Naomba ni seme kidogo kuhusu hili swala la ushoga kama ambavyo watu wamekuwa wakilijadili. Mimi kwa uelewa wangu na kwa jinsi ambavyo nimelifahamu hili tatizo. Nitalizungumzia kwa mifano halisi kwa watu ambao nimewafahamu.
Kwanza kabisa, nimezaliwa nimekuta kuna majina au maneno watu wakiyatumia ktk jamii, 1. Msenge 2. Hanithi, na 3 wasagaji. Haya majina yamekuwepo miaka nenda rudi ktk jamii na sio msamiati mpya. Maneno haya hawaitwi wanyama bali ni sisi, na ktk jamii watu hawa wapo na ndio maana kumekuwa na maneno haya.
Kitu cha kwanza ni jamii kutambua kuwa vitendo hivi vipo na vinafanyika, na kwa nini vipo, hilo ndio swali la msingi lazima watu wajiulize kwanza na sio kulalamika tu na kuwanyooshea vidole wausika.
Nitoe mfano mmoja, kuna family moja niliwahi kuishi nayo kwa kipindi cha takribani miaka 10, ile family ilikuwa na watoto 4, wakike 3 na mdogo wao wa mwisho alikuwa wakiume.
Huyu mtoto alikuwa hapendi kucheza na watoto wa kiume hata kidogo, bali ni watoto wakike tu nilimfahamu akiwa na miaka 9, bado anasoma primary school, mpaka akaenda secondary school, na kila alivyokuwa ana kua, ndivyo alivyojidhihirisha kuwa na hisia za kike, na wazazi wake wamemkubali kwa jinsi alivyo, kumbuka ni mtoto pekee wa kiume.
Kwa hiyo hawa watu uzaliwa hivyo na sio kama watu wengi wanavyodhani. Pili kuna rafiki yangu mmoja aliolewa na mwenyezi Mungu aliwajalia kwakapata mtoto, lakini kabla ya hapo tulikuwa tunaambiwa kuwa jamaa anaingiliwa na wanaume wenzake, tukawa hatuamini ila amini usiamini mkewe alithibitisa hilo na ukawa ndio mwisho wa ndoa yao. Kumbuka wamezaa mtoto.
Nimejaribu kutoa mifano ya watu ninao wajua fika na sio kitu cha kusimuliwa na mtu. Kwa nini nimeamua kuanzisha uzi huu ni kujaribu kueleza kuwa hawa watu wapo na tunaishi nao sioni sababu ya jamii kuwatenga ni wenzetu na hivyo ndivyo walivyo, hawa kupenda kuwa hivyo walivyo kama wengi wanavyo amini.
Wazungu walichofanya wao ni kutambua tatizo na kuwatambua ni sehemu ya jamii yao. Ila kwa Tanzania tunahisi kuwa ni utamaduni wa kizungu wakati sio kweli, ni kutafuta mtu wa kumtwisha lawama pasipo kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia.
Jaribu kufikiria mtaani, shuleni au hata makazini tumeishi na watu wa jinsi hiyo ila tulikuwa tunasema, huyu ana tabia za kike au za kiume, jaribuni kukumbuka.
Kwa hiyo mimi nawaona ni watu ambao ni vilema kama kilema kingine chochote kile, tunatakiwa kuwa angalia kama ni watu ambao wanahitaji kuwa sehemu ya jamii.
Hebu chukua kesi ya yule jamaa wa zanzibar, unaenda kumpima, kisha majibu yana kuja ameingiliwa, je uliwahi kujiuliza background history yake kabla ya kumpima?.
Au ndio sisi tunaamini bado tunaamini kuwa watoto wetu hawajamiani mpaka wanapofunga ndoa au akipata ujauzito ndio wazazi wanasituka.
Mwisho tunapojadili swala la ushonga tuliangalie kwa upana wake na sio kwa ushabiki