Maasi ya Jeshi ya 1964 hayatambuliki kama jaribio la mapinduzi. Maasi hayo yalitokana na mwendelezo wa Afrikanization ambapo Wazawa hawakupenda vyeo vya juu jeshini kushikiliwa na Wazungu. Kambona alijitahidi kuzungumza na waasi wakati Mwalimu na Kawawa wakiwa mafichoni.
Jaribio la Mapinduzi ambalo Kambona alihusishwa ni la 1969 akituhumiwa kushirikiana na Bibi Titi na wengine. Tofauti baina ya Nyerere na Kambona ilitokana na namna ya kuendesha siasa ya ujamaa. Inasemekana Kambona alitaka Ujamaa uendeshwe kidogo kidogo kwa majaribio wakati Nyerere alitaka jumla jumla.
Excellent. Hii ndio habari yenyewe. Kambona na viongozi kadhaa ndani ya TANU walistushwa na muelekeo wa kikomunisti wa Nyerere kuanzia kufuta vyama vingi, kutangaza siasa ya ujamaa isiyo wazi, utaifishaji wa mali za “mabepari” na “makabaila” bila fidia, uanzishaji wa vijiji vya ujamaa kwa nguvu, n.k.
Kwa kifupi, Nyerere alikuwa akitekeleza ajenda yake ya “ujamaa” kidikteta bila kuhusisha taasisi za mashauriano na uwakilishi ndani ya chama na serikalini.
Ulikuwa ni mgogoro wa kiitikadi dhahiri kati ya Nyerere aliyekuwa akiidhibiti dola na Kambona aliyeishia kuwa muasi.
Mpambano wa Magufuli na Lissu si wa kiitikadi na hauelezeki kimantiki katika mazingira ya kisiasa. Unaweza kutizamwa zaidi kama harakati za kuleta demokrasia (ambayo haijawahi kuwepo) Tanzania. Ni muendelezo wa maumivu ya taratibu ambayo taifa linayashuhudia tangu 1992 ilipotangazwa rasmi kuwa Tanzania imechagua kuwa demokrasia ya vyama vingi.
Magufuli ameonyesha kuwa kiongozi mkali zaidi ya wote aliyeamua kivitendo “kutoendekeza” wale wote walioamua kwa dhati kuendesha upinzani uliodhamiria kuiondoa au kuhatarisha nafasi ya CCM kuwa madarakani.
Lissu ndiye mwanasiasa na mgombea urais wa upinzani aliyeonyesha ujasiri na ujeuri wa kipekee wa kukabiliana na tishio la Magufuli.
Kwa bahati mbaya, Watanzania wengi hawana uelewa wa mapambano ya aina hii - kwamba yanahusu mustakabali wa maisha yao kama Wanachukulia kama ushabiki wa klabu za mpira. Na wengi pia hawana “interest” na haya mambo ya siasa siasa.