Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Mbona Marekani, Uingereza, Ufaransa,na Ujerumani huwaweki kwenye list ya waliokuwa wapeleka silaha wakubwa kwa waasi?
Wao pia walihusika pakubwa kupeleka silaha na kutoa mafunzo kwa waasi ila baada ya Isis kuibuka waliachana na huo mpango na kuamua kuwashawishi Wakurdi kuungana nao kupigana na Isis.....jambo lililoikera sana Uturuki.
 
Naona Mji waHama umekuwa mfupa mgumu kwa Waasi wamerudishwa nyuma kwa mara ya pili.

Naona Hama sio kama Aleppo Majeshi ya Serikali yamejizatiti.
 
Naona Mji waHama umekuwa mfupa mgumu kwa Waasi wamerudishwa nyuma kwa mara ya pili.

Naona Hama sio kama Aleppo Majeshi ya Serikali yamejizatiti.
Nipe Link basi kama ni you tube niingie nichek
 
Hapo anatafutwa Iran jombaa. Mizizi yote ya Iran inatakiwa kukatwa hapo Middle East.
Hizi hadithi tushazichoka huyo iran anaetafutwa kamdunda Israel mchana kweupe jua linawaka dunia imeona kama ni hiyo vita si ingeanzishwa pale,, zaidi ya kumjibu kwa shambulizi uchwara lililopambwa na propaganda nyingi kuficha aibu.
 
View: https://x.com/Osint613/status/1863602609455546419?t=wxCrPgA_WgTLkcV-OyMd0Q&s=19

FaizaFoxy Assad na yeye ni mzayuni au hana namna 😂😂😂

Unajua Israel ikisema itupe zile Silaha ilizokamata kwa Hezbollah na Iwe inafanya Mashambulizi 10 Syria kila siku kuwasaidia Makobazi ndani ya miezi 3 Assad atabaki na Kijiji tu

Hii Israel iliyo peleka wanajeshi zaidi ya elfu hamsini wenye kila aina ya siraha kupambana na wanamgambo wa Hizbullah wakaambulia kuteka eneo la km za mraba 7 ambazo ukubwa wake haufiki hata kitongoji?
 
Wao pia walihusika pakubwa kupeleka silaha na kutoa mafunzo kwa waasi ila baada ya Isis kuibuka waliachana na huo mpango na kuamua kuwashawishi Wakurdi kuungana nao kupigana na Isis.....jambo lililoikera sana Uturuki.
Chanzo cha silaha za ISS ni siraha za Marekani na Wingereza zilizo zagaa wakati wa uvamizi wa Iraq na sio Syria.
Kiufupi Marekani ndo muasisi wa uovu na mauaji yanayo endelea hapo Mashariki ya kati.

Kabla ya Marekani haja fanya uvamizi dhidi ya Afghanistan,na Iraq mashariki ya kati ilikuwa imetulia.

Hata mgogoro wa Israel na Palestina Marekani ndo kikwazo kikubwa maana asinge kuwa anaikingia kifua Israel ingekuwa imesha kubali kuchagua amani badala ya ubabe.
 
Hayo Makundi yakishika madaraka yataishambulije Israel wakati na yeye ni mmoja wapo wa waungaji mkono wa makundi hayo?
Hayo Makundi yapo Syria zaidi ya miaka 13 sasa ulisha wahi kuona yanashambulia Israel hata kwa risasi moja?

Alafu aliye kwambia kuwa kipimo cha kuwa mkorofi ni kugombana na Israel ni nani ? Ya kuwa leo hii akingia kiongozi nchini Syria akataka kuirudisha Golan atakuwa ni mkorofi?
Hao Israel mnao taka wafanyiwe usitaarabu wao ni wastaarabu?
Mara zote mnaanza nyiny kushambulia Israel , Acha ajilinde
 
Chanzo cha silaha za ISS ni siraha za Marekani na Wingereza zilizo zagaa wakati wa uvamizi wa Iraq na sio Syria.
Kiufupi Marekani ndo muasisi wa uovu na mauaji yanayo endelea hapo Mashariki ya kati.

Kabla ya Marekani haja fanya uvamizi dhidi ya Afghanistan,na Iraq mashariki ya kati ilikuwa imetulia.

Hata mgogoro wa Israel na Palestina Marekani ndo kikwazo kikubwa maana asinge kuwa anaikingia kifua Israel ingekuwa imesha kubali kuchagua amani badala ya ubabe.
We jamaa ni mnafiki sn , eti Mashariki ya kati ilikuwa imetulia , Kwa vile walikuwa hawakuonesh Sadam anavyoua wapinzan wake ?
 
Huku wanakofanya Askari wa Serikali ya Syria sio Surrender bali mass defections haiwezekani Askari 1000 wakubali kuweka Silaha chini bila kupiga risasi hata moja.

Hawa Askari wengi wao ni Sunni watajiunga na Waasi. Duuh!
Assad muda wote alikuwa busy kulifanya jeshi lake kuwa coup-proof tu mambo mengine ziada. Kati ya Marais nawakubali kwa kujilinda dhidi ya mapinduzi duniani ni Bashar al-Assad.

Mkuu wa 4th Armored Division, kikosi maalum cha jeshi la Syria kinachokuwa kusini mwa Damascus kinaongozwa na Major General Maher al-Assad mdogo wake Rais.
Assad ana mashirika ya ujasusi kama matatu hivi yanayojitegemea na yanachunguzana, kama sikosei jeshi wana la kwao, Airforce ina la kwake (nahisi sababu baba yake Hafez alipindua kutokea Airforce aliasisi hili), polisi wana la kwao, wizara gani sijui mambo ya ndani wana la taifa kiujumla.

Assad anaongoza nchi ambayo dhehebu lake na jamii yake ni minority hivyo wanajeshi wengi sio dini yake wala jamii yake. Anachokifanya anakusanya wanajeshi kutoka maeneo yanayomuunga mkono ila maofisa wa juu wa majeshi yake ni kutoka minorities. Si rahisi Msuni kutoka Allepo awe ofisa mkubwa kwenye jeshi la Assad. Kwa hiyo jeshi maofisa wake sio competent bali asili, eneo, uchawa na dhehebu ndio vinawabeba.

Hata kwa wanajeshi wenyewe, baada ya vita kutokea kulikuwa na forces recruitment. Serikali ya Assad ina rushwa kubwa na ufisadi kupindukia, na jeshini hachukui hatua kuzuia ilimradi maofisa ni machawa wake anawaachia nafasi "wale" ili walinde serikali yake huku wanalinda matumbo yao. Kwahiyo recruitment inakwepwa endapo kijana familia yake ina hela kutoa rushwa asiende jeshini. Recruitments waliopo jeshini hawako motivated, huwezi wapiganisha na waasi au magaidi ambao wengi wamejiunga kwa kutaka wenyewe.

Training ya Syrian Arab Army ni dhaifu. Wana miaka zaidi ya 10 vitani ila hawana defensive lines, hawajui repelling of fast attack, hawajajipanga dhidi ya drones, hawajui kufanya retreat wakiondoka sehemu wanakurupuka wanaacha silaha ziko intact zinachukuliwa na adui badala kuziharibu au kuzihamisha.

Na kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na hali ngumu nchini Syria, Assad alitumia vyombo vya usalama kuzalisha kipato kwa madawa ya kulevya. Wanasafirisha shehena ya madawa pale Middle East angalau wapate kipato cha kudunduliza juu ya hali yao ngumu.

Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.
 
Back
Top Bottom