Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Vita ya Corona: Nahodha wetu katelekeza chombo Baharini, tutaponaje?

Gellangi,
Unadai [/]Kinachoumiza zaidi ni namna baadhi yetu tunavyoteteana hata kunapokuwa na uzembe kwenye hatua zinazochukuliwa kutulinda na Corona[/I], je, umejitathmini wewe mwenyewe, fanilia, ndugu, jirani, na rafiki zako kiwango cha kuzingatia ushauri wa kinga dhidi ya maambukizi na kubadili tabia?

Je, ni hatua gani zaidi zichukuliwe na Serikali kutulinda na Corona?
 
mwengeso,
Ninajitahidi kufuata baadhi ya ushauri unaotolewa na serikali Mimi na familia yangu.Kuhusu majirani, Ndugu, marafiki nawashauri ila sina mamlaka ya kuwadhibiti wanapokiuka.

Kuhusu hatua za kuchukuliwa na serikali ni pamoja na kuhakikisha vifaa vya kujikinga vinapatikana katika ngazi zote na kwa bei nafuu/bila malipo,kuhakikisha upatikanaji wa vitendanishi vya uchunguzi, vifaa tiba, PPE kwa watoa Huduma za afya,

kuhakikisha mazingira bora na salama vya quarantine, strong surveillance and updated reports nk.Tukiona serikali IPO kimya lazima tupaze sauti kwa pamoja vinginevyo tunaangamia.

Twende pamoja.
 
Unadai [/]Kinachoumiza zaidi ni namna baadhi yetu tunavyoteteana hata kunapokuwa na uzembe kwenye hatua zinazochukuliwa kutulinda na Corona[/I], je, umejitathmini wewe mwenyewe, fanilia, ndugu, jirani, na rafiki zako kiwango cha kuzingatia ushauri wa kinga dhidi ya maambukizi na kubadili tabia?

Je, ni hatua gani zaidi zichukuliwe na Serikali kutulinda na Corona?
Hatua ya kujifukizia mvuke sitaifanya maana inafanana na matendo ya ushirikina.
 
Hatua ya kujifukizia mvuke sitaifanya maana inafanana na matendo ya ushirikina.
Ushirikina tena, aloo. Haya ni maelezo na maelekezo ya mtaalamu.

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Yunus Mgaya alisema wanapendekeza aina tatu za mchanganyiko wa mimea tiba kutengeneza joto tiba au mvuke. Aliutaja mchanganyiko wa kwanza wa mimea ambayo wananchi wanaweza kuutumia ni mchanganyiko wa majani ya mkaratusi, majani ya kivumbasi au kashwagala na majani ya mchaichai.

Aina ya pili ni mchanganyiko wa majani ya mchaichai, karafuu, tangawizi iliopondwapondwa na majani ya mlimao. Aliutaja mchanganyiko wa tatu kuwa ni majani ya mwarobaini, majani ya mpera, mchaichai na majani ya mlimao.

Kwa mujibu wake, tiba joto hiyo au mvuke ni muhimu kwani inasaidia kuongeza kinga ya mwili, kufungua njia ya hewa na kukirarua kirusi cha corona kama bado kiko kwenye njia ya hewa na hakijaingia kwenye mapafu.

Alisema tiba ya kujifukiza haisaidii kama tayari kirusi cha corona kimeshaingia kwenye mapafu, hivyo mgonjwa anatakiwa kupewa matibabu mengine ikiwemo antibiotic.

Joto nyuzi 50-70 “Joto la mvuke linatakiwa liwe kati ya nyuzi 50 hadi 70, likizidi linaweza kuumiza njia ya hewa, mtu anatakiwa avute mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni, watu wazima wavute kwa dakika nane hadi kumi na watoto kuanzia umri wa miaka saba wavute kwa dakika mbili hadi nne, watoto chini ya miaka saba hawaruhusiwi kutumia tiba hii,” alisema Profesa Mgaya.

Kwa kuwa mvuke una kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni, alisema watu wenye matatizo ya kupumua hawapaswi kutumia tiba hiyo kwani wanaweza kupoteza maisha, pia wanaotumia wasijifukize wakati sufuria iko kwenye jiko la mkaa bali iwekwe chini au mahali pengine kwa kuwa mkaa hutoa hewa yenye sumu hatari kwa binadamu.

Kuhusu maandalizi ya dawa hiyo, Profesa Mgaya alisema hatua ya kwanza ni kuchemsha maji ya lita tano au kumi hadi yachemke, kisha yawekwe majani na kuyafunika na kuyachemsha kwa dakika tano tu.

Alisema dawa ikichemshwa kwa zaidi ya dakika tano inakuwa imepikwa na haifai kwa tiba kwa sababu virutubisho muhimu vinakuwa vimepotea kwa njia ya mvuke.

Alisema wakati wa kujifukiza mtu anaweza kujifunika kwa blanketi au shuka au taulo zito ili mvuke usipotee, na baada ya kujifukiza muhusika asipewe maji baridi ya kunywa kwani ataharibu tiba bali apewe glasi ya maji ya moto au chai.

Kuhusu kipimo cha dawa hizo, alitoa kipimo kwa mchanganyiko wa kwanza tu ambapo mtu anatakiwa atumie gramu 50 za majani ya mkaratusi na gramu 50 za kivumbasi na gramu 20 za mchaichai
 
Hapa naandika kwa majonzi kwa kusikia jinsi Watanzania wenzetu wanavyougua Corona na wengine kupoteza maisha. Poleni nyote.

Kinachoumiza zaidi ni namna baadhi yetu tunavyoteteana hata kunapokuwa na uzembe kwenye hatua zinazochukuliwa kutulinda na Corona.

Kuna wanaosema Nahodha wetu ni shujaa, mwenye uthubutu na tupo salama ilhali abiria tunaona hatari iliyopo mbele yetu.

Nahodha wetu tunaambiwa yupo mapumzikoni. Je, tukisema kajitosa baharini na kutuachia chombo kielee kwenda kuzama tunakosea?

Corona bila lockdown itatumaliza, ilikuwa Arusha, Dar na Zanzibar hatukuona haja ya lockdown eti tutakufa njaa. Sasa tuna wagonjwa mikoani na hakuna kinachoonekana kufanyika, hatujaamua bado kulock maeneo yenye wagonjwa.

Tunafahamu kuwa hakuna dawa, chanjo, vifaa tiba, maabara za uchunguzi na vifaa vya kujikinga hasa kwa watoa huduma za afya.

Tuamini kuwa tupo salama? Tuamini kuwa Nahodha hajajitosa na kuacha chombo katikati ya mawimbi makali?
Kapicha Tafadhali 🤔🤔🤔
 
Kwanza nitoe salamu na pole zangu za dhati kwa waathirika.Mungu awape nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.Tunaamini hili nalo litapita kama yalivyopita mengine.Na sisi ambao kidogo tuko wazima wa afya tumshukuru Mungu Alhamdulillah bila kusahau kinga ni bora kuliko tiba hivyo tuendelee kuchukua tahadhari za hapa na pale kujikinga.

Nafahamu tupo kwenye wakati mgumu kama Taifa.Tupo kwenye janga ambalo viongozi wakilifumbia macho basi wengi wetu tutapukutika kama majani ya muembe kipindi cha kiangazi.Tupo kwenye wakati ambao umaridadi wa viongozi kwenye kuongoza mitumbwi hudhihirisha umakini wao.Lakini hili kwa taifa letu la ahadi kiongozi wetu kashindwa kabisa kutuongoza.Katuacha hadharani kwenye mataa

Aliwahi kusema Maya Angelou "Leader is the one who knows the way,shows the way and lead the way " kwamba kiongozi ni yule anayejua njia,ni yule anaeonyesha njia na ni yule anayeongoza njia.

Kiongozi wetu kwa alikotokomea ni dhahiri shahiri kashindwa kuongoza njia.Ni muda wake mwafaka kuachia madaraka

Tuendelee kuchukua tahadhari
Waislamu Wenzangu mfungo Mwema 🤟
Nawasilisha
 
Kiongozi kashindwa kutetea jahazi.Kaonesha udhaifu wa hali ya juu kabisa.Kakosa la kufanya kabaki kujichimbia ndani.Kiongozi kashindwa kuongoza
Tumekosa imani nae hakika 😔
 
Kiongozi kashindwa kutetea jahazi.Kaonesha udhaifu wa hali ya juu kabisa.Kakosa la kufanya kabaki kujichimbia ndani.Kiongozi kashindwa kuongoza
Tumekosa imani nae hakika [emoji17]
Jamaa ni muoga na mwepesi wa kujificha kama mboni za macho.








kush and Wisdom
 
Nadhani atawafaa sana huko akiwa diwani wao!Haiwezekani aende kujificha Chato na kuacha majukumu yake ya msingi!Hadi kuapisha wateuliwa wake ameenda kuwaapishia Chato,katika umri wangu sijawahi kuona!
Kama anapapenda sana huko Chato na si kukimbia Corona basi mwaka huu achukue fomu agombee udiwani ili aishi huko moja kwa moja!

Naunga mkono hoja!😀😀

Ni maoni yangu tu!
 
Acheni kusikiliza uzushi wa mtandaoni Rais Magufuli anafanya kazi
 
Lakini kusema ukweli ameonyesha udhaifu mkubwa sana kama kiongozi.
Nadhani atawafaa sana huko akiwa diwani wao!Haiwezekani aende kujificha Chato na kuacha majukumu yake ya msingi!Hadi kuapisha wateuliwa wake ameenda kuwaapishia Chato,katika umri wangu sijawahi kuona!
Kama anapapenda sana huko Chato na si kukimbia Corona basi mwaka huu achukue fomu agombee udiwani ili aishi huko moja kwa moja!

Naunga mkono hoja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom