Ni kwamba jamaa alitambua purpose ya yeye kuwa duniani.
Alipata maono (vision) au ndoto ya wapi apitie kufikia hayo makusudi (purpose).
Wanasema hivi ukitaka kujua maono yako yametoka kwa Mungu juu ya ndoto yako ya kimaisha basi kila mtu atakuona mwehu au mjinga au kichaaa.
Hata Nduguzo na wazazi wako wote watakupinga au kukudharau juu ya hiyo ndoto yako.
Unakumbuka jinsi Yusuf (Joseph) alivyoota ndoto atailisha famila yake yote?
Yaani baba , mama na kaka zake. Nao wote watakuwa chini yake?
Kaka zake walimchukia na kumuuliza unadhani wewe ni bora kuliko sisi? Wakamuita the dreamer. Mwishowe kwa chuki wakamtumbukiza kwenye kisima afe, baadaye wakamtoa na kumuuza utumwani Misri. Kule akapitia jela na mwisho akaishia kuishi nyumba ya mfalme Farao akiwa na mamlaka makubwa.
Baadaye akawasaidia nduguze na kuwalisha na kuwaleta Misri....
Ushauri:
1.Tafuta makusudi(purpose) ya maisha yako hapa duniani kisha utapata maono(vision)/ndoto za nini ufanye kutimiza ndoto zako.
2. Siyo kila mipango yako au ndoto zako zote za kimaisha uwashirikishe watu au nduguzo. Unaweza kujenga chuki kati yenu wakawa kikwazo cha kutimiza ndoto zako.
Soma Biblia Mwanzo 37:1-36..(Bible read Genesis 37:1-36..)
CC:
Saint Anne Mshana Jr Carleen Paula Paul nisaidieni kumtag Davinci