Vita ya Ukraine; Waafrika tuamke, ni ubeberu wa Magharibi dhidi ya walimwengu

Vita ya Ukraine; Waafrika tuamke, ni ubeberu wa Magharibi dhidi ya walimwengu

Libya,iraq,Syria wamechukuliwa ardhi zao?
Crimea wamechukua kinguvu na Sasa hivi wanataka wachukue donbas kinguvu.
Nakwambia kila mtu akitaka achukue ardhi ya mwenzake hapatakalika ni sawa sawa Tanzania achukue burundi,Rwanda na malawi
haelew huyo mkuu
 
Baada ya miezi miwili urudi hapa , Urusi amejichanganya mwenyewe
Sawa mkuu, Ila Biden alisema anataka Ruble iwe rubble...naona hadi saivi hajafanikiwa. Inachukua nguvu nyingi sana kuangusha mataifa makubwa, na hadi taifa kubwa lianguke ni lazima kuna athari kubwa kwa mataifa mengine mengi tu.

Usiyachukulie mataifa makubwa for granted.
 
ebu jikite kweny uhalisia na sio hoja za kufikirika , nan kamvamia mwenzie ?
Nimekupa maswali badala ya kunijibu unataka nijikite kwenye uhalisia, upi?
Root cause ni nini hasa?
 
Kwanini Russia asisambaratishe nato kama Soviet Union ilivyosababishwa kuvunjika?
Umoja wa kujihami wa urusi na nchi za kikomunisti ukiitwa warsaw pact walijifuta kwa maelewano nato nayo ijifute. Kama kawaida ya nchi za kibepari ikawa wamewalaghai warsaw pact. Nato ikabakia kwa lengo la kuidhibiti urusi kwamba idhoofike kabisa kijeshi na kiuchumi idhibitiwe na nchi za kibepari. Putin alivyoingia urusi ikaendelea na kuimarika kiuchumi na kijesji tofauti na malengo ya nato kuidhibiti.
 
Umoja wa kujihami wa urusi na nchi za kikomunisti ukiitwa warsaw pact walijifuta kwa maelewano nato nayo ijifute. Kama kawaida ya nchi za kibepari ikawa wamewalaghai warsaw pact. Nato ikabakia kwa lengo la kuidhibiti urusi kwamba idhoofike kabisa kijeshi na kiuchumi idhibitiwe na nchi za kibepari. Putin alivyoingia urusi ikaendelea na kuimarika kiuchumi na kijesji tofauti na malengo ya nato kuidhibiti.
sijajua kuna uhusiano gan na uvamiz wa ukraine ! kwa hoja yako nlitegemea Urusi awavamie mabeberu na sio Ukraine
 
Nimekupa maswali badala ya kunijibu unataka nijikite kwenye uhalisia, upi?
Root cause ni nini hasa?
weka hoja zinazoonekana na sio hoja za kufikirika , hii ni vita kamili sio cold war so humu tunahitaji reality sio simuliz za abunuas
 
Ujue nato ilianzishwa baada ya vita vya pili vya dunia kwa lengo la kuidhibiti urusi kijeshi. Urusi baada ya kusambaratika soviet union imekua inapinga waliyokua washirika wake kwenye warsaw pact kuingia nato. Hii ni kutokana na hofu ya urusi nato kukaribiana mipaka na nchi yao. Kumekuepo makubaliano na nato kwamba nchi iliyokua ndani ya soviet union kama ukraine isiingie nato lakini nato wamekua hawaheshimu wala kujali matakwa ya kiusalama ya urusi. Nchi za nato zimejiingiza ukraine kiasi cha urusi kutishika kwa usalama wake ndio sababu ya mgogoro hadi kuivamia nchi hiyo.
wanatuma maombi wao wenyewe kujiunga na NATO na sio NATO inatuma maombi kwao , sababu kubwa ni Uonevu wa Urusi dhidi ya majirani zake , nchi za NATO haziingiliani kisiasa , cha zaid wanahakikisha misingi ya demokrasia inalindwa kwa kila mshirika wa NATO
 
Kama tuna taka maendeo west natufaa ila kama tuna taka umaskin basi tumfate Russia.
 
Urusi ni nchi inayomiliki eneo kubwa sana katika Dunia hii kuliko nchi nyingine yoyote. Himaya ya Urusi imeenea hadi kwenye eneo la ardhi iliyoko katika ncha ya kaskazini ya Dunia hii.

Maliasili iliyoko kwenye eneo lote linalomilikiwa na Urusi ni mali ya warusi na hili haliwafurahishi mabeberu wa Magharibi.

Ili kupora mali za Urusi ni kuuvunja muungano wa kisovoeti kwanza na mkakati huo ulishaanza kutekelezwa tangu mwaka 1989. Poland ndio nchi kibaraka inayotumika kuisambaratisha Urusi, Tatizo ni kuwa Poland iliishajiunga na NATO kitambo, hivyo haiwezi kuichokonoa Urusi moja kwa moja maana NATO itahusika, ndio maana nchi za Magharibi zimetafuta nchi nyingine kibaraka (Ukraine) itumike kuleta chokochoko itakakayofanikisha lengo lao.
Bro kama nchi tume ushi kwenye mifumo yote miwili .usinambie tuludi kwenye kupanga foreni ya kununua sukali . Na nchi kuwa chini ya kikundi Cha watu wachache ndo hivo inavyo taka?
 
Wewe nae kibaraka wa wamagharibi tu, hivi unadhani ulaya magharibi na marekani zinafurahi urusi kutegemewa kwa kiasi kikubwa kwenye nishati ya gesi na mafuta? US anataka kuitawala dunia, ameshafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno, ndio maana ulaya magharibi yote(umoja wa ulaya) wanakubaliana na kila marekani anachotaka, Japan, Korea ya kusini, Australia, Canada...zote hizi hazimpingi mmarekani kwa lolote.

Urusi ana resources za kutosha sana, vikwazo alivyopigwa ingekuwa nchi yoyote, na hasa ingekuwa nchi ya kiafrika hadi leo hii uchumi ungekuwa umeanguka mazima, mkate ungeuzwa hata 200,000, lakini utegemezi was ulaya kwa urusi ndicho mmarekani hakipendi.
Sasa Kwa miaka yote tulio tumia ujamaa umetufikisha wap kama nchi ona wenzetu Kenya ,ona south Korea ona singapole ona nchi za ulaya magharibi haya fananisha na nchi za ulaya mashariki zile zilokuwa chini ya Urussi, haya angalia china Kwa ndani miaka 30 walivyo Fanya maajabu Kwa kutumia mfumo wa kibepari .shame on you bro unadhani tupo miaka 1970s saiv.
 
you guys hizi porojo hazisaidii kitu, dunia ilishahama uko kwenye hizo dhama za kuporana kwa nguvu rasimali.
wenzenu wanapiga hatua kwa kuwekeza kwenye tafiti na kuuza technolojia nyie mmejaliwa kupiga domo tu et wanaiba rasimali!!.
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana 🚮🚮🚮
 
Waafrika tuamke wenzetu asia amerika latino wanaelewa nini kinaendelea.

Ukiangalia vita vya ukraine ni kwamba hapo pamekua tu uwanja wa mapambano. Ni kati ya nchi za kibeberu za marekani na ulaya ya magharibi wakiongozwa na marekani wakipigania hati miliki kudhibiti uchumi wa dunia.

Utaona hata zile nchi wajomba wa nchi za magharibi kama australia na new zealand na japan japo hazipo ulaya wala amerika wapo kwenye ugomvi upande wa nato dhidi ya Urusi.

Nato lengo lao kuidhibiti urusi kijeshi ili kuigeuza shamba la bibi. Urusi siku zote hofu yao ni lengo la ulaya ya magharibi. Hawataki kuiona Urusi kama nchi yenye uwezo mkubwa kiteknolojia huru kutoka nchi za magharibi.

Hawataki kuona ustaarabu mbadala wa kijamii na kiteknoloji tofauti na ule wa magharibi. Walijitahidi kuidhibiti china ikawashinda.

Hili la urusi kutaka kulipwa kwa ruble ni mojawapo ya mambo yanazidisha chuki ya marekani kwa urusi. Wao wanataka hela yao dola iendelee kua hela ya biashara duniani hasa kwa mafuta. Pia hela yao ndio ibakie hela ya kuweka akiba kwa nchi zote tena kwenye benki zao.

Tatizo kubwa linatokea pale ukikorofishana na marekani anakupora akiba yako ya fedha kwenye bank zao. Huu ni ukoloni mpya na udhalimu.

Kinachoendelea sasa ni nchi mbalimbaki kuanzisha namna ya kufanya biashara ya kimataifa kwa kutumia fedha tofauti na kuweka akiba zao kwenye fedha tofauti na dola ya Kimarekani.
Utakataaje mabeberu wakati huna kitu,wanakupa misaada mpaka ya chandarua,condom,huyo Russia anakupa nini
 
Back
Top Bottom