Vitu/vifaa gani ulivinunua kwa mihemko na umejikuta huvitumii kabisa?

Vitu/vifaa gani ulivinunua kwa mihemko na umejikuta huvitumii kabisa?

Ha ha mimi kwavmanunuzi ndio mwenyewe,sasa huo mkandavwa ngozi inakubidi ununue mashine yake ya kutoboloea matundu,kama upo dar nenda kwenye maduka makubwa ya mikanda wanakiuza hicho kifaa pia,ama kuhusu air frier hicho ni kifaa muhimu sana kwako,kwamba ulimcha kuku kwenye air frier hakuwa mtamu,hapana dosari ipo kwako ni marination ndio hukufanya,ili kuku awe mtamu mfanyie marination.Vifaa ni muhimu sana ni namna ya kuvitumia
Kwa mkanda achukue screwdriver unafungua hapo halafu unakata kwa kiwango unachotaka
 
Wengine Bado tupo Kwa wazazi😁,

Mie labda pochi,pochi siwezi imenishinda kusombelea vitu kwenye bega na kwapani🙌,,napenda kununua pochi,mkoba mzuri nikiupenda lkn siwezi kutumia.

Nguo viatu nk,watoto wa kike tupo wengi usipoivaa mwenzio anayivaa
 
1. Kuna kitu kinadumu kama mkanda wa ngozi?nakumbuka nina mkanda huo nilinunuliwa na babu yangu 2012 huwezi kuamini mpaka leo ninatumia huohuo japokuwa umechoka sasa mwaka jana mwishoni nikaona duka la mikanda ya ngozi nikanunua ila ilanibidi niutafutie kwanza msumari nitoboe tobo basi hio kazi ya kutafuta msumari imenishinda mpaka leo wala sina time nao mkanda Mpya nimeufungia tu kabatini bado natamba nao wa zamani wenye miaka zaidi ya 10 na fresh tu japo umelegea sio smart.

2. Karibu yangu kuna swimming pool nikaogelea siku moja sasa kwa kuwa sijui kuogelea nikaingia mtandaoni nikaagiza swimming gears kama fins, goggles lengo niwe naogolea kila siku ..vifaa vikawasili ila hamasa ya kuogolea siioni tena kumbe sio hobby yangu kumbe ilikuwa mihemko tu.

3. Air fryer nilinunua maana niliiga kwa jamaa yangu ..nikalinunua ila nilipoonja tu kuku niliyemchoma nalo sikurudia tena kuku anakuwa hana ladha kabisa bora kukaanga na frying pan tu nimeliacha mpaka lile li basket lishaanza kupata kutu

4. Blender pia miyeyusho haitoi juice smoothie kama zile zilizosagwa na blender zenye nguvu..
vitu vingi watu tunanunua kwa kufuata Mkumbo tu.
TV, wakati nina mishe zakutoka saa 11 asubuhi na kurudi saa 5 usiku au sita nimejichokea nalala hadi na viatu. TV lipolipo tu halitumiki,nawaza kuliuza tu maana hata mpira tunaangalizia Bar huko.
 
Back
Top Bottom