Vitu hivi vinamaliza pesa bila sababu za msingi, fanya hivi kuepukana navyo

Vitu hivi vinamaliza pesa bila sababu za msingi, fanya hivi kuepukana navyo

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Salaam jamiiforum.

Threads zangu nyingi zinawahusu zaidi vijana tena ambao hawajaoa kwani ndilo kundi ambalo lipo onfire kutokana na umri wao lakini pia hata baadhi ya watu wazima siyo mbaya tukakumbushana.

1.Acha tamaa ya kuweka pesa ili upate pesa.

Ni dhahiri shahiri vijana wengi wanatumia kila mbinu kujipatia pesa kirahisi.yaani uweke laki tano uvune million tano, serious!!
Hapa ndipo kampuni uchwara Kama LBL ,Kalinda ,na vijiforex kibao ,zinapopata mwanya wa kuwaibia kirahisi na kuacha vilio.

2.Fanya mazoezi nyumbani ya wastani.

Siku hizi ni rahisi mtu kumkuta Gym Kwa kusudi la kupunguza uzito,yaani ulipie pesa kwa kitu ambacho kinawezekana kabisa,ni kiasi cha kufanya mazoezi hapohapo kwako ,kama kujiwekea utaratibu wa kupiga
Pushups and squats kadhaa kila mara na kegel ,kuliko kugharamia kitu kinachowezekana.

3.Acha kununua vitu vya kuongeza nguvu za kiume.

Ndugu zangu,wadogo zangu na wanangu,mnapaswa muelewe ,
Hakuna dawa rasmi ya kuongeza nguvu Bali kuna dawa kama ganzi za kufanya misuli iwe hivyohivyo kama zile za kusisimua misuli Kwa wanamichezo. Cha kufanya ni Kula vizuri,fanya mazoezi, kunywa maji mengi ili kutengeneza mzunguko wa damu pamoja na kuwa na mpenzi sahihi mwenye hisia na wewe.

4.Punguza kumiliki vifaa tofauti na maisha yako.

Kumiliki TV kuuuubwa ya gharama na Una laptop geto wakati huna kazi za maana kwenye hiyo PC tofauti na kuangalia movie, kama huna kazi au mchongo wa uhakika,mashine za kufulia na friji lakini muziki wa mamilion upo geto.hivi havimfai kijana anayejitafuta.

5.Usilazimishe kumiliki mwanamke Kwa kuwatambia wana.

Iko hivi ,yaani Una demu mkali,na anakuchuna kweli ,na pengine hana mapenzi na wewe ila unatumia nguvu kubwa kuwa naye ili kuwalingishia watu kwamba unamiliki pisi kali ikiwa unaumia na kuumizwa vibaya.miliki mwanamke anayekuheshimu na kukuvumilia wapo kibao tu,sema wanetu mnaangalia sana Sura na ta....

6.Jifunze na kujizoesha kutembea Kwa miguu.

Utaokoa Sana buku buku zako,lakini inakupa ukakamavu na kuhimili mishindo siyo safari fupi ,umepanda boda au daladala,

7.Kula sehemu na vyakula unavyomudu.

Usipelekeshwe na hesabu za watu wa mitandaoni humu kila mtu tajiri,
Piga msosi Kwa mamantilie bei ni kuanzia 2000 tu yaani bei rafiki kabisa.

8.Punguza mitindo ya nywele.

Hairstyles ni Kwa wasanii na waigizaji kama haupo kwenye kapu hilo ni bora kunyoa kawaida,tu ni kuanzia 1500 hadi 2000. Kuliko kwenda saloon ya bei ghali ikiwa kipato chako hakiruhusu.

Ni hayo tu ila zingatia vitu vifuatavyo hakikisha ni vya gharama ili kujitengenezea heshima yako.

Simu iwe ya gharama,
Kiatu kiwe cha gharama,
Kama ni saa iwe ya gharama.

Hivi vitu vitatu ni utambulisho tosha Kwa kijana mpambanaji .
 
Simu -smartphone ni 'poverty gateway' unamiliki ya gharama ili iweje, itakula vzr kuliko ww
Saa kazi yake ni moja tu...unaweza tumia saa ya simu pia
Kiatu cha gharama?
Binafsi hii conclusion yako naipinga
 
Back
Top Bottom