Vita ya Ukraine; Waafrika tuamke, ni ubeberu wa Magharibi dhidi ya walimwengu

Ok nimekuelewa mentality yako. Naona kama vile mzungu wa unga. Ukivaa kidani cha dhahabu shingoni na pete vidole kote.. unajiona inatosha umeukata mwenyewe umaskini 😂😂. Kama nakosea sorry bro🙏
 
'Kwenda zako' mbona poa tu mkuu? Naona unaovereact.
 
unataka kusema kwamba wingi wa resources zake ndiyo chanzo cha kuwekewa vikwazo? hii sababu na Putin anaijua ama ni wewe tu? kwa hiyo sababu ya kuivamia Ukraine ni pumbao tu ila sababu kuu ni resources?.

Yeye Putin anasema Ukraine ni kitisho cha Urusi, wewe unasema resources za Urusi ndiyo chanzo cha kitisho cha chake. sasa ninaomba unishauri, nikuamini wewe ama Putin?.
na zaidi kuhusu kuporomoka kwa uchumi wa Urusi ni jambo linalohitaji muda. Zimbabwe haiku fika hapo for a month it took a many years na si sahihi kudhani Urusi itashuka hadi kufika Levo ya Zimbabwe.
 
Kwanini pasikalike ilivamiwa IRAQ SYRIA LIBYA VIETNAM JAPAN nabado pakakalika vyema tuu
UKRAINE anatakiwa apelekewe moto mpaka aelewe yakwamba yeye ni nani na RUSSIA ninani
 
Sio nchi za AFRIKA
VIKWAZO alivyogongwa RUSSIA kama lingepigwa taifa lolote jengine hapo ULAYA jengine lolote hapo ULAYA now days wangekua wanataftana tena chini ya mwezi mmoja
RUSSIA kama kaweza kutoboa sasa basi ndio imekula kwao
Njia pekee ambayo ni nyepesi lakini gharama zake kubwa zakuiangusha RUSSIA nikuingia vitani na MOSCOW moja kwamoja
Sasa shida inakuja nani atamgunga paka kengeleeee !!!??
 
Huenda hujaelewa hoja yangu mkuu.

*Kwanza tujue kwa nini Russia amefanya operation ya kijeshi?

*Nani amekuwa akichochea hizi nchi hadi kuingia katika hali hiyo?

*Sababu/maslahi ya huyo mchochezi ni nini?

*Aftermath ya mgogoro huu, nani anafaidika na nani anapoteza?
 
Kwanini pasikalike ilivamiwa IRAQ SYRIA LIBYA VIETNAM JAPAN nabado pakakalika vyema tuu
UKRAINE anatakiwa apelekewe moto mpaka aelewe yakwamba yeye ni nani na RUSSIA ninani
Libya,iraq,Syria wamechukuliwa ardhi zao?
Crimea wamechukua kinguvu na Sasa hivi wanataka wachukue donbas kinguvu.
Nakwambia kila mtu akitaka achukue ardhi ya mwenzake hapatakalika ni sawa sawa Tanzania achukue burundi,Rwanda na malawi
 
.
hayo yameshajadiliwa sana hapa shida kuna upande wanaona Urusi ni an angels nation hawawezi fanya makosa na hata wakikosea majibu ni mbona US alifanya hivi na vile.

Turudi tulipoishia, ni nani kati yako na Putin anatoa sababu za kweli?.
nimekutaka unichagulie wa kumuamini, nikuamini wewe ama Putin?.
 
Unanionea
Mkuu sijui nakuonea kwenye lipi mimi sio moderator ....Lakini ukweli ndio huo ulioandikwa.
Hizi siasa za kimataifa zinakutaka uwe mdadisi na kufuatilia mienendo ya wanasiasa na matajiri wa ulimwengu ili wasikushangaze.

Ukitaka kuuelewa vizuri mgogoro huu, anza na historia ya kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya Dunia, kuundwa kwa muungano wa kisovoeti, kuundwa kwa NATO na mwisho kuanguka kwa muungano huo wa kisovoeti na hasa hatua ya kuuvunja ukuta wa Berlin....

Fanya hiyo homework at leisure bila kuchagua upande utajifunza mengi..... Kila la kheri mkuu !.
 
Mkuu; Ukraine ilivamiwa na Urusi ss iweje Ukraine ilileta chokochoko?
 
Kinachoendelea sasa ni nchi mbalimbaki kuanzisha namna ya kufanya biashara ya kimataifa kwa kutumia fedha tofauti na kuweka akiba zao kwenye fedha tofauti na dola ya Kimarekani.
Marekani ina financial markets kubwa na zenye nguvu duniani, ukizingatia na uchumi mkubwa ilionao. Pia, ndiyo nchi inayoongoza kwa kununua bidhaa duniani ambapo inapelekea biashara nyingi kufanyika kwa dola kuliko sarafu nyingine yeyote duniani.

Kwa sababu hizo kadhaa, dola itaendelea kuwa reserve currency kubwa duniani.

Nchi haziwezi tu kuanzisha utaratibu mwingine ghafla. Nchi zinahitaji kufanya biashara kimataifa kwa urahisi na ufanisi zaidi. Hivyo, zinahitaji kutumia sarafu yenye nguvu zaidi (dominant) katika soko kwaajili ya manunuzi ya nje, ambayo kwa sasa ni dola ya Kimarekani.
 
Mbunge wa bunge la Germany mwenyewe na wabunge wenzake wanajua khs uchokozi wa USA,Cha ajabu Wamarekani wa ukerewe humu JF wanabisha bisha ujinga.
 
Libya,iraq,Syria wamechukuliwa ardhi zao?
Crimea wamechukua kinguvu na Sasa hivi wanataka wachukue donbas kinguvu.
Nakwambia kila mtu akitaka achukue ardhi ya mwenzake hapatakalika ni sawa sawa Tanzania achukue burundi,Rwanda na malawi
SYRIA kuna upande kule kama sijakosea wanasema kwenye milima ifrati cjui
Kule US wameigawa nchi wanajibebea tu wese la watu
Usione kubeba sehem ya nchi nijambo jepesi lazma kwanza uwe na nguvu yakijeshi na kiuchumi usiache na nguvu za kiintelijensia nk ili uweze kuzimanage hizo sehem baada yakuzikwapua
Nandio maana ukaona baada ya CRIMEA kuondoka kumekua kama hakujatokea jambo maisha yanaenda
Kuhusiana na UKRAINE hawa jamaa watake au wasitake wapende au wasipende lazima ukanda wa mashariki huko kwa DON BASS ODESSA nk iwe jua ama mvua kwa amani ama kwadamu kumwagika kama unavyona sasa lazima ile sehemu RUSSIA atapita nayo yaani lazima nisuala la muda tuuu
Pia hata ARGENTINA ilibebewa eneo lao na waingereza la fallkland namaisha yakaendelea
Haya mambo sio mazuri ila hayatakaa yaishe tuwe wapole tu kwakweli
RUSSIA sio ZIMBABWE
 
Mkuu; Ukraine ilivamiwa na Urusi ss iweje Ukraine ilileta chokochoko?
Kuvamiwa kwa Ukraine kunatokana na mipango ya siri inayoendeshwa na watu wachache kwenye Serikali ya Ukraine, wanaoshabikia nchi za magharibi na kuachana kabisa na unasaba wa asili na Urusi. Kimsingi ni ndugu wawili wa damu wanaogombanishwa na nchi za magharibi.
Hii mipango ya siri tunaweza kuifananisha na ile iliyofanywa na Poland hadi kujiunga na EU na NATO. Kama ukifuatilia mwenendo wa Ukraine utaona kuwa wanafuata nyayo zile zile za Poland, isipokuwa Ukraine wanawaua sana raia wabishi wanaozungumza kirusi huko Donbas na Rugantsk kimya kimya.
 

Hakuna kitu. kasomea Allegory in the cave then utakuja nishukru.
 
Oh! Umenitoa ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…