Vita yetu dhidi ya ushoga ni dhaifu sana

Vita yetu dhidi ya ushoga ni dhaifu sana

Hachana na Afrika tuizungumzie Tanzanania yetu....Unaijuishaje Tanzania inayojikongoja na mataifa mengine yaliyokwisha kupiga hatua?.
Mataifa yapi ya Africa yaliyopiga hatua, yanaweza kutunisha msuli kwa Europe??
 
Naungana na wewe kiongozi kwani mtu wa kwanza kulisimamia hili ni mzazi au mlezi katika familia ni ngumu sana kwa serikali kuingia mpaka kwenye malezi yetu
 
Huku kupinga ushoga watu hufanya kimazoea tu ila sio kwamba wako serious, ndio maana unaona hauoni nguvu kupinga umalaya tena unatangazwa hadi mitandaoni waziwazi na hao mashoga unakuta hadi harusi na shughuli zengine wanaalikwa, kuna mashoga maarufu kabisa wanajulikana. Sasa hii pinga pinga ya ushoga nashindwa kuelewa wanachokipinga wao hasa ni kipi?
Wapi hao unao wajua wee?? Ushahidi unao??
 
Ngoma ishapitishwa sema na marekani washaibuka tena kuipiga biti Uganda,Nashangaa Marais wa Afrika mashariki wapo kimya,Tulipoteza chuma chetu kingeshatoa Tamko.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unachekeshaaa wee sanaaa. Lol
 
Kinachotokea wanatumia ile kitu inaitwa "divide and rule" kwa kutumia mikopo na misaada yao. Kwanjia hii ya divide and rule wanafanya yafuatayo kulingana na ukubwa wa maslahi wanayoyakusudia kuyapata kwenye bara au nchi husika.

1. nchi inayokubali inapewa misaada ya kifedha na mikopo na nchi inayokataa inanyimwa
2. Jirani yako anaekubali anapewa silaha kubwa na mafunzo ya kijeshi na wewe unaekataa hupewi silaha hizo, hivyo uko hatarini kupigwa na jirani yako.
3. nchi inayokubali inatembelewa na viongozi wakuu na watalii kutoka magharibi wakati nchi inayokataa haitembelewi na watalii hawaendi. Kama vile mtoto mtundu anavyonyimwa kupewa pipi.
4. Nchi inayokubali viongozi wake wanaruhusiwa kukwea pipa na kutembelea nchi za magharibu, wakati iliyokataa viongozi wake wanapigwa marufuku. hapa wanajua kuwa waafrika wanapenda sana kwenda nchi hizo kuficha hela, kufanya manunuzi au kufanya matanuzi.
5. nchi inayokubali inasamehewa madeni yake wakati ile inayokataa deni linabaki palepale na kutakiwa ilipe haraka vinginevyo......
6. Inayokataa inawekewa vikwazo vya kiuchumi wakati inayokubali hilo jambo inapewa fursa mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kielimu.
7. na mwisho kiongozi anayekataa wanaweza kumpindua, kushindwa kwenye uchaguzi na hata kuuawa.

Hakuna kiongozi wa Afrika anayetaka kimojawapo kati ya hivyo hapo juu kimtokee yeye, na kama yuko basi ni mmoja au ameshapinduliwa, shindwa uchaguzi au kufa tayari.
Sasa haya yote mnayajua, hizi kelele za nn??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huwezi kupambana na ushoga kama sera zako nizakutegemea misaada na kutegemea mikopo ya beberu.

Ukiwa na mentality ya kujitegemea bila kuwaza kuombaomba misaada lazima uwe na nguvu na misimamo kwenye mambo kama haya.
 
KUNA NJIA MBILI ZA KUPAMBANA NA TATIZO, MOJA KUPAMBANA NALO KIMYA KIMYA NA KULIMALIZA KIMYA KIMYA, PILI, NJIA YA KUPIGA KELELE KUSHINDANA NA TATIZO, TANZANIA IMEAMUA KUSHINDANA NA SHETANI KIMYA KIMYA, HATUTUMII NJIA ZA WENGINE KUPIGA MAKELELE
Sawa, unamaanisha mashoga wote wataonekana kama vile wamejinyonga wenyewe?
 
Kama tunashindwa kujitoshereza kwa chakula na rasilimali zote muhimu tunazo,tutaweza kweli kupambana na wazungu kuhusu ushoga,wakati tunahitaji dollar zao?
Nigeria ina mafuta,lakini wananchi wake wanapanga foleni kununua Tena kwa bei juu.
Congo Kuna msdini,lakini kampuni zote zinazochimba,zinatoka ulaya,
Bongo Kuna ardhi na maji kibao,lakini tunasubili msaada wa ngano kutoka Ukraine,nchi iliyopo vitani!hatuna pesa ya kuwekeza kwenye kilimo,lakini tuna bilioni 500+kila mwaka kununua ndinga mpya za watumishi serikali kuu,
Kipindi Cha Kikwete na Lowasa,Kanda ya ziwa kulikuwa na shida ya huduma ya maji,na ziwa Victoria lipo!yakafanyika maamuzi magumu,miundombinu ikawekwa Ili maji yatumike,kagera,mwanza,na sasa hv inabidi yafike singida mpaka Dodoma,
Tunahitaji maamuzi ya kuthubutu kama haya,bila hivyo vijana waachwe wabomolewe tu
Kilimo kwetu ni ndoto ya mchana, serikali haithamini kilimo Cha kibiashara, hata Yale mashamba makubwa aliyoyaacha mkoloni na Nyerere yanageuzwa makazi na kupewa wananchi walime kwa mkono kwa kutegemea mvua inyeshe. Halmashauri ziko bize kupima viwanja lakini haipimi ardhi ya kilimo na ufugaji, watu wanajijengea holela TU. Mkuu wa wilaya Hana uhakika ni wapi watu wataluma kwa miaka 100 ijayo na wapi ni makazi kwa miaka 100 inayokuja.

Msingi mkuu wa maamuzi yetu ni kuangalia uchaguzi ujao tutapataje kura za kusalia madarakani. Rais Magufuli aliweza kufanya baadhi ya maamuzi magumu tuliyoyaona kwakuwa alikuwa hatagemei kura kubaki madarakani. Hata hivyo hata yeye alishindwa kuwaondoa machinga mtaani kwa sababu ya kura ya 2015 iliyomuingiza madarakani. Tanzania tutapiga hatua kama tutaamini kwenye kushindwa na kushinda kihalali, hii itasaidia kuwaweka mbali mabepari na maadui wetu wanaotumia chaguzi zetu kutuibia,
 
Sawa, unamaanisha mashoga wote wataonekana kama vile wamejinyonga wenyewe?
Tunapambana nao kimya kimya, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu juu ubaya wa tabia hizi na athari zake, hivyo wanafundishwa kwanza kujitambua, this sometimes could be psychological problem, wanawekwa pahala panapofanania na sober house!
 
Wazungu wanao msemo wao maarufu usemao "nionyeshe rafiki zako ili nikwambie tabia yako", wakimaanisha kuwa kama ukiwa na marafiki shoga na wewe upo uwezekano mkubwa ni shoga vilevile au huuchukii ushoga hata kama wewe sio shoga.

Baba yangu alikuwa sheikh mkubwa lakini alikuwa na marafiki zake wengi ambao ni wachungaji, mapadre na wakristo ambao walikuwa wanamtembelea hadi nyumbani na wakati mwingine alikuwa anawaomba fedha za kujengea au kumalizia kujenga misikiti mbalimbali.

Tabia hii ya baba ilisababisha baadhi ya watoto wake kuolewa na kuoa wakristo bila kipingamizi kutoka kwa baba, yaani hakuona kama haiwezekani kabisakabisa mtoto wake kubadili dini na kuwa mkristo.

Tanzania tunapokea misaada na mikopo mingi kutoka "nchi rafiki" zetu ambazo wanaamini ushoga ni haki ya msingi ya mtu, na tunajisikia vizuri sana kuwa na marafiki kama hao wanaotusaidia fedha za kukwamua maendeleo yetu.

Binafsi sioni kama tunao uwezo wa kuwaambia kwa dhati na kwa moyo wetu wote marafiki zetu hawa kuwa ushoga kwetu hapana kwa sauti kubwa na ya mamlaka kwa kumaanisha.

Kama una rafiki shoga lazima na wewe nyuma ya pazia na off-camera unakubaliana na tabia hiyo. Kama hutaki tabia ya mtu furani lazina ukae nae mbali yeye na hata vitu vyake, vinginevyo utakumbana na msemo ule wa baniani mbaya kiatu chake dawa.

Kama tumedhamiria kupambana na ushoga kwa dhati na kwavitendo LAZIMA tukatae marafiki mashoga au wanaoamini kwenye ushoga. Kwenye hili nchi zote zinazoona ushoga sio sawa hazina budi kuzigeuzia mgongo nchi za magharibi hata kama kwa kufanya hivyo tutakosa mengi sana, yaani ni ile wachumi wanayoiita "opportunity cost".

Yaani tuchague kati hasara na faida za ushoga vs hasara na faida za kukosa misaada kutoka nchi za mashoga. vinginevyo tusidanganyane kuwa kuna kiongozi wa siasa mwenye mahusiano na nchi za magharibi anaepinga ushoga.

Umaskini Mbaya, ushoga ni Mbaya sana, ila Umaskini zaidi, Maana huna msimamo wakati hujiwezi, ni watu wachache sana kama Mugabe dunia hii, au Museven, na kizazi cha aina hiyo ndo kinaishilia hivyo
 
Umaskini Mbaya, ushoga ni Mbaya sana, ila Umaskini zaidi, Maana huna msimamo wakati hujiwezi, ni watu wachache sana kama Mugabe dunia hii, au Museven, na kizazi cha aina hiyo ndo kinaishilia hivyo
Njia za kupambana na tatizo hili kwa tanzania tumeliweka kwenye kundi la waathirika wa kisaikolojia hivyo ni watu wenye kuhitaji tiba za namna fulani za kiakili kwa kipindi fulani. Hivyo upambanaji wetu ni wa kipekee we solve the problem, HILI NI UGONJWA WA KIAKILI.
"Hivyo kumpa shoga haki kwetu ni sawa na kumpa mwendawazimu haki " kitu ambacho siyo sahihi. Hawa ni wagonjwa wa kiakili kama wagonjwa wengine ispokuwa ugonjwa wao umeriakti ktk kutamani Jamii yake!
 
*Tulipanda Usiku, tunavuna Mchana.*ila MATUNDA HAYAFANANI na MBEGU ZETU tulizootesha USIKU.
Ushoga, ulawiti, usagaji

Tulipoamua sote kuwa wafanyakazi, wajasiriamali na watumishi (wanaume kwa wanawake) hatukutafakari vyema.

Tulipoamua kuingia mtaani na kujipotosha juu ya haki sawa bila kujua undani halisi wa haki, fursa na wajibu hatukutafakari ya kesho.


Tulipoamua kufanya hayo yote, hatukuwaza vyema juu ya familia. Hatukuwaza juu ya misingi na malezi ya watoto wetu. Hatukuwaza nani atabaki nyumbani kusimamia jukumu kuu la nyumbani.

Tukaanza kuwakebehi akina mama wa nyumbani na kuwaita majina mabaya. Tukawaita magolikipa, chuma ulete, wajaza vyoo, mizigo, punching bags na kila jina tuliloona linatosha kuwafanya wachukie kusimamia jukumu lao kuu ambalo wengi wetu mama zetu walilifanya ndiyo maana leo tupo imara na tunawaona kama walikuwa wanawake wa chuma.

Wanawake nao walipoona imezidi, na kwamba akiwa dokta, mwanasheria, mfanyabiashara n.k ndo anaonekana bora na wa kisasa, nao wakaingia mzigoni.

Walipoelezwa kuwa maisha ni kusaidiana, bila kujua kuwa mama kusimamia jukumu la mji wake ndiyo msaada mkubwa kwa mumewe kuliko misaada yote, nao wakaingia kingi. Baba anaondoka na mama anaondoka. Mji unabaki na mtu ambaye huitwa housegirl au houseboy au ndugu wa mume au mke ambao nao wana ndoto zao, tabia zao, changamoto na mahitaji yao ambayo sasa yakawa ndiyo msingi wa malezi ya watoto wa baba na mama watafutaji.

Haijazidi miaka 30 toka huu mchakato usambazwe zaidi kupitia mifumo yetu ya kielimu, kisiasa na kijamii, Sasa tumeanza kuvuna matunda ya haki sawa, matunda ya kusaidiana, matunda ya mwanamke anaweza, matunda ya mkutano wa Beijing, na matunda ya kila aina ya utumbo tulioutafuna bila kuuosha. Sasa bakteria wa utumbo huo wameanza kutuozesha.

Mwelekeo huu wa matendo na matukio ya ushoga waweza kuwa mwanzo wa magumu mengi ambayo tutapitia kama jamii na taifa.

Wazungu na mashirika yao yaliyojificha kupitia taasisi za misaada chini ya dini, afya, siasa, elimu na sanaa wanajua ni kizazi gani kiliandaliwa ili kuja kuzalisha watoto ambao watapokea elements za LGBT (rejeeni haya mambo ya haki sawa yalianza kusambazwa zaidi lini nchini).

Sasa wanachofanya ni kuanza kuvuna matunda ya watoto wengi ambao hawakuelewa vyema na wazazi wao. Watoto waliokabidhiwa kwa walezi tofauti na wazazi wao kama vile wasaidizi wa kazi, walimu na wakufunzi wa dini.

Wengine ni watoto walioanza kutazama vipindi vya TV vyenye maudhui yanayoonesha ushoga wakiwa wadogo kuanzia miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni kuelekea 2010 na hata sasa kila tamthilia ya nje inayooneshwa nchini ina viashiria vya ushoga. Bado hatujashtuka.

Wazungu na washirika wao wanajua kizazi walichokiandika nao watazalisha kizazi dhaifu zaidi yao. Na ndiyo mchezo wenyewe unapoanzia.

Juzi Waziri wa Afya Dada Umy Mwalimu alisema na kuwakumbusha akina mama juu ya majukumu yao ya msingi ya kulea familia zao kuliko kujitokeza mitaani kama watafutaji na wafanyabishara zaidi. Akasema kuwa wasishindane na wanaume.

Kama Waziri ameona changamoto, tuna kila sababu ya kuona hili tatizo na kulichukulia kuwa tatizo la kitaifa.

Tulidanganywa tukadanyika. Leo tuna watoto ambao hata mzazi akiteseka, akiugua au hata akifa hawana uchungu maana wamelelewa zaidi na watu baki kuliko wazazi wao. Tuna watoto ambao wanathamini zaidi watu wa nje na marafiki kuliko walio wazaa. Na hawana mahusiano chanya na familia.

Ikumbukwe ukifanikiwa kuvunja bond ya familia, umeangamiza taifa zima.

Tumetikisa na tunaendelea kuvunja taasisi ya familia kwa kugeuza msingi wa majukumu kiasi kwamba kuna nyumba huwez kujua baba ni nani na mama ni nani. Utafutaji umekuwa ndo tatizo ambalo leo hii linavunja ndoa na kupelekea mauaji kitu ambacho hakikuwepo enzi za wazazi wetu wa chuma.

Na zaidi tuna familia nyingi za mzazi mmoja (single parent) ambazo zaidi kabisa ni za wanawake na watoto wao.

Hii ni kwasababu mwanamke wa kisasa mwenye kaelimu ka darasani hususani waliofika hadi vyuoni, wengi wao huona wanaweza hata wakiwa pekee yao. Mwisho ni mwendelezo wa uzinzi na mabadiliko ya ma-anko kila cku.

Matokeo yake mtoto anajifunza tabia hizo na kukosa misimamo ya kimaisha. Akifikisha umri wa balehe tu mama anabak analia na hana uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya mtoto wake. Na wakati huo huenda mtoto alishaambiwa baba yako alikufa au alikukataa.

Kuna mwanamama mmoja mmiliki wa taasisi moja inajihusisha na sanaa, sitaitaja jina. Naye ni single mother. Wakati mmoja alisikia wimbo uliokuwa na maadhi ya kuwatia moyo single mothers...wimbo ule ulimtia simanzi na hata akatoa machozi. Yeye ni single mother aliyefanikiwa, na alisema amefanikiwa akiwa single mother. Je kufanikiwa ndiko kulikomtoa machozi baada ya kusikiliza wimbo ule? Kwanini atoe machozi? Kwanini asifurahie tu ila hadi chozi linamtoka? Kuna mahusiano gani kati ya mafanikio na machozi? Nadhani kuna mihangaiko mingi na misukosuko na mateso mengi amepitia hadi kufanikiwa kama single mother ndiko wimbo ule ulimkumbusha hadi akatoa Machozi yake.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anayetamani kuishi pekee yake hadi uzee wake. Watoto huja kama baraka na matunda ya familia, ila wakati wao ukifika nao huondoka na kwenda kuanzisha familia zao. Wenza hubakia wawili wakiendelea kuliwazana na kushea hisia zao hadi mwisho wao.

Hakuna anayetamani kuishi peke yake na ikiwa yupo ni wachache sana na hawakuanzisha familia.

Mfano huo utufundishe kuwa tunahitaji familia ibaki kujengwa na baba na mama na siyo vinginevyo. Huu ni msingi na ni kanuni za kimaumbile. Labda changamoto nyingine zisizoepukika ziingilie kati. Napo bado mfiwa anayo haki ya kupata mwenza mwingine ikiwa bado anahitaji.

Kama taifa tujifunze kitu na tuanze kujirekebisha kabla hatujafikia wakati ambapo kabla ya kijana wa kiume na wa kike kuoana, watalazimika kupelekwa kupimwa kama ni mwanaume kweli au kama ni mwanamke kweli.

Wakati bado hatuna sheria ya moja kwa moja juu ya ushoga, kila mtu ashike na kutunza vyema alicho nacho.

Wanawake wafanyakazi na watafutaji tengeni muda kwaajili ya watoto na waume wenu. Jueni jukumu lenu kuu na la msingi ni usimamizi wa nyumba zenu na malezi ya watoto na waume zenu. Mengine hufuata baada ya hilo. Kubwa zaidi kumbukeni kuwa na utiifu na adabu kwa waume wenu bila kujali uwezo wenu kiuchumi.

Msisahau kuwa mwanamke mtumishi ni daraja la 3 katika ubora wa mke. Hivyo pamoja na hilo jitahidini sana kuweka uzito kwenye familia zenu maana utumishi una mwisho, ila familia ni mwendelezo wa maisha na vizazi vyenu.

Nanyi wanaume jitahidini kuwapenda, kuwafundisha, kuwahurumia na kuwahakikishia usalama wake na watoto wenu. Msiwachokoze ili wasiwe na uchungu nanyi. Mtakosa baraka. Mkumbuke kutoa sadaka kwa watoto wenu ili milango yenu ifunguliwe.

Pia tambueni kuwa jukumu la kwanza kuhakikisha usalama na ustawi wa familia ni lenu bila kujali mke ana kipato au hana kipato. Na ikiwa wake wenu wanawasaidia iwe ni katika utafutaji ambao mnaufahamu na kuusimamia. Na kama ni watumishi, watieni moyo na kusimamia vipato vyao visitawanyike na mwisho wakatawanya na familia zao kwa kiburi.

Na zaidi muwe na muda wa kukaa na familia ili kujua wapi kuna tatizo na kurekebisha mapema.
Kumbukeni kuwa mwanaume mtumishi naye pia ni daraja la tatu la ubora wa mume. Hivyo ule udhaifu utaokuwa unajitokeza kwenye familia ni lazima kutafuta namna ya kuupunguza ili watoto wenu waje kuwa imara zaidi yenu.

Pia wanafamilia tianeni moyo katika changamoto zenu kwa kuvumiliana na kuhurumiana.

Tanbihi...

Uimara wako ni matokeo ya yule mama ambaye sasa ni mzee. Ikiwa alikuwa mtumishi, ubora wako unauona, ikiwa alikuwa mfanyabiashara pia vilevile na ikiwa alikuwa golikipa bado ubora wako ni matokeo ya muda na jitihada zake.

Amua aina ya familia yako kulingana na malezi bora uliyopewa na siyo unayoona kwenye TV na kuambiwa na wengine.

Tunavuna matunda ya tulichopanda usiku na sasa tunashangaa kuona matunda hayana mbegu kama zile tulizopanda usiku.
Hata vitabu vya Mungu vilimtaka Mwanaume ale kwa jasho na mwanamke azae kwa uchungu. Maana yake kazi kuu ya msingi ya mwamke kwa mujibu wa maandiko ni kuzaa, kunyonyesha na kutunza/kulea familia na baba kazi yake ya msingi ni kujamiana na kutunza/kuilisha familia yake iwe jua iwe mvua. Mungu hakukosea kuagiza iwe hivyo, alijua hatari ya mama kuzaa kwa uchungu na kula kwa jasho kwa wakati mmoja. Mama zetu wa Sasa wanakula kwa jasho na kuzaa kwa uchungu, wako bungeni kwa miezi mitatu mfululizo, wako kazini kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa 3 usiku wanaporudi kazini, wako china kufuata bidhaa za biashara mwezi mmoja. Watoto hawana mtu wanaemuogopa na kumtii pale nyumbani, wameachiwa pesa nyingi za matumizi na shule, Kuna tv, smart phone na hela za bundle masaa 24 ili wasomee na kuwasiliana na wazazi ambao hawako nyumbani.

Mama zetu hawakusoma lakini watoto wao ni maprofesor wa kutumainiwa Leo hii inagwa waliwazalia nyumbani kwa msaada wa wakunga wa hadi. Tumepotoka sana kwa kuwa zoazoa wa maelekezo na tamaduni za magharibi
 
Umagharibi umetuelemea skuizi kila mtu anapeleka mtoto english medium wanakofundishwa kiuzunguzungu mtoto anadekezwa kamayai hatajembe halijui bullshhh...!! Nikuchezea tuu intanet kudere maporno.
Serikali iingilie mitaala ya shule binafsi watoto wafundishwe kazi za mikono wasidekezwe kipumbafu tutaharibu kizazi chetu.
Mashoga yafungwe yakaharibuliwe gerezani sio uraiani
 
Tunapambana nao kimya kimya, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu juu ubaya wa tabia hizi na athari zake, hivyo wanafundishwa kwanza kujitambua, this sometimes could be psychological problem, wanawekwa pahala panapofanania na sober house!
Mhhh, isije ikawa mnawapa sumu wafe, maana nyie hamshindwi kitu! [emoji848]
 
Umagharibi umetuelemea skuizi kila mtu anapeleka mtoto english medium wanakofundishwa kiuzunguzungu mtoto anadekezwa kamayai hatajembe halijui bullshhh...!! Nikuchezea tuu intanet kudere maporno.
Serikali iingilie mitaala ya shule binafsi watoto wafundishwe kazi za mikono wasidekezwe kipumbafu tutaharibu kizazi chetu.
Mashoga yafungwe yakaharibuliwe gerezani sio uraiani
Wewe una hasira kisa wanao wanasoma senti kajamba.

Na wewe pia ulisoma senti kajamba.

English medium ni shule za viwango, tafuta hela Kaka uachane na senti kajamba.
 
Umaskini Mbaya, ushoga ni Mbaya sana, ila Umaskini zaidi, Maana huna msimamo wakati hujiwezi, ni watu wachache sana kama Mugabe dunia hii, au Museven, na kizazi cha aina hiyo ndo kinaishilia hivyo
Njia za kupambana na tatizo hili kwa tanzania tumeliweka kwenye kundi la waathirika wa kisaikolojia hivyo ni watu wenye kuhitaji tiba za namna fulani za kiakili kwa kipindi fulani. Hivyo upambanaji wetu ni wa kipekee we solve the problem, HILI NI UGONJWA WA KIAKILI
Mhhh, isije ikawa mnawapa sumu wafe, maana nyie hamshindwi kitu! [emoji848]
HILI NI TATIZO KAMA YALIVYO MATATIZO MENGINE TATIZO HILI "PSYCHIATRIC DISORDER" HUTIBIWA INGAWA WENGINE HUONA JAMII HIYO IPEWE UHURU KITU AMBACHO HATUKIKUBALI NDIO MAANA KINATIBIWA TARATIBU KWA FARAGHA.
 
Sasa haya yote mnayajua, hizi kelele za nn??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Viongozi wetu wa afrika watumie akili ili kuishi kwenye dunia hii. Ulaya Magharibi zIko mbali sana na America lakini ziliamua kushirikiana na Marekani ili kupata ulinzi wa kijeshi na kibiashara. Nchi za Afrika ni lazima zifanye maamuzi magumu ya kuungana moja kwa moja na upande mmoja wenye nguvu kama uchina na urusi ili kutoa sauti ya pamoja. Hii tabia ya umalaya tunaofanya wa kutofungamana na upande wowote ndio chanzo Cha shida zetu nyingi. Tunajidhoofisha sisi wenyewe na tunadhoofisha china na urusi kuwa na nguvu sawa na Magharibi kwa manufaa ya usalama wa dunia.
 
Back
Top Bottom