Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Vita vya Syria vina mchanganyiko sana, ila dikteta Assad ni uovu wenye afadhali (lesser evil) kuliko waasi Wanajihadi

Waasi wameshindwa kuuteka Mji wa Hama wamekumbana na upinzani mkali kutoka kwa Majeshi la Syria Arab Republic +Russia+Hezbola+ Shia Millitias.

Je hii offensive ya Waasi ndio imefikia mwisho?! Je wataanza kurudishwa nyuma?! Yetu macho na Popcorns 🍿 na Bia bariidi.
Ila we jamaa wewe
 
Wamefanikiwa kuuteka Mji wa Hama na sasa wanaelekea Homs😁

Kutokea Hama kwenda Homs ni Kilometa 44 nadhani kufikia kesho Vita vimehamia huko.

Wananchi wameanza kuikimbia Homs na kukimbilia Damascus.
Huu meaka umeondoka na damu nyingi sana za wasio na hatia kuanzia Cuba Hadi Caracas Venezuela
 
Sasa hao Israel ndio wanafadhili hayo makundi,

Siku zote nawaambia humu Huyo Israel ndio adui yenu na sio hao viongozi wa hizo nchi, na ndio maana unaona Wakristo WA lebanon wameamua kufadhili Hezbollah wa nafahamu nini kitawapata ikiwa Israel atakua na influence za Hio Nchi.

Hao Al Qaeda Wa Syria wana full Silaha za Marekani na wakiumia kutibiwa ni Israel.

Syria chini ya Assad kabla ya 2011 makundi mengi yaliexist pamoja, yes ana mabaya yake ila kama unavyosema ni lesser evil.

Same kwa Sadam na viongozi wengine wa huo ukanda.

Tatizo hiyo dini iliyobuniwa na muarabu, imekua kero duniani kote.
 
Malysia, Indonesia na Brunei ni mataifa ambayo majority ni Wasuni, Bangladesh huwa kuna machufuko ya mara kwa mara kati ya Waislamu na Wahindu na Wabudha pia katika baadhi ya maeneo.
US na wapambe wanawaunga mkono wamng'oe jamaa na baada ya kumng'oa wakaanza mambo yao utawasikia wale wale wakiuliza imekuwaje taifa limefika pale dunia iuangane kuwapiga kama vile hawakujua walichokuwa wanakitengeneza.
 
Breaking; Waasi wameshika Mateka wengi katika mapigano ya Usiku wa kuamkia leo miongoni wa waliotekwa ni Wanamgambo wa Madhehebu ya Shia kutokea Iraq.

Msemaji wa Waasi anasema Upinzani umeanza kuwa mkali lakini Allah yuko na wao.

Source: Jaz English

Kwahiyo sasa Shia Millitias wameshapenya ndani ya Syria mbona tena na wao wanasarenda?!
 
IDF imeshambulia Daraja la mpakani na kukata mawasiliano baina ya Syria na Lebanon.

Mchezo umeisha kwa Ayatolah's Corridor 😂

Source:Aljazeera
 
Ndege za Urusi zimeshambulia leo kutwa Mji wa Waasi wa Idlib ninadhani kuna Intelligence kuwa Silaha zimeshushwa usiku.

Ninachokiona ni kwamba safari hii Assad anaweza kuondoka kwasababu baadhi ya Vikosi vya Waasi vimeizunguka Hama na vinaelekea Homs vinataka kukata mawasiliano.
Aondoke tu huyo fedhuli,amejaa damu za wananchi wake...Tena akipatikana hai akachinjwa itakuwa Bora zaidi
 
05e0f2d8-73b5-470a-96b7-9efd22596f7e_w408_r1_s.jpg

Daraja katika kituo cha mpaka wa Lebanon na Syria limeshambuliwa na kuteketezwa na Ndege za IDF na kukata mawasiliano ya Ardhini baina ya Ayatolah na Hezbola.
 
Yani Kuna muda hadi unasikitika mkuu.

Kama ukisema ni uislam mbona Malaysia,Indonesia,Brunei waislam wengi na hayo hayatokei!?

Bangladesh Kuna waislam wengi na dini zingine kibao ila wanaungana chini ya bendera moja ya nchi.

Hata Sheikh Hasinah alipopinduliwa na wananchi waislam,wakristo kwa wapagani waliungana chini ya kauli moja.

Sijui waarabu wana nini kichwani kiasi hawana umoja!?
Nyinyi waafrika mna umoja?
 
Ukiangalia kwa undani makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya utawala wa dikteta Bashir Al-Assad nchini Syria hayatoi matumaini mema kwamba endapo yatafanikiwa kumng'oa Assad siku za usoni za Syria zitakuwa njema chini ya utawala wao mpya, makundi yanayompinga Assad ukiondoa Wakurdi nusu yake ni makundi ya kijihadi yenye msimamo mkali. Haya makundi yakishika madaraka ina maana Syria itageuzwa taifa la kidini rasmi na inaweza kugeuka changamoto nyingine kubwa si kwa raia wa ndani tu bali hata nchi majirani ikiwemo Israel.

Familia ya Assad ambayo ni alawites , tawi la Washia lenye msimamo tofauti na sehemu kubwa ya Waislamu ikiwemo kuruhusu matumizi ya pombe na kutoamini kabisa wanawake kuvaa hijabu ni takwa la lazima la dini wameiendesha Syria kama taifa jumuishi la imani zote kwa muda mrefu japo chini ya utawala wa chama kimoja cha Baath, hakuna uhakika kama waasi watakoingia kumrithi Assad watadumisha taifa jumuishi la Syria lisilo la kidini au lenye mrengo wa upande mmoja zaidi wa kidini na hapo ndipo migogoro itapozidi na kuharibu mambo kabisa.

Ni kweli kihistoria Syria chini ya utawala wa familia ya Assad haujawahi kuwa rafiki sana wa Israel lakini pia haijawahi kuwa utawala wa uadui wa kiwendawazimu sana kuipasua kichwa Israel, mara nyingi imejizuia au imejiepusha kuingia katika migogoro isiyo ya lazima na Israel. Mtihani mkubwa ni kwamba Syria ya Assad imekuwa kibaraka wa Iran wakati wote ambaye ni adui mkubwa wa Marekani na Israel.
Assad ni km Putin waliwanyima wamarekani ma western kuchimba mafuta/gas/madini ndio maana akapigwa jina la dictatorship ila undani wake nikuwanyima mali,as long as haupo na western majina yote ya kishenzi utapewa ni sawa na jiwe wa TZ alipokua anawanyima Mali walimwambia anaviolate human kwakua aliwanyima na kuwapiga vita, bukinafaso wao wameingia wanajeshi hakuna swali
 
Habari njema ni kuwa huyo fedhuli aliyeua maelfu ya raia wake,hayupo madarakani na kakimbilia kwa mabwana zake,asubiri kujibu mashtaka yake Kama sio hapa duniani basi kesho akhera
 
Sunni imegawanyika katika madhebu/sects mbalimbali, wapo Wahhabi wanaojulikana kwa misimamo mikali na kukosa uvumulivu dhidi ya imani nyingine, magaidi wengi ndio wanatokea mkondo huu. Wapo salafi, sufi, hanafi n.k Ukiwa bongo sio rahisi uelewe kwa sababu hakuna hii migawanyiko kwa uwazi kutokana na udhibiti wa BAKWATA.
Hakunaga kitu wahabi, hilo neno ni kama mtu aseme plutnumz, mwingine aseme dangote, mwingine aseme mtoto wa Tandale mwingine aseme Simba, mwingine aseme Baba Tiffah wote wakilenga Diamond.
Kwa hiyo Salafy, Sunni walipewa hiyo a.k.a ya wahabi na watu wanaochukia itikadi zao, halafu tambua kuwa wahabi na hanafy ni watu Ulamaa wakubwa na siyo dhehebu/ sect.
Jitahidi ukiona jambo pitia maandiko ulichimbe vyema kuliko kulisha watu matango pori
 
Back
Top Bottom