Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Nchi hii ukiifuatilia kwa umakini utagundua Corona iliingia kipindi kile anakagua daraja la Ubungo akapitia moro, then Dodoma kwenye mawe then to Chato.

Kiashiria cha kutokuwepo kwa corona nchini ni mwenyekiti wa chama kuwa katika ofisi mbili ile ya Dodoma au Dar.

Asipokuwa katika ofisi hizo endelea kujua kuwa hali ni mbaya nawe kama una uwezo jichimbie ndani mpka bwana mkubwa akitoka chato nawe utoke.
 
Waliokuwa wanadhani kuwasweka ndani, kuwanyanyasa wapinzani na kuitetea serikali kutawaweka salama dhidi ya kutekwa, kushambuliwa na hata kuuawa... WAMEKUFA KWA CORONA

Walioshangilia mbunge mwenzao kuuawa eti ni mhaini wakidhani wao wapo salama, MMOJA KAFA KWA CORONA na MWINGINE HATUI CORONA YAKE IMEFIKA WAPI

Anayekimbia majukumu makubwa na kujificha mapangoni akiogopa kufa kwa CORONA huku akiwaachia mzigo vibarua wake, ATAKUFA KWA SHINIKIZO LA MOYO
 
Nchi hii ukiifuatilia kwa umakini utagundua Corona iliingia kipindi kile anakagua daraja la Ubungo akapitia moro, then Dodoma kwenye mawe then to Chato.

Kiashiria cha kutokuwepo kwa corona nchini ni mwenyekiti wa chama kuwa katika ofisi mbili ile ya Dodoma au Dar.

Asipokuwa katika ofisi hizo endelea kujua kuwa hali ni mbaya nawe kama una uwezo jichimbie ndani mpka bwana mkubwa akitoka chato nawe utoke.
Watu mna akili ya ziada, du.....!
 
Jamani tujaribu kuwa serious kidogo. Utawatoaje watu hofu ya Corona wakati wewe mwenyewe unaonekana una hofu na hiyo hiyo Corona?

Hivi tunajidai kuzuga kwa faida ya nani? Mbona mfumo wako wa maisha hapo Chato unaonesha kabisa wewe ndiyo una hofu kubwa ya Corona kuliko sisi?

Mimi nitatoa hofu ya Corona mpaka nikikuona wewe pia hauna hofu vingine ni bora kila mtu abaki na hofu yake
 
Za kuambiwa changanya na zako!Mimi familia nilishaikimbizia huko kijijini kwa bibi yao!Nimebaki napambana mwenyewe!Nitakapoona karudi mjini nami ndio nitaanza kujua kuna ahueni na nitatafakari kama niirudishe familia au la!

Sasa we waache tu wachumia tumbo waendeleze mapambio badala ya kuiga namna jamaa alivyoficha familia yake mbali kabisa,wenye uwezo wajiongeze!
 
Ishi kwa nafasi yako mkuu ..kinga ni bora kuliko tiba


It is never too late to begin. Start now
 
Uzuri wa bahati hii vita kila mtu anajipambania mwenyewe! Nashangaa unapomtegemea mwenzako na wakati kukupa uhuru wa kuchagua mwenyewe!

Kama unaweza jifungie ndani, kama huwezi toka nje ukapambane. Hii siyo vita ya siraha za nuclear!

Chamsingi tu, serikali iko kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais ni binadamu kama wewe. Sio kila analolisema lazima ulifuate. Use your common sense. Use your brain. Rais sio malaika. By the way yeye kaogopa sana tu. Hofu imemfanya hadi akakimbia majiji na kukimbilia kijijini.
 
Samahani mkuu, umetafakari kabla ya kuandika
Sana tu. Chukua hatua. Mfano kama ni lazima uwe unatoka unaweza kujitenga na familia yako, ukawapeleka sehemu tofauti kabisa, ukahakikisha wanapata chakula, ww ukaendelea kupambana huku ukichukua tahadhari.

Usisubiri serikali itandaze polisi nchi nzima kuzuia watu wasitoke. Pigania maisha yako na familia yako mwenyewe. Acha kulalamika.
 
Wiki iliyopita waziri mkuu wa uingereza Boris Johson alirejea ofisini mara baada ya kuruhusiwa hospitalini aliko kuwa amelazwa kwa kuugua COVID19.

Waziri mkuu huyo akiongea na watu wake. Aliwashukuru wafanyakazi wa sekta ya Afya kwa namna wanavyo fanya kazi zao kuokoa uhai wa raia wa nchi yao. Pia aliwapongeza na kuwashukuru Madaktari na wadumu wa Afya kwa namna walivyo pigania kuokoa uhai wake kipindi akiwa hospitalini.

Tukiacha habari hizo za Mabeberu yule Rais mwenye kujiita mzalendo wa nchi ya Kusadikika, na aliyekuwa akiwasema sana mabeberu kuwa hayana huruma, taarifa tulizo nazo ni kuwa amekimbia Makasri yake yote mawili na kutokomea kujificha nyumbani kwake kusiko julikana.

Huyu ndiye rais ambaye hujifanya mzalendo na kupenda maskini. Hupenda kuwasimanga Mabeberu ili ajioneshe yeye kuwa ni mwema amekuja kuwakomboa watu. Taarifa zinasema Raia wake wanakufa kama kuku na kuzikwa mchana na usiku.

Anahimiza watu wachape kazi wakati yeye kajificha kulinda uhai wake. Vilio vya raia wake vinasikika mchana na usiku lakini hajali. Watu wachache wameanza kung'amua kwamba tuna majanga mawili. Kuna janga la Covid19 na janga la hili jamaa Nondo mla watu. Majanga yote mawili lazima yaondolewe.

Wakati Waziri mkuu wa uingereza anawapongeza watumishi wa Afya na kuwatia moyo kuendelea kupiga kazi ktk mazingira magumu. Huyu Nondo mla watu eti anaongea na Migambo. Anaita viongozi wa Migambo na kuwapa maelekezo waendelee kuruka na kukanyaga raia wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom