Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Yani Kuna muda hadi unasikitika mkuu.

Kama ukisema ni uislam mbona Malaysia,Indonesia,Brunei waislam wengi na hayo hayatokei!?

Bangladesh Kuna waislam wengi na dini zingine kibao ila wanaungana chini ya bendera moja ya nchi.

Hata Sheikh Hasinah alipopinduliwa na wananchi waislam,wakristo kwa wapagani waliungana chini ya kauli moja.

Sijui waarabu wana nini kichwani kiasi hawana umoja!?
Cha kushangaza zaidi nchi zetu zina amani ila hatuzipi maendeleo hizo nchi za kiarabu zenye vita kila siku
 
Ndio swali langu lilipo hapo mkuu.
Hao Mabikra 70 na ushee sijui wataanza kutoa penzi kwa Sunni au kwa Shia au watawagawana?! Kwakweli maswali ni mengi sana kuliko hata majibu.

Kwasababu Magaidi yanavyouwana huko Syria na mengine yanazidi kuongezeka kutokea Lebanon Iraq na Iran mpaka sasa vifo ni 1000+
 
Waliokimbia maeneo yao miaka 13 iliyopita waanza kurejea
1000041928.jpg
 
Waasi wameshindwa kuuteka Mji wa Hama wamekumbana na upinzani mkali kutoka kwa Majeshi la Syria Arab Republic +Russia+Hezbola+ Shia Millitias.

Je hii offensive ya Waasi ndio imefikia mwisho?! Je wataanza kurudishwa nyuma?! Yetu macho na Popcorns 🍿 na Bia bariidi.
 
Assad muda wote alikuwa busy kulifanya jeshi lake kuwa coup-proof tu mambo mengine ziada. Kati ya Marais nawakubali kwa kujilinda dhidi ya mapinduzi duniani ni Bashar al-Assad.

Mkuu wa 4th Armored Division, kikosi maalum cha jeshi la Syria kinachokuwa kusini mwa Damascus kinaongozwa na Major General Maher al-Assad mdogo wake Rais.
Assad ana mashirika ya ujasusi kama matatu hivi yanayojitegemea na yanachunguzana, kama sikosei jeshi wana la kwao, Airforce ina la kwake (nahisi sababu baba yake Hafez alipindua kutokea Airforce aliasisi hili), polisi wana la kwao, wizara gani sijui mambo ya ndani wana la taifa kiujumla.

Assad anaongoza nchi ambayo dhehebu lake na jamii yake ni minority hivyo wanajeshi wengi sio dini yake wala jamii yake. Anachokifanya anakusanya wanajeshi kutoka maeneo yanayomuunga mkono ila maofisa wa juu wa majeshi yake ni kutoka minorities. Si rahisi Msuni kutoka Allepo awe ofisa mkubwa kwenye jeshi la Assad. Kwa hiyo jeshi maofisa wake sio competent bali asili, eneo, uchawa na dhehebu ndio vinawabeba.

Hata kwa wanajeshi wenyewe, baada ya vita kutokea kulikuwa na forces recruitment. Serikali ya Assad ina rushwa kubwa na ufisadi kupindukia, na jeshini hachukui hatua kuzuia ilimradi maofisa ni machawa wake anawaachia nafasi "wale" ili walinde serikali yake huku wanalinda matumbo yao. Kwahiyo recruitment inakwepwa endapo kijana familia yake ina hela kutoa rushwa asiende jeshini. Recruitments waliopo jeshini hawako motivated, huwezi wapiganisha na waasi au magaidi ambao wengi wamejiunga kwa kutaka wenyewe.

Training ya Syrian Arab Army ni dhaifu. Wana miaka zaidi ya 10 vitani ila hawana defensive lines, hawajui repelling of fast attack, hawajajipanga dhidi ya drones, hawajui kufanya retreat wakiondoka sehemu wanakurupuka wanaacha silaha ziko intact zinachukuliwa na adui badala kuziharibu au kuzihamisha.

Na kwa sababu ya vikwazo vya kiuchumi na hali ngumu nchini Syria, Assad alitumia vyombo vya usalama kuzalisha kipato kwa madawa ya kulevya. Wanasafirisha shehena ya madawa pale Middle East angalau wapate kipato cha kudunduliza juu ya hali yao ngumu.

Kwa mazingira haya usitarajie Syria Arab Army iwe na maajabu, hata hivyo Syria hawajawahi kuwa na jeshi la maana katika historia. Ila sasa wamezidi yani kama mgambo.
Ina maana Hezbollah na wanamgambo kutoka Iran ndio wanaopigana badala ya jeshi la Syria ?.

...Sasa wafadhili wake wote wana hali ngumu, Assad atakiona cha moto.
 
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Sunni hakuna mgawanyiko! Sunni inaundwa na ncha 4.

Hizi ncha zinaitwa madheheb, ndipo kuna Hanafi, Hanbali, Maliki na Shafii.

Hakuna mahali popote ukasikia hayo madheheb yamegombana, hakuna!
Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki kwa ukubwa ni madheheb ya Shafii. Madheheb yaliyobakia ni yana wafuasi wachache kama shia, ibadhi n.k na hatujawahi kusikia hata siku moja wakigombana.

Sufi siyo dheheb, sufi ni mojawapo katika matawi ya elimu mtu anaamua kushughulika nayo! Wanasema sheria ni timilifu la kiwiliwili, Sufi ni timilifu la kiroho. Kwenye usufi wapo madheheb ya Shafii, Hanbali, Hanafi na Maliki. Wote utawakuta humo. Hilo ni tawi la elimu la tazkiya (elimu ya kuitakasa nafsi).

Kwenye usufi kuna madheheb napo!
Kuna Shisti, Naqshibandi, Sahrawardii, Qadir, Shadhalii n.k

Mtu anaweza akawa sunni na asiwe kwenye usufi n.k

Wahabi ndiyo Salafi na ndiyo Answar Sunna. Hayo majina yote yanawakilisha dhehebu moja Siyo dhehebu tofauti.

Hili dheheb lipo tofauti na madheheb yote ya juu niliyoyaorodhesha. Hili dheheb linapingana na madheheb yote ya hapo juu kwa namna yake. Na madheheb ya hapo juu yanapingana na Salafi au wahab kwa namna yao pia.

Kupingana kwao ni kielimu si kimapigano ya kimwili.

Na salafi au wahab wamegawanyika! Wapo ambao wenye msimamo mkali sana na wapo ambao wapo safi hawana matatizo yoyote kwenye jamii.

Tanzania na ukanda wa Afrika mashariki wengi wao ni Sunni madheheb ya Shafii, ambapo humo kwenye Usunni wapo ambao wanaofuata sufi.

Madheheb mengine ni Shia, Ibadh Wahab/Salaf n.k
 
Wahabi=salafi na kila kundi linalofadhiliwa na Saudi litaitwa Wahabi/Salafi.

Ila kama una hata Abcd za Hao salafi utaona ni Bullshit tu. Katika madhehebu yote ya kiiisilamu wao ndio wa mwisho kwenda Jihadi kutokana na akida yao. Hata Unapoongelea Ulamaa mkubwa Wa Salafi Zama Zetu Sheikh Albani Fatwa yake ni wapalestina Waondoke Palestina hii hapa


Hapa Tanzania tuna salafi wengi mno watu kama Kina Kishki ama Answari sunna etc, ushawahi hata siku moja kuwasikia wana Criticise Serikali? Kwa Imani yao Kiongozi Anakuwa criticised kwa siri tu, unamfata kimya kimya unamuambia

So kusema Salafi ndio wanaongoza hizo Jihadi ni Ignorance ya wasio waisilamu kuhusu Uisilamu.

Kwenye Uisilamu Vita ama Jihadi Zinatokana na Fatwa za Scholars, Hawa maulamaa ndio wanatoa fatwa fanya hivi ama usifanye hivi, sijawahi ona maisha yangu yote hata Scholar mmoja akihalalisha hivyo vikundi, na siku Zote makundi kama Isis na Al Qaeda utaona Scholars wengi wana Wa Refer kama mbwa wa Motoni, Sababu Media ina wa refer kMa Salafi haimaanishiwapo Sahihi na Uisilamu ama Scholars wa Kiisilamu wa nakubaliana na Hilo.
Hicho kinchofanywa na makundi kama HTS huko Syria kinafaa kuitwa Jihad?

Au ni vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgogoro wa kisiasa uliovalishwa vazi la kidini Ili kuvutia waumini kushika silaha ?
 
Waasi wa Kisunni wamelivamia Gereza kuu la Aleppo na kuwafungulia Wanamgambo wa ISIS waliokuwa wamefungwa hapo.

Vita inazidi kuchukua mkondo wa Kigaidi.
 
Hicho kinchofanywa na makundi kama HTS huko Syria kinafaa kuitwa Jihad?

Au ni vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na mgogoro wa kisiasa uliovalishwa vazi la kidini Ili kuvutia waumini kushika silaha ?
Sio jihadi na ndio point yangu hii, HTS walikua wanaitwa Al Nusra Aka Al Qaeda, sijawahi maisha yangu kusikia Ulamaa yoyote wa Kiisilamu akitoa Fatwa kwamba Al Qaeda Wanapigana Jihadi. Na hata ukiangalia matendo yao hayaendani na Uisilamu bali ni Exactly matendo Yaliyofanywa na wakoloni ambayo kila siku tunaimbishwa kwenye Somo la Historia, Divide and Conquer.
 
Sio jihadi na ndio point yangu hii, HTS walikua wanaitwa Al Nusra Aka Al Qaeda, sijawahi maisha yangu kusikia Ulamaa yoyote wa Kiisilamu akitoa Fatwa kwamba Al Qaeda Wanapigana Jihadi. Na hata ukiangalia matendo yao hayaendani na Uisilamu bali ni Exactly matendo Yaliyofanywa na wakoloni ambayo kila siku tunaimbishwa kwenye Somo la Historia, Divide and Conquer.
Huwezi kusikia Ulamaa yeyote akisema hadharani kwamba Al Nusra au Al-Shabaab wanapigana jihadi ya haki kwa sababu atawekwa kwenye us terror watch list na maisha yake yatakuwa magumu sana.
 
Huwezi kusikia Ulamaa yeyote akisema hadharani kwamba Al Nusra au Al-Shabaab wanapigana jihadi ya haki kwa sababu atawekwa kwenye us terror watch list na maisha yake yatakuwa magumu sana.
UNAFKIRI Maulamaa they even care about USA? Pengine hata hujui Ulamaa ni nini, mtu akishafikia hio level maisha ya Dunia hana tena.

Hapo Saudi kuna Scholars wapo Against government hadi wanauliwa they even don't care na bado wanasema ukweli, hayo mambo ya kuwa dubbed terrorist na government ni ya kwenu, kwa Mtu level ya Scholar haya wezi mtingisha imani

Kwenye uisilamu hakuna Kumung'unya maneno kama ni kweli ni kweli kama so kweli bali si kweli.

Na kuna sehemu kibao dunia ya sasa Mathalan kama Palestina scholars kadhaa wanakubali ile ni Jihadi, so sio suala la kuogopa ama kutoogopa bali ni suala la ukweli na haki na uovu.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa Jamii ya Wakristo imeanza kuchinjwa huko Idlib hawa Waasi wa Kisunni ni Magaidi wa ISIS walichobadilisha ni jina tu.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa Jamii ya Wakristo imeanza kuchinjwa huko Idlib hawa Waasi wa Kisunni ni Magaidi wa ISIS walichobadilisha ni jina tu.
Mbona hueleweki? Au umeamua kujifyatua. Mara unamnanga Asad na kuwasifia Waasi na Israel. Mbona kama lishoga jipya mtaani.
 
Mbona hueleweki? Au umeamua kujifyatua. Mara unamnanga Asad na kuwasifia Waasi na Israel. Mbona kama lishoga jipya mtaani.
Mimi naongelea mgogoro wa Syria kama ulivyo, lakini inavyoonekana hao Waasi wa Kisunni hawajaacha mbinu zao za kigaidi ambazo mwanzo walisema wameachana nazo na kuzihakikishia Jamii za Minorities Wakristo Druze nk. Kuwa hawatazivamia na kuwachinja.

Lakini sio kweli kuna taarifa kuwa huko Idlib Jamii za Kikristo zimeanza kuuwawa na Waasi.
 
Ndege za Kivita za Marekani A10 'Warthog' zimeanza kuwasaidia Waasi karibia na Mji wa Deir Ez Zor.
 
Back
Top Bottom