Utafiti wako hauna uhalisia kwa kiasi fulani,mkuu.
Miaka kadhaa nilihamia sehemu Fulani. Demu wangu akaja kunitembelea akakaa kama wiki.Kuna tom boy wa pale mtaani akamwona ila hakujua kama ni Manzi yangu,akamletea pigo za kumsifia uzuri. "Cheupe mzuri sana " bibie anaitikia Asante,kumbe tom boy ana yake
Siku Moja Jioni hapo home kukawa na birthday party alafu Mimi ni mgeni Nina kama wiki mbili sijazoeana na mtu. Jamaa mmoja akanifata "oii mwana njoo tuchome mbuzi hapa nje,tunahitaji kampani yako Mzee!! Nikaona fresh Wacha nijichanganye ,nizoeane na watu pia. Tukatoka wote Mimi na "wife" tukaungana nao kuparty...mziki mkubwa !!
Wakati muziki ukiendelea,Yule demu tomboy nikaona kama analeta pigo za kumganda bibie ila sikutilia maanani.
Muda kidogo nikaona bibie karudi ndani bila kuniambia. Namfuata na kumuuliza kimetokea nini mbona ghafla kabadilika akaniambia yule demu aliyesuka Rasta analazimisha kunikula mate na kunishika maziwa na huku chini. Alafu ananiambia anaomba "akaninanii" atanipa Hela yoyote ninayoitaka eti amenipenda.
Nilishikwa na wivu uliochanganyika na hasira,nikataka nimfate ila wife akanishika mkono na kuniambia niache nisije kuharibu shughuli ya watu.
Kesho yake mapema tu nikamfata kwao mana tulikuwa majirani. Nikamchimba bonge la biti,akaomba msamaha akasema hakujua kama ni demu wangu eti!! Tangu siku hiyo nikiona wanawake kwa wanawake wanakuwa marafiki kupitiliza Tena mmoja awe na Rasta ,Huwa natilia shaka kidogo.