kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Waafrika tuamke wenzetu asia amerika latino wanaelewa nini kinaendelea.
Ukiangalia vita vya ukraine ni kwamba hapo pamekua tu uwanja wa mapambano. Ni kati ya nchi za kibeberu za marekani na ulaya ya magharibi wakiongozwa na marekani wakipigania hati miliki kudhibiti uchumi wa dunia.
Utaona hata zile nchi wajomba wa nchi za magharibi kama australia na new zealand na japan japo hazipo ulaya wala amerika wapo kwenye ugomvi upande wa nato dhidi ya Urusi.
Nato lengo lao kuidhibiti urusi kijeshi ili kuigeuza shamba la bibi. Urusi siku zote hofu yao ni lengo la ulaya ya magharibi. Hawataki kuiona Urusi kama nchi yenye uwezo mkubwa kiteknolojia huru kutoka nchi za magharibi.
Hawataki kuona ustaarabu mbadala wa kijamii na kiteknoloji tofauti na ule wa magharibi. Walijitahidi kuidhibiti china ikawashinda.
Hili la urusi kutaka kulipwa kwa ruble ni mojawapo ya mambo yanazidisha chuki ya marekani kwa urusi. Wao wanataka hela yao dola iendelee kua hela ya biashara duniani hasa kwa mafuta. Pia hela yao ndio ibakie hela ya kuweka akiba kwa nchi zote tena kwenye benki zao.
Tatizo kubwa linatokea pale ukikorofishana na marekani anakupora akiba yako ya fedha kwenye bank zao. Huu ni ukoloni mpya na udhalimu.
Kinachoendelea sasa ni nchi mbalimbaki kuanzisha namna ya kufanya biashara ya kimataifa kwa kutumia fedha tofauti na kuweka akiba zao kwenye fedha tofauti na dola ya Kimarekani.