Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

Vitu gani vya kuzingatia hasa unapofanya biashara ya uuzaj wa mayai ya kisasa?

ila ingekuwa vizuri kama ungeeleza ni mayai gani hasa unayotaka kufanya biashara ya kisasa au ya kienyeji?
mawazo yangu katika hili,kama ni ya kienyeji inatakiwa uangalie pia soko limekuwa gumu kutokana na kwamba hayatumiki sana kibiashara kwasababu ni madogo na ni gharama haya yanatumika sana kwa matumizi ya familia

ila kama ni ya kisasa hapo sawa haya yapo kibiashara ila sasa sio hadi uende singida maeneo tunayoishi kuna watu wengu wanayauza inatakiwa utafute sehemu ya karibu uwe una chukua mzigo
 
Kuharibika tatizo ya kienyeji hayakai sana na joto la dar balaa tupu
 
Unayaweka kwenye maboksi unaweka na pumba za mpunga au maranda ila wanaouza wanajua jinsi ya kuyapanga ili yasivunjike ila hapo kwenye joto ndiyo Sina uhakika maana Singida na Dar parefu.
Hahahaha kwahio anaweza kupokea vifaranga Tray kadhaa badala ya Mayai tray 10
 
kama great thinker nimebuni iv apa dsm mayai najumua 7000 kila trei af nauza 9000 mana saiv DSM mayai yamepanda kidogo alaf napita katika vijiwe vya chipsi mbalimbali vingine ambavyo vipo mbali na masoko kabisa naingia ob na watu nakua nakupa trei mbili au moja alaf nakuja kuchukua pesa baada ya siku mbili nakua napata faida ya 2000 mara 40 ndan ya siku mbili inakua 80000 na mtaj wa trei 40 ni 280000 kwa mwez ni 1200000 ndan ya mwaka ni milionaire....na usafiri kuna mchiz ananiuzia lipikipik

Sent using Jamii Forums mobile app
Mahesabu ya mdomoni kuhusu faida kwenye biashara huwa mepesi sana mkuu, sijaona ukiwaza kuhusu Risk yeyote hapo, kuna kutapeliwa, mzigo kuharibika, kuuziwa mayai mabovu na mengineyo! We umeona 1,200,000 tu bila gharama nyingine sio!
 
Sikuvunji moyo ila umeongea kirahisi sana, umeassume kama hamna changamoto yoyote katika hizo siku mbili upate hiyo 80,000.

1) Hiyo pikipiki unauziwa bei gani? Maan hujaweka kwenye mtaji ina maana hii biznez ni nzuri kwa mtu mwenye pikipiki tayari. Na kama ni kukodi Kwa kawaida hesabu za pikipiki ni kurudisha elf 8 hadi 10 kwa boss kwa siku, hujaweka hii.

2) Hayo mayai ya 7000 kwa trey unapata wapi kila siku? Believe me kuna kipindi mayai yanaisha kwa supplier wako na inabidi utafute sehemu nyingine na bei inakuwa tofauti, ukipata kwa lets say 8000 kwa trey kwa siku mbili au tatu ujue ni faida nusu tayari.

3) Hakuna kitu kibaya kama kumuachia muuza chips hela kwa siku mbili, kibanda cha chips faida yake ni ndogo na boss anachukua almost kila siku hivyo kurudi baada ya siku mbili na kudai hela ya juzi mtaanza kutafutana lawana. Ukipigwa kalendar hata siku moja tu deni linakuwa kubwa na inazidi kuwa ngumu kulipa, ushauri hapa ni kupita kila siku kesho yake kuchukua hela ya jana. Na je what if hayakuisha atakuwa tayari kulipa yote na kuchukua tena mzigo? Wewe unasema 80,000 faida siku mbili..[emoji58]

4) Umesema unategemea kuzungusha kama trey 40 kwa siku hizo mbili ili upate faida ya hiyo 80,000. Na pikipiki yako unazungukaje na trey 20 za mayai? Au utakuwa unaenda na kurudi kila saa, hivyo vibanda havipo mtaa mmoja hivyo utakuwa unapeleka vipi hizo trey 40 zote kwa hizo siku mbili kwa pikipiki? Kama unabeba kidogokidogo je vipi kuhusu mafuta(petrol).

5) .......

-Wengi tunakimbiliaga tu kwenye faida(sijui milion ngapi kwa mwezi) na tunasahau changamoto zake, ukianza biashara baada ya week mbili tu unaacha na unakuwa umepoteza muda na hela. Tuache ndoto za kina forever living kuwa ukialika tu watu watano na hao wakaalika wengine basi unakuwa milionea. Nijibu kwa hoja hizo changamoto hapo juu ili tusaidiane kujikwamua.
Big up sana kwa hii idea nzuri !
Mkuu umeongea point ambayo hata mi nilijaribu kumwambia mwana, biashara ina risks zake sasa wengi wetu tume focus katika faida tu! Sio kwamba haitapatikana ila kuna wakati business inaweza kukukataa ikala faida za mwanzo!
 
Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.

uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.

kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.

mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.

Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.

0658438825 nicheki
 
Habari wakuu,
Kadri siku zinavyokwenda naona wafugaji wa kuku kwa ajili ya mayai wanaongezeka. Nataka kujua kwa wale wanaofanya biashara ya kuuza mayai mambo yafuatayo?
-changamoto wanazokumbana nazo
- hali ya soko ya mayai ikoje
-faida inayopatikana kwa kila trei
-upataji wa mayai kwa wale wasio wafugaji changamoto zake
-wafugaji wa moja kwa moja changamoto gani wanakutana nazo
Na taarifa zozote zile zinazohusiana na hii biashara
Karibuni kwa mjadala
 
Kama unafuga kuku wa mayai unayo mengi...chukua fremu kitunda ,wale wanaotembeza na vibaskeli no wateja wakubwa sana wa mayai na wanachukua trei ata 20 kila mteja mmoja...ukiwaekea bei nzuri wanajazana dukani kwako...unaweza kuta unauza trey 200 kwa siku...na frem n bei poa sana...biashara unafanya asubuhi sana kwenye saa nne unafunga zako duka unafanya mengine
 
Biashara hii ukitaka kuifanya vizuri tafuta usafiri kama vile bajaji, unachofanya unatafuta chanzo kizuri cha mayai hasa kwa wafugaji, unachukua mzigo unapeleka kuuza, mfano ukiwa na uhakika wa kuuza tray 50 kwa siku na na tray moja unapata faida ya 1000/= maana yake kwa siku utakuwa unapata 50000/= ukitoa gharama za usafiri kama 15000 unabakiwa na 35,000/=.
Wateja wa kubwa wawe ni wachoma chips na maduka ya reja reja.
 
Biashara hii ukitaka kuifanya vizuri tafuta usafiri kama vile bajaji, unachofanya unatafuta chanzo kizuri cha mayai hasa kwa wafugaji, unachukua mzigo unapeleka kuuza, mfano ukiwa na uhakika wa kuuza tray 50 kwa siku na na tray moja unapata faida ya 1000/= maana yake kwa siku utakuwa unapata 50000/= ukitoa gharama za usafiri kama 15000 unabakiwa na 35,000/=.
Wateja wa kubwa wawe ni wachoma chips na maduka ya reja reja.
Nimekuelewa mkuu, unachokisema ni sahihi na nimeanza kufanya, ulichokiandika ndicho kinachotokea
 
Kama unafuga kuku wa mayai unayo mengi...chukua fremu kitunda ,wale wanaotembeza na vibaskeli no wateja wakubwa sana wa mayai na wanachukua trei ata 20 kila mteja mmoja...ukiwaekea bei nzuri wanajazana dukani kwako...unaweza kuta unauza trey 200 kwa siku...na frem n bei poa sana...biashara unafanya asubuhi sana kwenye saa nne unafunga zako duka unafanya mengine
Kitunda ni wapi huko mkuu, hilo soko nimelitamani sana
 
Kama unafuga kuku wa mayai unayo mengi...chukua fremu kitunda ,wale wanaotembeza na vibaskeli no wateja wakubwa sana wa mayai na wanachukua trei ata 20 kila mteja mmoja...ukiwaekea bei nzuri wanajazana dukani kwako...
Bei nzuri ya kuvutia wa vibaskeli huko ktunda ni kama ngapi kwa trei?
 
SOKO KUBWA.

Tuanze na Biashara ya Chips Miji mikubwa kama Dar.

CHIPS ndo soko kuu namba 1 la mayai, Jiji kama la Dar kuna Vibanda vya chips visivyo na idadi na ukienda kuna teri na trei zinashushwa na kuisha pale.

Chips ina consume mayai sana na ndo soko kubwa kabisa la mayai.

SASA JE CHIPS Inatumia mayai yapi? KISASA au KIENYEJI?
Jibu unalo.

2. Bekary
Bekary zinatumia mayai mengi mno tena mno, Hawa no soko jingine kubwa kabisa la mayai hasa kwenye kuoka vitu kama keki na kadhalika.

Bekary hununia mizigo ya trei za mayai kila siku.

JE BEKARY hutumia mayai gani? KISASA au KIENYEJI?

3.Mahoteli makubwa ya kitalii.
Hawa ni watumiaji wa tatu wakubwa mno wa mayai ukija kwa single use joteli moja kama Serena inaweza kuwa inatumia mayai zaidi ya wakaanga Chips 30 hapo mjini.
Mayai yana pasuliwa mahotelini aaikuambie mtu.

Kwenye miji kama Arusha wakati wa Msimu wa utalii huwa Mayai yanakosekana kabisa make consuption huwa iko juu mno make Hoteli moja unakuta kwa siku inatumia si chini ya trei 30 hapo ni chini ya kiwango.Piga idadi yao.

JE HOTELI ZA KITALII hutumia mayai ya KISASA au KIENYEJI?


4.Matumizi ya majumbani

Hawa ndo watumiaji wa miwsho au ndo soko la mwisho la mayai. Hapa ni pale mru anapo nunua kwenda kuwaangaangia watoto wake au kuwachemshia watoto wake

Hapa sasa ndo Soko la Mayai ya Kienyeki linapo ibukia ndo uwanja wake wa nyumbani.

Ingawa bado hapa wana shindana oia na Kisasa.

Ila kwa Twajwa hapo juu hakuna Kienyeji

PIA TAMBUA HILI.

Miji mikubwa kama Dar, Arusha, Mwanza na Dodoma ba Mbeya ndo Masoko makubaa ndo kuliko na Consumption kubwa.

Matumizi ya mayai kwa mji kama Babati manayara yanaweza zidiwa mbali mno na mtaa mmoja wa Dar.

Hivyo jamani tuwe tunafanya utafiti tuache mihemuko.

Hivi mfano Dar hapo wapi uliona wakaanga Chips wanahangaika na mayai ya kienyeji?

Au kwa kweli Bekary waanze kutafuta mayai ya kienyeji ndo waokee keki zao?

MWISHO

Soko la Mayai ya Kisasa ni kubwa mno achana na story za mitaani na vijijini wacha kulinganisha na ulaji wa Mayai kienyeji kijijini kwenu ndo ufanye Case study.

kuku wa layers ni Cormercial breeds.
 
Uko sahihi sana mkuu mimi ni mfugaji wa kuku chotara nauza mayai ya kuroiler.Pia kwasababu ya uhitaji wa mayai ya kisasa huwa nanunua kwa jumla trei 100 then nawauzia watu wa chips.Soko kubwa la mayai ni wauza CHIPS.

Na hao wadau wanaangalia vitu vitatu nitavipanga kulingana na umuhimu wake.

1.Bei
2.Size
3.Kiini cha njano

Sasa mayai ya chotara au kienyeji hayawezi kukidhi hivyo vigezo kwanza yanauzwa bei juu pili ni madogo kwa size kigezo cha tatu walau yanakidhi kuwa na kiini cha njano. Huwezi mueleza mtu wa chips Habari za mayai kuwa yana mbegu bla bla hizo hazina maana.
 
Ni bakery sio bekary. Bakery mayai yanayotumika ni ya kisasa coz ya Gharama. Kwa watengenezaji WA keki za jumla hasa zile ndogo ndogo ndio wanunuaji Wakubwa WA mayai. Hizi bakery za kawaida ununuaji Uko wastani sio mkubwa Kama wale WA keki za jumla.
 
Back
Top Bottom