●Zamani sisi ukianguka chini hakuna kulia vitoto vya sikuizi vitalia kama vile viko msibani na hapo kamejikwaa tu.
●Watoto wa siku hizi wakitoka shule wasipokuta chai na chakula cha mchana ni vita , sie zamani tulikuwa tukitoka shule unakuta mboga tu utasonga ugali ule mwenyewe.
●Michezo yetu ya zamani ilikuwa ya nguvu tulikuwa tunacheza mchezo mmoja wa tuletule tumbakishie baba ule mchezo mtoto wa mama huwezi kucheza, leo sasa watoto ni katuni tu kikitoka shule nikatuni tu hakitakia ubadili channel .
● watoto wa. Siku hizi wazazi ndio wa kwanza kuamuka wao wamelala kikija kuamka ni saa tatu au saa nne asbh, zamani sisi ile saa kumi na moja kamili upo macho na hii imetujenga sana kikazi.
● Watoto wa siku hizi kufanya kazi za nyumbani wanaita mateso kizazi cha ajabu sana hiki, sisi zamani kufanya kazi ilikuwa lazima na usipofanya utakula viboko vya kutosha.
● watoto wa sikuhizi wanachqgua mitindo ya kunyoa nywele eti ninyoe kama jux , sisi zamani ilikuwa ni kipara tu twna kinapakwa mafuta mengi tena unanyolewq kwa wembe ikitokea umekatwa bahati mbaya hakuna kulia.
● Watoto wa siku hizi vikipigana huko, kikipigwa kinakuja kinalialia , sisi zamani ukipigwa na wewe piga hakuna kulia ukija unalialia unaongezewa kipigo.
●Watoto wa siku hizi ice cream mara chocolate kinakuagiza kabisa ukirudi uje na chocolate yangu utadhani kimekuwekesha hela, zamani ni uji tena wa chumvi ya mawe chakula chetu ni ugali daily na hakuna kuuliza utakachokuta ndio unakula hicho vitoto vya sasa wali na chips tu.
● watoto wa sasa eti ugali ni chakula cha mifugo kama wahenga wakisikia kauli hii hivi vitoto vitalaaniwa.
● Usipokapa hela ya shule ni vita yaani hatari , zamani sisi hakuna kupewa hela ya kula shule kula utarudi ule nyumbani.
Niishe tu hapo ila vitoto vya 2000 mmekuwa kimayaimayai sana, na hiki ndio kizazi maadili yameporomoka sana ukijichanganya kinakuonyesha dole la kati asee