Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Sunni hakuna mgawanyiko! Sunni inaundwa na ncha 4.
Hizi ncha zinaitwa madheheb, ndipo kuna Hanafi, Hanbali, Maliki na Shafii.
Hakuna mahali popote ukasikia hayo madheheb yamegombana, hakuna!
Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kwa ukubwa ni madheheb ya Shafii. Madheheb yaliyobakia ni yana wafuasi wachache kama shia, ibadhi n.k na hatujawahi kusikia hata siku moja wakigombana.
Sufi siyo dheheb, sufi ni mojawapo katika matawi ya elimu mtu anaamua kushughulika nayo! Wanasema sheria ni timilifu la kiwiliwili, Sufi ni timilifu la kiroho. Kwenye usufi wapo madheheb ya Shafii, Hanbali, Hanafi na Maliki. Wote utawakuta humo. Hilo ni tawi la elimu la tazkiya (elimu ya kuitakasa nafsi).
Kwenye usufi kuna madheheb napo!
Kuna Shisti, Naqshibandi, Sahrawardii, Qadir, Shadhalii n.k
Mtu anaweza akawa sunni na asiwe kwenye usufi n.k
Wahabi ndiyo Salafi na ndiyo Answar Sunna. Hayo majina yote yanawakilisha dhehebu moja Siyo dhehebu tofauti.
Hili dheheb lipo tofauti na madheheb yote ya juu niliyoyaorodhesha. Hili dheheb linapingana na madheheb yote ya hapo juu kwa namna yake. Na madheheb ya hapo juu yanapingana na Salafi au wahab kwa namna yao pia.
Kupingana kwao ni kielimu si kimapigano ya kimwili.
Na salafi au wahab wamegawanyika! Wapo ambao wenye msimamo mkali sana na wapo ambao wapo safi hawana matatizo yoyote kwenye jamii.
Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki wengi wao ni Sunni madheheb ya Shafii, ambapo humo kwenye Usunni wapo ambao wanaofuata sufi.
Madheheb mengine ni Shia, Ibadh Wahab/Salaf n.k