kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kama kuna barabara, daraja, kiwanja cha mpira, benki, uwanja wa ndege, kiwanda, shule, chuo, umeme, maji, au kikosi cha jeshi havikujengwa kwenye kijiji, kata, wilaya, mkoa au kanda kabla ya mtu wa kutoka kabila lao, kijiji chao, kata yao, wilaya yao, mkoa wao au kanda yao hajakuwa kiongozi mkubwa kwenye nchi na vikajengwa vyote baada ya mtu wao huyo kushika nafasi kubwa ya uongozi wa kitaifa.
Hii inachochea na kuamsha hisia za ukabila na ukanda kwenye nchi hasa wakati wa kuwatafuta viongozi wakubwa wa kitaifa.
Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa walikiepuka kikombe hicho lakini wengine waliyanywa maji ya kikombe cha ukabila, ukijiji, uwilaya, umkoa na ukanda kwa lugha ya walituonea sana na sasa ni zamu yetu.
Watanzania sio wapumbavu, wanaona na taratiiibu wataelekeza vichwa vyao kwenye kampeni za kikabila, kimkoa na kikanda nyakati za chaguzi.
Tuache kufukua mizizi ya mti wa umoja wa nchi iwe hata kwamakusudi au bahati mbaya, kwa kujua au kwa kutokujua.
Haiwekani upande mmoja kuna barabara ya vumbi inayounganisha wilaya na wilaya lakini kiongozi anatumia madaraka yake kujenga barabara kwao inayounganisha kijiji na kijiji kwa lami, watu hawana maji ya kunywa wewe kiongozi unajenga airport kijijini kwako, upande ule wa nchi hakuna umeme kabisa wewe unajenga uwanja wa kisasa wa mpira kwako, mkoa ule hakuna shule kabisa lakini wewe unajenga Ikulu kijijini kwako, watu wa kanda ile hawana hospitali kubwa lakini wewe unajenga barabara ya lami ya mkato kwenda kijijini kwenu.
Vitendo hivi kidogokidogo vinarejesha fikra za ukabila kwenye nchi.
Mfano, kiongozi mmoja ameitambua Israel ambayo ilikuwa hatuitambui kwasababu za kuikalia Palestina, kwanini kiongozi mwingine nae asiitambue OIC? mwingine kamwaga ugali makusudi, mwingine ataogopa nini kumwaga mboga makusudi?
Halahala kidole na jicho