Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhan imeeleweka!!VITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.
Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.
Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’
Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.
Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.
Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.
“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.
“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.
“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.
Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.
“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.
“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.
“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.
Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.
Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.
Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.
Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.
Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.
Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.
“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.
“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.
“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?
“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.
“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.
“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.
Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.
Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.
Source: Tanzania-Panorama
Hahahahah na haituhusu🤣🤣kama ndiyo hivyo basi hao watoto wasitusumbue, tuna mengi ya kufanya.
Wazungu, mtoto anakuwa na maisha yake pasipo tegemea mali ya mzazi. Ikitokea mzazi amefariki, mtoto au watoto uwa hawana kielehele na mali ya mzazi wao. Wanachoangalia mzazi aliacha wasia gani? Wanafuata wasia, na si waafrica ambao wakati mwingine wosia uwekwa pembeni na kuanza mapambano na ugomvi wa mali. Wazungu wanaheshimu wosia wa marehemu. Hata marehemu akiwa kaandika mali yake apewe mbwa au paka, hakuna atakaye enda mahakamani kupinga. Wanasema ni uamuzi wa marehemu, kwakua mali ni yake.Utajiri wa familia za kiafrika haudumu kwa generation zaidi ya 1
Na hapa ndipo wazungu, wahindi na Waarabu wanaptupiga gepu
Kila mara utasikia migogoro ya kugombea mali za tajiri mweusi mara Mengi, mara bilionea Msuya, Lwakatare, kuna yule Mrema wa Ngurdoto n.k
Ila ni mara chache sana kusikia tifu kama hizi kwa matajiri wa ki Asia au kizungu.
Wazungu na wahindi utajiri wao ni wa kurithishana vizazi na vizazi.. Ila kwa mswahili utajiri wa baba unasamabaratika akishjakufa, watoto na wajukuu wanaanza upya, kwa mtindo huu hatutakaa tuwafikie hata tupewe karne 100
Saccos kama hizi zote mwisho wake ni pale muanzilishi wake anapokufa. Hii ni pamoja na zile za akina Gwajima, Moses Nkolola, Mwakatobe, kakobe n.kVITA ya kugombea mali za aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God - Mlima wa Moto, Marehemu Mchungaji Getrude Rwakatare sasa imeshika kasi huku ikizidi kuwagawa watoto wake.
Taarifa za kuwepo kwa vita hii zimekuja ikiwa ni miezi kadhaa baada ya mtoto mkubwa wa kiume wa Marehemu Rwakatare, anayefahamika kwa jina la Tibe Kenneth Rwakatare kumuandikia barua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akimueleza jinsi ndugu zake wanavyokiuka sheria kwa kutenda makosa ya jinai, akiwatuhumu kughushi nyaraka za mauzo ya baadhi ya mali za marehemu mama yake, Mchungaji Rwakatare.
Tibe Kenneth Rwakatare aliandika barua hiyo Disemba 31, 2021 ikiwa na kichwa cha maneno kinachosomeka ‘mauzo batili plot no 259 Udindifu Bagamayo.’
Katika barua hiyo, Tibe aliandika kumweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa uuzwaji wa kiwanja hicho umehusisha nyaraka za kughushi pamoja na kutolipwa kwa kodi stahiki za Serikali.
Akithibitisha kuandika barua hiyo, Tibe aliiambia Tanzania PANORAMA Blog kuwa amedhulumiwa haki yake na ndugu zake hivyo hakuwa na jingine zaidi ya kuandika barua hiyo.
Wakili kiongozi wa Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza Advocates, Alloyce Komba ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake, amesema adhabu itakayowakabili watuhumiwa wakibainika mahakamani kutenda jinai hiyo ni kifungo.
“Kosa la kughushi, adhabu yake iwapo mahakama ikimtia hatiani mtu kwa ushahidi usio na shaka yoyote ni kufungwa kwa mujibu wa kifungu cha 337 cha sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019.
“Mtu anapaswa kuripoti polisi kosa lolote la jinai linalofanywa na mtu yoyote ili mradi awe na ushahidi wa kutosha.
“Ni kosa pia kunyamazia kosa la jinai. Ndiyo maana mtu hukosa kwa kutenda (commission) au kutotenda (omission), mfano kutomzuia mtoto kutumbukia kisimani wakati unaona anacheza karibu na kisima,” alisema Wakili Komba.
Mwanasheria mwingine aliyezungumza na PANORAMA kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa alisema tuhuma zilizotolewa na Tibe dhidi ya ndugu zake ni nzito na iwapo zitathibitika mahakamani hawatakwepa mkono wa sheria.
“Sheria zipo lakini inashangaza watu wanatenda makosa ya makusudi kama haya ambayo adhabu yake ni kali.
“Huyu anayewatuhumu wenzake naye hayuko salama kwa sababu ni wazi anajua vema jinsi ndugu zake walivyotenda hiyo jinai, walivyoghushi kwa sababu ni ndugu zake hivyo alipaswa kutoa taarifa polisi.
“Sasa inashangaza kijana msomi kukaa kimya huku akijua kuna jinai inafanyika. Kwa vile kalipeleka kwa waziri tumpe nafasi ya kulifanyia kazi,” alisema.
Kwa mujibu wa kifungu cha 338 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania, toleo la 2019 ambayo Tanzania PANORAMA Blog imeiperuzi inaeleza kuwa mtu akibainika mahakamani kwa kughushi wosia, hati za umiliki ardhi, hundi n.k adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Hilo likiwa halijapoa, mtoto mwingine wa kiume wa Marehemu Mchungaji Rwakatare anayefahamika kwa jina la Muta Robert Rwakatare ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizungumza na mwandishi wa Tanzania PANORAMA Blog na kumshutumu ndugu yake Tibe Kenneth Rwakatare kwa kutwaa kimabavu Shule ya Sekondari ya St. Mary’s International School, Dodoma Campus ambayo ni mali waliyoachiwa na marehemu mama yao.
Muta alieleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na Marehemu Mchungaji Rwakatare enzi za uhai wake lakini hivi sasa Tibe imeibadilisha jina na kutwaa umiliki wake.
Alisema ikiwa chini ya umiliki wa mama yao, ilikuwa ikijulikana kwa jina la St. Mary’s International School, Dodoma Campus, lakini sasa baada ya kubadilishwa jina inafahamika kwa jina la St. Mary’s Dodoma.
Muta alisema Tibe sasa anachukua mapato yote ya shule hiyo na eneo ilipojengwa nalo amelibadilisha jina na kuweka la kwake.
Watu walio karibu na familia hiyo wameeleza kuwa chanzo cha mzozo wa umiliki wa shule hiyo baada ya Marehemu Mchungaji Rwakatare kufariki ni mmoja wa watoto wake kuwazunguka wenzake na kuhamisha fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya shule kwenda akaunti yake binafsi na pia akaanza kuchukua mapato yote ya shule hiyo.
Kwamba baada ya hilo kubainika, Tibe aliamua kuitwaa shule hiyo, akaibadilisha jina na majina ya akaunti za benki, hatua ambayo sasa inalalamikiwa na ndugu zake.
“Huyu ndugu yetu anashangaza sana kuanza kuandika barua kwa viongozi wa Serikali akitutuhumu kwa kukiuka sheria za nchi, eti tunaghushi nyaraka wakati yeye ndiyo bingwa wa kughushi nyaraka kuanzia Brela mpaka ardhi na anayemtumia kufanya hizo kazi za kughushi anafahamika, ni kijana aliyesoma kwenye moja ya shule zetu. Anachotaka amiliki yeye mali zote za mama.
“Ana madudu mengi mno lakini sie hatujishughulishi naye matokeo yake akiona tunamzuia kuchukua kila kitu anatafuta huruma nje ya familia kwa kutuchongea serikalini.
“Amejimilikisha shule ya Dodoma na kuibadili jina na akaunti za benki wakati shule hiyo ina mkopo wa benki moja kubwa nchini. Wewe unaweza kubadili umiliki wa mali ambayo ina mkopo wa benki kweli? Muulizeni na yeye hilo kalifanikishaje?
“Anamiliki mali nyingi sana za mama ambazo mapato yake yote yanaingia mfukoni mwake na hakuna anayemsumbua lakini yeye jambo dogo tu analalamika na kuandika barua huku na kule.
“Tulipouza hizo ardhi nyingine na kugawana mbona hakusema lolote? Kamuulizeni anataka nini hasa maana shule aliyotupora baada ya kuibadilisha jina imeondolewa kwenye orodha ya mali za marehemu mama. Hivi sasa anaimiliki yeye bila ridhaa ya sisi ndugu wengine.
“Nyumba za kupangisha za marehemu mama, zile ‘Appartments’ za Tabata zaidi ya 25, vyumba vya biashara 20, kote anachukua kodi yeye na pia mgodi wa dhahabu Chunya nao kachukua lakini bado anatupiga vita,” alisema Muta.
Alipoulizwa Tibe kuhusiana na madai hayo alisema hana muda wa kuyazungumzia.
Tanzania PANORAMA inaendelea kumtafuta Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kulizungumzia hilo.
Source: Tanzania-Panorama
Na wao Ni vile vile....sema Kama uko mbali nao huwezi jua kirahisi!Waarabu wanawezaje? Sijawai sikia mgogoro wa waarab
Maisha yetu ni miaka sabinI mimali yote hayo ya kazi gani?
Udiwani ni level ya chini sana kwa huo uwekezaji na ni cheo cha usumbufuUdiwani una faida kubwa sana. Maana mkurugenzi wa manispaa uliyopo anakuwa rafiki yako. Uwekezaji wako unakuwa hausumbuliwi sumbuliwi na watu wa serikalini. Na pia kwenye ma viwanja yakigaiwa wewe unapewa tu kwa urahisi
Mkuu tatizo la waafrika kuwa na hu ujinga ni ile biashara ya undugu, yaani hata ukaandikiqhe kisheria bado ukifa mahakama inafuata ulichoandika but watoto wanapewa nafasi.Utajiri wa familia za kiafrika haudumu kwa generation zaidi ya 1. Na hapa ndipo wazungu, wahindi na Waarabu wanaptupiga gepu
Kila mara utasikia migogoro ya kugombea mali za tajiri mweusi mara Mengi, mara bilionea Msuya, Lwakatare, kuna yule Mrema wa Ngurdoto n.k
Ila ni mara chache sana kusikia tifu kama hizi kwa matajiri wa ki Asia au kizungu.
Wazungu na wahindi utajiri wao ni wa kurithishana vizazi na vizazi.
Ila kwa mswahili utajiri wa baba unasamabaratika akishjakufa, watoto na wajukuu wanaanza upya,
Hii sio kwa Tanzania tu, hata Kenya inatokea sana, hata Marekani kwa watu weusi ambao wana exposure kubwa tu, utajiri haudumu
Usije kushangaa siku Dangote anafariki, ndugu wakagawana mbao hivihivi
kwa mtindo huu hatutakaa tuwafikie hata tupewe karne 100
Anaitwa SHAABAN ALLY MHOJA .... unaweza kumuita TX MOSHINimekumbuka ule wimbo, Mali ya baba inanitoa roho, bora nikae pembeni
Atauza mpka kanisa la mlina wa [emoji91][emoji91]Hivi kweli mali zote hizo za mama bado unagombea udiwani kuna shida sio bure.
Mali zote Muta anagombea Udiwani,shangaa Mali zote na bado alikua ni tapeli wa kiwango cha kimataifa kabla hata Mama Rwakatale hajafariki
Kwenye udiwani ndio anakopigia viwanja
Udiwani ni level ya chini sana kwa huo uwekezaji na ni cheo cha usumbufu
Tatizo ni umasikini ndio unaosumbua, sijui mzungu alipitia njia zipi mpaka akawa mstaarabu kama alivyo sasa,Wazungu, mtoto anakuwa na maisha yake pasipo tegemea mali ya mzazi. Ikitokea mzazi amefariki, mtoto au watoto uwa hawana kielehele na mali ya mzazi wao. Wanachoangalia mzazi aliacha wasia gani? Wanafuata wasia, na si waafrica ambao wakati mwingine wosia uwekwa pembeni na kuanza mapambano na ugomvi wa mali. Wazungu wanaheshimu wosia wa marehemu. Hata marehemu akiwa kaandika mali yake apewe mbwa au paka, hakuna atakaye enda mahakamani kupinga. Wanasema ni uamuzi wa marehemu, kwakua mali ni yake.
Wazungu wao ugawa mali zao kwa mashirika ya misaada, makanisa hata kwa serikali. Na watoto upata potion yao na hakuna anae mdhurumu mwenzie. Hata kama marehemu hakuacha wosia watoto ugawa mali kwa haki sawa. Ona sasa hawa hivi awawezi kuendeleza kwa pamoja mali alizowaachia mama yao, mfano hayo mashule, kuna haja gani kuanza gawana na kubadili majina. Kuuza viwanja badala ya kuendeleza maono ya mama yao. Hizi tamaa ndo maana watoto siku hizi wanauwa wazazi wao kwa tamaa za mali.
Wahindi, na waarabu hata wao wanaheshimu sana mali ya marehemu, kama marehemu alikuwa na maono fulani, basi uyaendeleza maono yale. Hivyo kama marehemu alikuwa na biashara wataendeleza ile biashara kifamilia, itazidi kukuwa, mali itamilikiwa na kuendeshwa kama marehemu alivyofanya. Bado itabaki mikononi mwa familia. Ndiyo maana biashara ya wahindi inadumu kizazi hata kizazi.
Sisi weusi ni kuvuruga. Mzazi anakufa siku hiyo hiyo unaona watu wanaanza kujitenga na kujiami. Wanaanza kununiana. Mara vikao vya siri.
Kuna kuwa na makundi hata hawa watu ni ndugu tumbo moja, ubinafsi, chuki, majigambo yanaanza. Hapo ni vita na kukosana ndugu kwa ndugu. Jamani weusi wenzangu, tutafute maisha na kujitegemea binafsi. Hizi mali za wazazi ukiendekeza uleta mafarakano tu katika maisha. Pia tuzingatie kuandika wosia, japo bado hata huu wosia umekuwa unaleta mafarakano.
Eeeh, Mungu sisi ngozi nyeusi tunamatatizo gani? Tupe mwanga tuondokane na tamaa pia na ubinafsi.
Huyu Tibe ndio 'amedata'? maana mmoja nasikia kadata kwa mapodaaaaaa!
Ewaaaaa sahihi kabisaAnaitwa SHAABAN ALLY MHOJA .... unaweza kumuita TX MOSHI
sie black wapi tunakosea kwa kweli waarabu usingesikia hizo mambo hapo wakileta tamaa pesa ya laana itaisha yoe wangetulia hofu noana hao wana baba zao tofautiWanajipanga.Mzazi wala haandiki hata hisia
Ingekuwa waarabu watoto wote wangekaa kikao pamoja kujipanga namna ya kuendesha hizo mali.Wangechaguana mmoja awe mkurugenzi mtendaji ,mwingine wa utawala,mwingine wa fedha nk na kuziendesha hizo mali pamoja wakawa wanalipana mishahara kila mwezi na wanagawana faida mwisho wa mwaka
Lakini mitoto ya kiswahili pasua kichwa yaani mali zote zile zinasambaratika kwa muda mfupi .Muda si mrefu hao watoto wa Lwakatare watakuwa maskini wa kutupwa
Baba Yao mmoja mama Rwakatare hakuchakachua ila alizaa mitoto mjinga inayofanana kiakili na ujinga wa upande wa Baba Yao sio upande wakesie black wapi tunakosea kwa kweli waarabu usingesikia hizo mambo hapo wakileta tamaa pesa ya laana itaisha yoe wangetulia hofu noana hao wana baba zao tofauti