Vitendo hivi vya Viongozi wetu wakuu vinaibua harakati za kikabila Tanzania

Vitendo hivi vya Viongozi wetu wakuu vinaibua harakati za kikabila Tanzania

Iko siku wagombea watazunguuka kwa kanda. Awamu hii kiongozi atatoka kanda ile na dini ile, akimaliza huyu ajae atakuwa wa kanda ile na dini ile. Tukifika hapo tumekwisha, lakini haiwezekani hadi leo kuja vijiji na kata havina umeme wala maji wala zahanati wakti vijiji vingine wanajenga uwanja wa ndege.
Damu nzito kuliko maji.

Hata Obama akiwa white house alimpa tenda kaka wa mke wake, ya mawasiliano ya jiji la Washington.

Lakini linapokuja suala uongozi wa nchi nzima marais siku zote wanatenda haki.

Hata awamu ya kwanza ya Julius Nyerere pale ikulu palikuwa panajaa watu wa Musoma, lakini siku zote alihubiri umoja wa kitaifa.
 
Watu Wana haki yakusema kuwe na uwiano sawa wa kimaendeleo Nchi nzima na sio upuuzi wakupeleka maendeleo sehemu Moja, unawezaje kufananisha makao makuu ya Nchi na Kijiji kama chato??.

Chato hata uchangiaji wa Pato la Taifa ni 0.01% sasa kuweka mabilion ya pesa nikuzitupa.
Kweli lazima kuwe na uwiano wa maendeleo, hiyo ndiyo itakayosababisha watu wote kuwa na uelewa wa aunaofanana.

Mtu hawezi kutumia nguvu nyingi kudai Katiba mpya badala ya kutumia nguvu hizo kudai maji, umeme na zahanati kwenye kijiji, kata, wilaya, mkoa au kanda yako.

Wakati Mbowe anadai Katiba mpya, Lissu alipaswa kudai maji, umeme na shule kwenye jimbo lake la Singida.

Inawezekana Mbowe kudai Katiba mpya ni sahihi kwake kwasababu Kilimanjaro kuna umeme, maji, barabara, shule na zahanati nyingi.
 
Damu nzito kuliko maji. Hata Obama akiwa white house alimpa tenda kaka wa mke wake, ya mawasiliano ya jiji la Washington.

Lakini linapokuja suala uongozi wa nchi nzima marais siku zote wanatenda haki. Hata awamu ya kwanza ya Julius Nyerere pale ikulu palikuwa panajaa watu wa Musoma, lakini siku zote alihubiri umoja wa kitaifa.
onyesha uwanja wa ndege Musoma/Butiama uliojengwa na Mwl Nyerere akiwa Rais kwa miaka 27 mfululizo na ulinganishe na Rais ambaye alitaka kugeuza kijiji chake kuwa Mkoa.

Rais Samia kuendelea kukamilisha kumalizia miradi yote ya aina hii ni dalili mbaya sana kwetu na kwa taifa, maana yake hakuna ubaya wa Rais kujianzishia miradi ya aina hii kwa aina hii, hivyo hataona ubaya na yeye, na mwingine na mwingine ajae kujianzishia utaratibu huu wa kujipendelea (presidency kwa marai wengine).

Rais Samia bila kupepesa macho anapaswa kusema mradi huu ni sawa tunaenda nao na huu sio sawa tunaachana nao kutokana bajeti na vipaumbele vya taifa ili liwe fundisho kwa marais wengine wajao.
 
Yuko sawa kabisa kulinganisha mana hata sasa tuna ubalozi wa Italy na Vatican, why not OIC?
Sababu za kuikataa Israel huko nyuma zinarandana na sababu zilizotumika kuikataa OIC huko nyuma.

Na sababu za kuikubali Israel kwenye awamu ya tato itafanana kabisa na sababu ya kujiunga na OIC kwenye awamu ya sita.
 
Kwahiyo wakiwa Marais sehemu wanazotoka automatically haziwi sehemu ya Tanzania and so hazistahili kuendelezwa!!?
Kwa maana hiyo hata wakiwachagua ndugu na watoto wao utasema kweni sio Watanzania.
 
Mavi ongozi ya sisim yameshatuona wananchi wa tz ni wajinga wakutupwa,mtu anaamua analotaka na anajua hamuwez mfanya kitu
 
Elimu inayotafutwa kwa ugumu wa kukesha usiku kucha mtu akisoma, ndio mkombozi wa makabila yanayoonekana ni madogo.

Pia umoja huanzia katika maisha ya kawaida kabisa ya kila siku ya makabila mbalimbali, kama kabila lako halina moyo wa umoja basi imekula kwenu.

Wachagga wanayo maendeleo kwa sababu hawatupani, katika shida za Covid 19 katika raha na starehe za mwisho wa mwaka wapo pamoja siku zote.
hapa ndipo yalipo mafanikio ya wachaga kwenye umoja japo sisi ilitaka kuwagawa
 
Aseee mtoa mada ungejaribu kufanya tafiti kidogo


Nadhani kuna kila sababu ya hoja zenye mashiko kama hizi zikija na nguvu ya matokeo ya utafiti na sio shuhuda za kitalii.

Ni sehemu gani ya nchi ambayo haikuguswa na jpm?
Kila kona ya nchi hasa sisi wa maporini maeneo yetu yameguswa saana.

Kuna mikoa ilitengwa sijui kwa mikakati gani na viongozi waliopita lakini huyu jamaa kaifungua.

Kama umejifungia majijini kwenu huwezi jua kwa nini huyu mwamba washamba tulimwita mwamba.
Tatizo lenu wajanja au watoto wa mjini hamna utu, hamtaki kile wajanja mnapata na sisi washamba tupate

Jipe kazi moja tuu
Zunguka toka huko jijini kwa wajanja njoo huku kwetu ushambani ndio utaona kwa nini washamba walimwelewa huyu jamaa.

Ungeona namna
Wagonjwa wanakufa huku dkt anachati
Wamama walivyokuwa wanafokewa na wengina kula kipigo kabisa huko leba.
Ukiingia ofisi yoyote kwa huduma wengine walilazimika kuweka mipira tumbomboni au matambala ilimradi tu aonekane ana kitambi ili kuhudumiwa
Huku ushambani huyu mwamba alitukomboa yani ilifika kipindi ukikanyaga rami iliyopit kijijini kwenu ukiangalia kwa mbaliiiiii ni kama unamwona jpm akikuhimiza kushangilia
Nikiangalia namna tulivyofungiwa umeme kwa tsh. 27000/= huku kijijini mpaka ukiwasha unaiangalia taa ikiwaka kwa mbaaaaaaaali ukiiangalia sana unamwona jpm kama katabasam
Kwenu wa mjini hili linaweza lisiwe ishu kwani kwenu mmevikuta na ni kawaida yenu kuwa navyo ila sisi hamjui namna tulivyolichukulia
Leo hii na bibi na mababu zenu huku na wao wanachaji simu nyumbani kwao hujui tuu

Hamjui namna tulivyojichanga changa kwa misimu miwili mpaka mitatu ya kilimo ili tuje mjini kuona
Rami
Taa ambazo hukesha zikiwaka ndani
Kushuhudia video bure ndani
Kuona taa zisizo na mwenyewe barabarani
Kwamba na mimi mtoto wa mwajuma anayejiremba kwa misuko ya twende kilioni niliweza kumhoji daktari, kumwambia askari, kuongea na mkuu wa shule, kuhudumiwa tena vizuri ndani ya ofisi za halmashauri.

ITATUCHUKUA MIAKA YA KUUMBWA KWA DUNIA KUMSAHAU HUYU MTU SISI WASHAMBA NA WANYONGE

NIKUIBIE TU SIRI
HUKU WENGINE TUME EDITI BAADHI YA SARA
YANI TUNAANZA NA

1 MITUME WETU (MTUME/YESU)
2. KWA WENGINE MARIA
3. JPM

TUNAMWOMBA MUNGU WETU KUPITIA HIYO LISTI




Ki ukweli huu ni ukweli mchungu jpm kwa washamba alikuwa katumwa na kuwaonjesha maana ya ulaia


Nyinyi wa mjini na nyie kilikuwa kipindi kigumu mnoo kwani hamkupenda na sie tufaidi

Naskia huko dar kuna stendi ya Magufuli sijui ilikuwaje
 
Haina tija kuhamia dodoma katika zama hizi za tehama, lakini sio mbaya sana kujenga dodoma sana kwakuwa tulikubaliana makao makuu ya tanzania yawe dodoma tangu zamani.
Lakini sio mbaya sana pia serikali wakijenga chato.
 
Kwahiyo wakiwa Marais sehemu wanazotoka automatically haziwi sehemu ya Tanzania and so hazistahili kuendelezwa!!?

Usichanganye kuendeleza na kujipendelea. Dhalimu ameotesha siasa chafu sana ndani ya nchi hii.
 
Anayepanga mipango ya maendeleo ni nani na anatumia vigezo vipi?

Wanaopanga ni binadamu na wana makabila yao kwahiyo upendeleo wa kijiji na kikanda hauepukiki

Zama hizi ni za uwazi na ukweli. Huko nyuma ilikuwa ngumu sana kujua kiongozi mkuu anafanya nini- siku hizi huwezi kuficha habari au maendeleo yanayoendelea sehemu ambazo wakuu wanatoka.

Huko nyuma tulikuwa tunadanganywa tu- kuna viongozi walikuwa hawaendelezi walikotoka lakini wanaendeleza sehemu ambazo wake zao wametoka.

Njia ya kuondoa ukabila na udini ni watanzania tuendeleze utamaduni wa kuoawana bila kujali dini au kabila.

Mawazo kwamba kiongozi akiendeleza sehemu anayotoka ni ukabila si sahihi kwasababu mtanzania yeyote hakatazwi kwenda sehemu hiyo ya maendeleo na kufanya shughuli zake.

Maendeleo yanaongeza mzunguko wa pesa mifukoni mwa watu wanaokaa maeneo hayo.

Tuwasihi viongozi waendelee kuleta maendeleo vijijini hasa walikotoka kuliko kupeleka na kuficha pesa zao kwenye mabenki ya Uswisi.

Tushangilie maendeleo na si kuyapiga vita- nchi inaendelea kwa hatua ndogo ndogo.
Mbegu ikiyokuzaa ilihujumiwa mno

Ilipaswa zitoe pacha angalau kuongeza idadi ya viumbe vyenye
Hekima
Busara
Heshima
Maono
Katika ulimwengu huu na kizazi hiki
 
Yuko sawa kabisa kulinganisha mana hata sasa tuna ubalozi wa Italy na Vatican, why not OIC?
Ungefatilia kwanini vatican ina ubalozi, oic ni nini na madhumuni ya kuundwa kwake pia soma katiba ya tanzania utapata majibu
 
Kama kuna barabara, daraja, kiwanja cha mpira, benki, uwanja wa ndege, kiwanda, shule, chuo, umeme, maji, au kikosi cha jeshi havikujengwa kwenye kijiji, kata, wilaya, mkoa au kanda kabla ya mtu wa kutoka kabila lao, kijiji chao, kata yao, wilaya yao, mkoa wao au kanda yao hajakuwa kiongozi mkubwa kwenye nchi na vikajengwa vyote baada ya mtu wao huyo kushika nafasi kubwa ya uongozi wa kitaifa.

Hii inachochea na kuamsha hisia za ukabila na ukanda kwenye nchi hasa wakati wa kuwatafuta viongozi wakubwa wa kitaifa.

Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa walikiepuka kikombe hicho lakini wengine waliyanywa maji ya kikombe cha ukabila, ukijiji, uwilaya, umkoa na ukanda kwa lugha ya walituonea sana na sasa ni zamu yetu.

Watanzania sio wapumbavu, wanaona na taratiiibu wataelekeza vichwa vyao kwenye kampeni za kikabila, kimkoa na kikanda nyakati za chaguzi.

Tuache kufukua mizizi ya mti wa umoja wa nchi iwe hata kwamakusudi au bahati mbaya, kwa kujua au kwa kutokujua.

Haiwekani upande mmoja kuna barabara ya vumbi inayounganisha wilaya na wilaya lakini kiongozi anatumia madaraka yake kujenga barabara kwao inayounganisha kijiji na kijiji kwa lami, watu hawana maji ya kunywa wewe kiongozi unajenga airport kijijini kwako, upande ule wa nchi hakuna umeme kabisa wewe unajenga uwanja wa kisasa wa mpira kwako, mkoa ule hakuna shule kabisa lakini wewe unajenga Ikulu kijijini kwako, watu wa kanda ile hawana hospitali kubwa lakini wewe unajenga barabara ya lami ya mkato kwenda kijijini kwenu.

Vitendo hivi kidogokidogo vinarejesha fikra za ukabila kwenye nchi.

Mfano, kiongozi mmoja ameitambua Israel ambayo ilikuwa hatuitambui kwasababu za kuikalia Palestina, kwanini kiongozi mwingine nae asiitambue OIC? mwingine kamwaga ugali makusudi, mwingine ataogopa nini kumwaga mboga makusudi?

Halahala kidole na jicho
MUULIANZA KWENU HUKO UCHAGANI TENA HAMKUWA VIONGOZI BALI MKIWA WATUMISHI WA UMMA
 
Ni eneo gani lilipendelewa na jpm zaidi ya dar?
1. Stand kubwa ya kisasa iko mbezi

2. Miundombinu ya kisasa iko dar

3. Flyovers zilijengwa dar

Baada ya dar, eneo lililofuata kwa kupendelewa ni dodoma, hapo mtu aiwaze tu dodoma kabla ya urais wa jpm na ile baada ya urais wa jpm

Mwanza walipelekewa daraja la busisi kigongo, chato airport

Je, kuna haja gani ya watu kupambania ukanda wa jpm ambao kiuhalisia haupo

Tufanyeni kazi
 
Back
Top Bottom