Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Damu nzito kuliko maji.Iko siku wagombea watazunguuka kwa kanda. Awamu hii kiongozi atatoka kanda ile na dini ile, akimaliza huyu ajae atakuwa wa kanda ile na dini ile. Tukifika hapo tumekwisha, lakini haiwezekani hadi leo kuja vijiji na kata havina umeme wala maji wala zahanati wakti vijiji vingine wanajenga uwanja wa ndege.
Kweli lazima kuwe na uwiano wa maendeleo, hiyo ndiyo itakayosababisha watu wote kuwa na uelewa wa aunaofanana.Watu Wana haki yakusema kuwe na uwiano sawa wa kimaendeleo Nchi nzima na sio upuuzi wakupeleka maendeleo sehemu Moja, unawezaje kufananisha makao makuu ya Nchi na Kijiji kama chato??.
Chato hata uchangiaji wa Pato la Taifa ni 0.01% sasa kuweka mabilion ya pesa nikuzitupa.
onyesha uwanja wa ndege Musoma/Butiama uliojengwa na Mwl Nyerere akiwa Rais kwa miaka 27 mfululizo na ulinganishe na Rais ambaye alitaka kugeuza kijiji chake kuwa Mkoa.Damu nzito kuliko maji. Hata Obama akiwa white house alimpa tenda kaka wa mke wake, ya mawasiliano ya jiji la Washington.
Lakini linapokuja suala uongozi wa nchi nzima marais siku zote wanatenda haki. Hata awamu ya kwanza ya Julius Nyerere pale ikulu palikuwa panajaa watu wa Musoma, lakini siku zote alihubiri umoja wa kitaifa.
Yuko sawa kabisa kulinganisha mana hata sasa tuna ubalozi wa Italy na Vatican, why not OIC?Umeongea vizuri ila umekosea kulinganisha suala la israel na oc
Sababu za kuikataa Israel huko nyuma zinarandana na sababu zilizotumika kuikataa OIC huko nyuma.Yuko sawa kabisa kulinganisha mana hata sasa tuna ubalozi wa Italy na Vatican, why not OIC?
Kwa maana hiyo hata wakiwachagua ndugu na watoto wao utasema kweni sio Watanzania.Kwahiyo wakiwa Marais sehemu wanazotoka automatically haziwi sehemu ya Tanzania and so hazistahili kuendelezwa!!?
hapa ndipo yalipo mafanikio ya wachaga kwenye umoja japo sisi ilitaka kuwagawaElimu inayotafutwa kwa ugumu wa kukesha usiku kucha mtu akisoma, ndio mkombozi wa makabila yanayoonekana ni madogo.
Pia umoja huanzia katika maisha ya kawaida kabisa ya kila siku ya makabila mbalimbali, kama kabila lako halina moyo wa umoja basi imekula kwenu.
Wachagga wanayo maendeleo kwa sababu hawatupani, katika shida za Covid 19 katika raha na starehe za mwisho wa mwaka wapo pamoja siku zote.
As long as wana sifa, acha wachaguliwe. Tusiwabague.Kwa maana hiyo hata wakiwachagua ndugu na watoto wao utasema kweni sio Watanzania.
Lakini sio mbaya sana pia serikali wakijenga chato.Haina tija kuhamia dodoma katika zama hizi za tehama, lakini sio mbaya sana kujenga dodoma sana kwakuwa tulikubaliana makao makuu ya tanzania yawe dodoma tangu zamani.
Kwahiyo wakiwa Marais sehemu wanazotoka automatically haziwi sehemu ya Tanzania and so hazistahili kuendelezwa!!?
Mbegu ikiyokuzaa ilihujumiwa mnoAnayepanga mipango ya maendeleo ni nani na anatumia vigezo vipi?
Wanaopanga ni binadamu na wana makabila yao kwahiyo upendeleo wa kijiji na kikanda hauepukiki
Zama hizi ni za uwazi na ukweli. Huko nyuma ilikuwa ngumu sana kujua kiongozi mkuu anafanya nini- siku hizi huwezi kuficha habari au maendeleo yanayoendelea sehemu ambazo wakuu wanatoka.
Huko nyuma tulikuwa tunadanganywa tu- kuna viongozi walikuwa hawaendelezi walikotoka lakini wanaendeleza sehemu ambazo wake zao wametoka.
Njia ya kuondoa ukabila na udini ni watanzania tuendeleze utamaduni wa kuoawana bila kujali dini au kabila.
Mawazo kwamba kiongozi akiendeleza sehemu anayotoka ni ukabila si sahihi kwasababu mtanzania yeyote hakatazwi kwenda sehemu hiyo ya maendeleo na kufanya shughuli zake.
Maendeleo yanaongeza mzunguko wa pesa mifukoni mwa watu wanaokaa maeneo hayo.
Tuwasihi viongozi waendelee kuleta maendeleo vijijini hasa walikotoka kuliko kupeleka na kuficha pesa zao kwenye mabenki ya Uswisi.
Tushangilie maendeleo na si kuyapiga vita- nchi inaendelea kwa hatua ndogo ndogo.
Ungefatilia kwanini vatican ina ubalozi, oic ni nini na madhumuni ya kuundwa kwake pia soma katiba ya tanzania utapata majibuYuko sawa kabisa kulinganisha mana hata sasa tuna ubalozi wa Italy na Vatican, why not OIC?
MUULIANZA KWENU HUKO UCHAGANI TENA HAMKUWA VIONGOZI BALI MKIWA WATUMISHI WA UMMAKama kuna barabara, daraja, kiwanja cha mpira, benki, uwanja wa ndege, kiwanda, shule, chuo, umeme, maji, au kikosi cha jeshi havikujengwa kwenye kijiji, kata, wilaya, mkoa au kanda kabla ya mtu wa kutoka kabila lao, kijiji chao, kata yao, wilaya yao, mkoa wao au kanda yao hajakuwa kiongozi mkubwa kwenye nchi na vikajengwa vyote baada ya mtu wao huyo kushika nafasi kubwa ya uongozi wa kitaifa.
Hii inachochea na kuamsha hisia za ukabila na ukanda kwenye nchi hasa wakati wa kuwatafuta viongozi wakubwa wa kitaifa.
Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa walikiepuka kikombe hicho lakini wengine waliyanywa maji ya kikombe cha ukabila, ukijiji, uwilaya, umkoa na ukanda kwa lugha ya walituonea sana na sasa ni zamu yetu.
Watanzania sio wapumbavu, wanaona na taratiiibu wataelekeza vichwa vyao kwenye kampeni za kikabila, kimkoa na kikanda nyakati za chaguzi.
Tuache kufukua mizizi ya mti wa umoja wa nchi iwe hata kwamakusudi au bahati mbaya, kwa kujua au kwa kutokujua.
Haiwekani upande mmoja kuna barabara ya vumbi inayounganisha wilaya na wilaya lakini kiongozi anatumia madaraka yake kujenga barabara kwao inayounganisha kijiji na kijiji kwa lami, watu hawana maji ya kunywa wewe kiongozi unajenga airport kijijini kwako, upande ule wa nchi hakuna umeme kabisa wewe unajenga uwanja wa kisasa wa mpira kwako, mkoa ule hakuna shule kabisa lakini wewe unajenga Ikulu kijijini kwako, watu wa kanda ile hawana hospitali kubwa lakini wewe unajenga barabara ya lami ya mkato kwenda kijijini kwenu.
Vitendo hivi kidogokidogo vinarejesha fikra za ukabila kwenye nchi.
Mfano, kiongozi mmoja ameitambua Israel ambayo ilikuwa hatuitambui kwasababu za kuikalia Palestina, kwanini kiongozi mwingine nae asiitambue OIC? mwingine kamwaga ugali makusudi, mwingine ataogopa nini kumwaga mboga makusudi?
Halahala kidole na jicho
Daah!!As long as wana sifa, acha wachaguliwe. Tusiwabague.