzalendo kwa wananchi.
 
Mkuu Kichuguu vijana wa siku hizi hawataki kujifunza historia ya nchi yao
 
Mkuu hapa sasa nimekuelewa baada ya Uganda kuingia madarakani aliua mapadri wengi na akiwemo huyu Kiwanukaa

Sent using Jamii Forums mobile app


Idd Amin hakuwa mdini , ila Kanisa Katoliki lilikuwa likijiingiza kwenye siasa kama linavyofanya kwenye nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania. Labda kwa kuona malengo yao hayatotimia kwa urahisi
 
Ila wahaya ni wakuwaonea huruma sana, Ukimwi ulipoingia uliwafyeka sana wao na Vita ya Kagera iliwamaliza sana.... haiyumkini leo hii hili ndio lingekuwa kabila kubwa na lenye nguvu nchini hasa kwa idadi ya watu.... pia Mji wa Bukoba ungekuwa Jiji pengine.... Mungu awape nguvu wahaya na makabila yote wazawa wa Bukoba
 
Mmmmmhhhhh, ukatoliki unakujaje tena kwenye hiyo vita?


Ukumbuke Kabla Idd Amin hata hakuwa na fikra za kuivamia TZ isipokuwa kwa vile wapinzani wa Amin walikuwa wakifanya vitendo vya kigaidi ndani ya Uganda kutokea Tanzania . Mwisho Amin akaona ni bora avamie aichukuwe Kagera iwe ni kama buffer zone yake kuzuia vitendo hivi vya kigaidi.
 
Yapo mengi yanapotoshwa kuhusiana na hii vita. Angalau wewe unatupa mwanga halisi na taswira kamili juu ya kilichotokea. Endelea kutushushia madini kama hutojari mzee wetu achana na huyu poyoyo anayekupinga bila kuweka hadidu za rejea
 
Ukitaka kujua unajadili na nani itisha ile hidden profile yake. Au muulize umri wake utapoteza muda na wanafunzi wanaosubiri tangazo la Covid 19 kuisha.
 
Ndugu mimi ni layman kwenye maswala ya kijeshi, lakini kwa mtazamo wa kawaida unajua hatuna kiwanda cha silaha na zote zinatoka nje, unadhani zilikua zinanunuliwa nini, unadhani tons ngapi za risasi zilikua zinatumika kwa siku, mabomu mangapi kwa siku, dawa kiasi gani kwa siku kutibu majeruhi, mafuta kiasi gani kubeba maaskari na vifaa, kwa kufirikia just even as a layman unaweza kuona kiasi gani cha fedha kilikua kinaenda kwa siku na nchi ilikua na just 18years umepata Uhuru.

Lazima uchumi utetereke, kama Marekani inatetereka, how about Tanzania? Vita si biashara the loss is always greater hata ukishinda. Ndio maana Sun Tzu akasema the greatest military strategist is the one who can win the war (diplomatically) before the fi bullet is fired. Kuhusu kupelekwa mgambo, nadhani hii ni obvious huwezi kuchukua all your professional and experienced soldiers ukawapeleka frontline. Anything can happen kule, kuna commanding errors na mambo mengine yanaweza kutokea. So lazima wawepo wa ku-train new recruits na pia wa kwenda nao front ili wazoee Vita. Si mpaka uwe mwanajeshi au ufanye kazi wizara hiyo kujua haya. Just a common sense
 
Waliosoma na kuhadithiwa vita ya Kagera wanaonekana wanajua sana kuliko waliopigana vita yenyewe soon natia neno
Ni kweli kwa sababu sisi tulio_iishi hiyo vita tupo kimya.

nakumbuka miaka hiyo wakati vita imepamba moto.

Mimi nilitokaga BELENGE sita sahau.

kipindi hicho VIAZI vilikuwa bado havijaanza kuitwa CHIPS
 
Watu 2000 walikuwa % ngapi ya watanzania? Je leo hawa 2000 wangekuwa wamezalisha watu wangapi? Population yetu leo ingekuwa inasoma watu 65 milion
 
Hapo nimekuelewa.
 
Tactician mkubwa wa JWTZ alikuwa ni Kanali Kitete (Siyo Lupogo) kabla hajawa Brigadier. Jamaa yule anajua kupanga vita siyo mchezo, sijui kama bado JWTZ leo hii ina tacticians kama yeye. Jamaa alichambua kuwa Amini alikuwa ameweka ulinzi mkubwa sana directly kwenye mpaka wa Tanzania (backed by heavily Mechanized Simba Batallion), ila hakuwa na ulinzi kule Magharibi kwa nsababu alikuwa na uhusiano mzuri sana na Mobutu wakati huo (mpaka leo Kampala kuna mtaa una jina la Mobutu liliowekwa na Amini). Kamanda akachambua ramani na kuweka mkakati uliomfuta Amin kwenye ramani kwa kutokea Magharibi ya Uganda.


Kwenye video hii hapa chini huwa napenda sana kile kipande kuanzia 1:04 hadi 1:34 kinachoonyesha makamanda wetu shujaa.

 
Uongo huo;

Kwanza elewa kuwa Professor Lule aliwekwa pale na Nyerere akiamini kuwa atawaunganisha waganda. Failure kubwa ya Professor Lure (hakuwa na PhD) ni pale aliposhindwa kujiweka katika maisha ya waganda na kushindwa kutuliza matakwa ya upkeeping cost ya cabinet yake. Hapo ndipo alipotofautiana na Nyerere mpaka mwisho
 
Si maoni yangu tu hata wewe unayo haki ya kunisahihisha kama si kweli
Kuna sababu za wazi na nyingine ni za siri. Mimi sina ushahidi wa hili ya Nyerere kuingiza nchi kwenye vita kisa ukatoliki wake. Ndio maana nimeita "maoni" maana sijui kama una ushahidi wowote wa hayo unayoyasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…