colin_morgan
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 2,443
- 2,912
Nipo siti ya mbele kupata elimu ya biashara hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha kwahio anaweza kupokea vifaranga Tray kadhaa badala ya Mayai tray 10Unayaweka kwenye maboksi unaweka na pumba za mpunga au maranda ila wanaouza wanajua jinsi ya kuyapanga ili yasivunjike ila hapo kwenye joto ndiyo Sina uhakika maana Singida na Dar parefu.
Mahesabu ya mdomoni kuhusu faida kwenye biashara huwa mepesi sana mkuu, sijaona ukiwaza kuhusu Risk yeyote hapo, kuna kutapeliwa, mzigo kuharibika, kuuziwa mayai mabovu na mengineyo! We umeona 1,200,000 tu bila gharama nyingine sio!kama great thinker nimebuni iv apa dsm mayai najumua 7000 kila trei af nauza 9000 mana saiv DSM mayai yamepanda kidogo alaf napita katika vijiwe vya chipsi mbalimbali vingine ambavyo vipo mbali na masoko kabisa naingia ob na watu nakua nakupa trei mbili au moja alaf nakuja kuchukua pesa baada ya siku mbili nakua napata faida ya 2000 mara 40 ndan ya siku mbili inakua 80000 na mtaj wa trei 40 ni 280000 kwa mwez ni 1200000 ndan ya mwaka ni milionaire....na usafiri kuna mchiz ananiuzia lipikipik
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeongea point ambayo hata mi nilijaribu kumwambia mwana, biashara ina risks zake sasa wengi wetu tume focus katika faida tu! Sio kwamba haitapatikana ila kuna wakati business inaweza kukukataa ikala faida za mwanzo!Sikuvunji moyo ila umeongea kirahisi sana, umeassume kama hamna changamoto yoyote katika hizo siku mbili upate hiyo 80,000.
1) Hiyo pikipiki unauziwa bei gani? Maan hujaweka kwenye mtaji ina maana hii biznez ni nzuri kwa mtu mwenye pikipiki tayari. Na kama ni kukodi Kwa kawaida hesabu za pikipiki ni kurudisha elf 8 hadi 10 kwa boss kwa siku, hujaweka hii.
2) Hayo mayai ya 7000 kwa trey unapata wapi kila siku? Believe me kuna kipindi mayai yanaisha kwa supplier wako na inabidi utafute sehemu nyingine na bei inakuwa tofauti, ukipata kwa lets say 8000 kwa trey kwa siku mbili au tatu ujue ni faida nusu tayari.
3) Hakuna kitu kibaya kama kumuachia muuza chips hela kwa siku mbili, kibanda cha chips faida yake ni ndogo na boss anachukua almost kila siku hivyo kurudi baada ya siku mbili na kudai hela ya juzi mtaanza kutafutana lawana. Ukipigwa kalendar hata siku moja tu deni linakuwa kubwa na inazidi kuwa ngumu kulipa, ushauri hapa ni kupita kila siku kesho yake kuchukua hela ya jana. Na je what if hayakuisha atakuwa tayari kulipa yote na kuchukua tena mzigo? Wewe unasema 80,000 faida siku mbili..[emoji58]
4) Umesema unategemea kuzungusha kama trey 40 kwa siku hizo mbili ili upate faida ya hiyo 80,000. Na pikipiki yako unazungukaje na trey 20 za mayai? Au utakuwa unaenda na kurudi kila saa, hivyo vibanda havipo mtaa mmoja hivyo utakuwa unapeleka vipi hizo trey 40 zote kwa hizo siku mbili kwa pikipiki? Kama unabeba kidogokidogo je vipi kuhusu mafuta(petrol).
5) .......
-Wengi tunakimbiliaga tu kwenye faida(sijui milion ngapi kwa mwezi) na tunasahau changamoto zake, ukianza biashara baada ya week mbili tu unaacha na unakuwa umepoteza muda na hela. Tuache ndoto za kina forever living kuwa ukialika tu watu watano na hao wakaalika wengine basi unakuwa milionea. Nijibu kwa hoja hizo changamoto hapo juu ili tusaidiane kujikwamua.
Big up sana kwa hii idea nzuri !
Wanandugu kama ambavyo tumekuwa tukishirikiana kubadilishana mawazo kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hatimaye kumekucha.. Mimi nafuga kuku 1000, kati ya hayo 580 ambao ni awamu ya kwanza wanaanza kutaga. awamu ya pili wanaanza kutaga Januari. nina soko la mayai katika duka moja. ila ningependa kupata soko jingine pia.
uzalishaji unategemea kuwa kama tray kama 10 kwa siku au 70 kwa wiki. production itaongezeka kadri ziku zinavyoenda na pia wale wa awamu ya pili wakianza kutaga.
kama kuna mtu ahahitaji mayai au anaweza kunipa mawazo wapi naweza kuyauza haya mayai kwa ujumla tupeane ushauri.
mayai ni wa kuku wa kisasa. wale wa kienyeji nitaanza kuwafuga next year baada ya kukamilisha sehemu ya kuwaweka shambani.
Note: nafugia Dar, maeneo ya bunju.
Nimekuelewa mkuu, unachokisema ni sahihi na nimeanza kufanya, ulichokiandika ndicho kinachotokeaBiashara hii ukitaka kuifanya vizuri tafuta usafiri kama vile bajaji, unachofanya unatafuta chanzo kizuri cha mayai hasa kwa wafugaji, unachukua mzigo unapeleka kuuza, mfano ukiwa na uhakika wa kuuza tray 50 kwa siku na na tray moja unapata faida ya 1000/= maana yake kwa siku utakuwa unapata 50000/= ukitoa gharama za usafiri kama 15000 unabakiwa na 35,000/=.
Wateja wa kubwa wawe ni wachoma chips na maduka ya reja reja.
Kitunda ni wapi huko mkuu, hilo soko nimelitamani sanaKama unafuga kuku wa mayai unayo mengi...chukua fremu kitunda ,wale wanaotembeza na vibaskeli no wateja wakubwa sana wa mayai na wanachukua trei ata 20 kila mteja mmoja...ukiwaekea bei nzuri wanajazana dukani kwako...unaweza kuta unauza trey 200 kwa siku...na frem n bei poa sana...biashara unafanya asubuhi sana kwenye saa nne unafunga zako duka unafanya mengine
Bei nzuri ya kuvutia wa vibaskeli huko ktunda ni kama ngapi kwa trei?Kama unafuga kuku wa mayai unayo mengi...chukua fremu kitunda ,wale wanaotembeza na vibaskeli no wateja wakubwa sana wa mayai na wanachukua trei ata 20 kila mteja mmoja...ukiwaekea bei nzuri wanajazana dukani kwako...