Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kwa mara ya kwanza katika historia CCM itaelekea katika uchaguzi wa urais mwaka 2030 bila kuwa na mgombea yeyote maarufu, mwenye ushawawishi au anayeweza kubebwa au kujificha chini ya kanuni za utamaduni wa chama wa "muendelezo" wa Rais aliye madarakani.
Hii inaweza kuwa fursa kubwa sana ya mabadiliko ya siasa Tanzania kwa sababu watu watapasuana sana humo ndani na wanaweza hata kugawana mbao hasa tukizingatia hakuna tena wazee wazito wa busara na wenye kauli ndani ya chama kama ilivyokuwa Nyerere na Mkapa.