Vita ya kuwania madaraka ya urais 2030 ndani ya CCM inaweza kuleta anguko lake

Ccm ni chama imara .hakiwezi kuteteleka kwa mambo madogo kama hayo.halafu ccm hawampendi mtu bali wanapenda chama Chao.kuna siku ulifikiri kwamba lowasa angekatwa ccm?
 
Kwa mara ya kwanza katika historia CCM itaelekea katika uchaguzi wa urais mwaka 2030
DAB atawamaliza wengi wanaotaka kukaa kwenye hicho kiti, DAB alitaka kua Mbunge akishakua Mbunge awe Waziri baada ya kua Waziri anataka kua rais, na yupo tayari kumfyeka yoyote atakaetaka kumzuia kufika hapo, suluhisho ni kumuwahi kabla maana atawamaliza wengi ili yeye akae juu, subiri uone
 
Hii dunia inachekesha sana
Watu wanapigania urais sio kwasababu ya maslahi ya wananchi bali kwa maslahi yao wenyewe.
Alafu eti uzalendo uzalendo?
Which where ?
... Utakuta jitu limepewa moja ya ofisi zetu nyeti kabisa na kila bajeti linashika mgao lakini , badala ya kututumikia kwa bidii na maarifa, liko bize kuunda kamtandao ka kupenya Ikulu SASA HIVI 2026 HII!
WAO WAANZE ILI SISI TUMALIZE!
 
2030 hatutakua na Aibu, Jungle doesn't care about your feelings,
 
Mbuyu wenye misukule mitata na wenye utata kuangusha ilikuwa Emma tu. Sasa iliyobaki kama huu wa BioGenerator ni ya shoka moja moja tu chali.

Kete zinasukumwa kwa ustadi mkubwa sana. Mwanaume mwenye kidoti usoni anaenda kuwa PM na mgombea wetu 2030.
Kama hilo ni kweli basi TUMEKWISHA!
MAANA OCT29 2025 ILIKUWA CHA MTOTO!
 
Kwa Sasa ndani ya mboga mboga hamna mgalatia anaeaminika kupewa kiti.
 
... huyo dogo akubali tu kuwa Kawawa wa kizazi kipya! 😅
 
Chungu lakini ni dawa, tuinywe tu.
Samia akitoboa hadi 2030 amini nawaambia hatatoka madarakani, tutakuwa nae hadi 2035.
Hatakubali kutoka!
 
Kwahiyo unataka isianguke? We mpuuzi Nini? Acha wauane. Piga kimya.
 
Kuna wale wanaosukuma kete ya Makonda huwa nacheka sana heti makonda heti hawe Rais 🤣
Kwani kuna tofauti gani kati ya Makonda na huyu wa sasa?
Nchi yetu ilipofikia mtu yoyote anaweza kua Rais as long as utalinda maslahi ya lile genge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…