Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Vitu vya uongo tunavyoonyeshwa kwenye muvi za kizungu

Kupigana juu ya treni inaweza fanyika live.

Kuweka bunduki kando na kupiga mkono pia inawezekana live.


Unaweza amini kama unaielewa sanaa ya mapigano na mkikutana wote wanaume kweli.

Pia kuchomoa nyaya kuungamisha na Gari kuwaka inawezekana live
 
Mama Kubwa nahisi wewe ni wale watu ambao mkiangalia muvi ukiona mtu kajificha na jambazi anakuja unaanza kumuambia "wewe ondoka hapo unakuja kuuliwa..!!" 🤣🤣🤣🤣
Acha Tu yaani hakuna kitu kinaniuma kama adui anamsogelea MTU Mwema halafu MTU Mwema kajificha, napataga kihede utafikiri ni Jambo la kweli.
 
Kupigana juu ya treni inaweza fanyika live.

Kuweka bunduki kando na kupiga mkono pia inawezekana live.


Unaweza amini kama unaielewa sanaa ya mapigano na mkikutana wote wanaume kweli.

Pia kuchomoa nyaya kuungamisha na Gari kuwaka inawezekana live

Mkuu sio kwamba hivyo vitu haviwezekani, ila kiuhalisia ni ngumu na hatari mno kuvifanya mfano kupigana kwenye treni inayotembea, nani na akili zake anaweza kufanya hivyo?

Hiyo ya kuwasha gari kwa waya, kuna siku niliwahi kuona gari imeharibika sehemu ya ufunguo jamaa akaita fundi ambae ni mtaalamu wa hayo mambo. Jamaa alikuja na toolbox na alihangaika pale zaidi ya lisaa ndio akafanikiwa kufungua ile sehemu ya starter. Sasa kwenye muvi hua ni sekunde mtu kashawasha kasepa. Ni sawa na ile ya kufungua kitasa cha mlango bila funguo kwa kutumia viwaya. Kiuhalisia utakesha hapo
 
Kurukia gari la taka tokea ghorofa ya 6
Wazungu hawadanganyi wanaigiza movie kiuhalisia Ila wanaongeza chumvi,
 
Namba 3 naona kama sijaelewa

Hapo kwenye jet li kupigana na majambazi 6 huku wakija kwa zamuzamu kidogo naweza kutetea... wajuzi wa ngumi nadhani watanisahihisha kama nakosea

Ni kwamba mkiwa wengi mkashambulia kwa pamoja kuna hatari ya kuzidiwa kiwango na wote mkawa defeated kwa pamoja kuliko akienda mmoja mmoja ambapo atapambana kwa weledi na kumchosha adui ili anapokuja mwingine akute jamaa kadebweda. Hatahivyo uongo wao unabaki palepale kwakuwa pamoja na kuja mmoja mmoja bado jamaa ndo kwanza nguvu inaongezeka maradufu na anawamaliza wote


Namba 2 hata me mwenyewe huwa nashangaa sana maana karibia muvi zote utakuta pambano la ngumi huku chombo kiko na mwendo hasa za kihindi. Unakuta eti pambano kali kabisa huku wako kwenye mwendo mkali katika sehemu ya nje ya chombo kama boti jet pikipiki gari au treni tena kwenye msongamano kabisa eti. Jambo hili ukitaka kujua haliwezekani fanya tu majaribio hata wewe mwenyewe

Hiyo ya mtu muovu lazima afe bwana imezoeleka sana kwamba "Stelingi hauawi" ila kinachoniacha hoi stelingi wa picha za zamani lazima aanze kuchezea kichapo cha maana yeye kwanza. Picha za kisasa nazo stelingi yeye anaadhibu wenzake tangu picha inaanza mpaka kuisha hutaona akidondoshwa chini wala kujeruhiwa kidole wala kupigwa hata kibao

Pia hapo kwenye stelingi hauawi huwa nacheka eti anagongwa risasi 16 anapona wakati yeye akiwashoot majambazi hata risasi moja ya mguu tu jambazi chali anakufa

Uongo mwingine kupita yote ni kupambana na polisi waliojihami na silaha na kuwashinda wote

Pia kuna ile ya kushtukia bomu pahala likiwa limebakiza sekunde chache sana kulipuka na kufanikiwa kukwepa madhara ya bomu hilo ndani ya sekunde hizohizo chache. Maranyingi unakuta eti staa mpaka anafanikiwa kuzuia/kukata waya/kutegua basi ilikuwa imebaki sekunde 1 tu kama angechelewa bomu lingelipuka

Ile ya wananchi hawawezi kujitetea mbele ya wahalifu hata kwa wingi wao mpaka aje mtu/watu fulani ambao ndio tegemeo lao aje awakomboe

Kuna vile unamkimbia adui yako mara unakutana nae mbele halafu yeye hakimbii wala nini

Pia mtu anapigwa teke/ngumi hadi mguu/mkono unavunjika. Haiishii hapo bado huyo mtu anafunga sehemu hiyo kwa shati yake na anaendelea kupambana na (huenda) akashinda
 
Jambazi na Staa wanawindana kwajili ya kuuana lakini jambazi anafika mpaka mahali alipo staa halafu anaua mtu mwingine tu kisha akitaka kuongeza shot nyingine ya kumshoot staa anashindwa eidha kwa staa kujificha kukwepa au kumuwahi yeye. Sasa huwa najiuliza hilo shambulio la kushtukiza si angelielekeza moja kwa moja kwa kumshoot star
 
Wengi hua tunadhani muvi za bongo tu ndio zina vitu vya hovyo. Kiukweli muvi za kizungu pia zina maujinga mengi yasiyo na uhalisia. Hivi ni kati ya vitu vya uongo na vinavyokera hasa kwenye muvi za kizugu.

1. Bunduki kutokuisha risasi. Ushawahi ona kwenye muvi mtu ana ki bastola au SMG anamwaga risasi lisaa lizima na haziishi? Uongo mtupu.

2. Watu kupigana juu ya treni huku inatembea! Hiki ni kitu cha hovyo kabisa hata kukiwaza tu. Hata kupigana juu ya treni iliyosimama ni shughuli pevu achilia mbali inayotembea.

3. Bomu la kutegwa kupiga alarm kabla ya kulipuka. Wanajeshi wanaingia kwenye nyumba, hawajui kama kuna bomu. Mara wanasikia mlio pi pi pi pi pipipipipipi...Booom! [emoji38] saa hiyo wanakua wameshatoka nje.

4. Watu wema kushinda. Katika muvi karibu nyingi, wale watu wema hua wanashinda na watu wabaya wanauawa. Hii haina uhalisia wowote kwenye maisha ya kawaida.

5. Kuwasha gari kwa kuchomoa nyaya chini ya usukani na kuzigusanisha. Japo hii inawezekana, lakini ni ngumu mno kutekelezeka kiuhalisia. Hata fundi mwenye vifaa, inakuchukua muda mrefu sana kufanikisha hili.

6. Maadui kuweka bunduki chini ili wapigane ngumi [emoji23]

Hebu na wewe ongezea vitu vya kijinga ulivyowahi kuona kwenye movie
kuruka toka juu ya ghorofa
 
Kurukia gari la taka tokea ghorofa ya 6
Wazungu hawadanganyi wanaigiza movie kiuhalisia Ila wanaongeza chumvi,
Kwenye movie unaweza kuruka kutoka ghorofa yoyote mradi tu chini kuwe na yale ma container ya takataka au swimming pool au kuwe na jengo lenye bati juu ambapo ukiangukia unaingia nazo mpaka ndani ila huumii popote 😀
 
Mkuu ukibahatika tazama movie inaitwa shut em up. Hii jamaa alimzalisha mwanamke wakati mwanamke huyo ana windwa kuuliwa majambazi wamezunguka wakati mapambano yakiendelea jamaa akakosa wembe akaamua kitovu cha mtoto kukikata kwa risasi,

Nyingine alikuwa anakula papuchi majambazi wakavamia alipambana nao huku dushe lipo ndani na mwanamke anaguna tu ana mbadili mitindo mbalimbali hadi maadui wakaisha na yeye akamwaga wachina..

Kuna uongo humo japo inafurahisha
 
Jambazi na Staa wanawindana kwajili ya kuuana lakini jambazi anafika mpaka mahali alipo staa halafu anaua mtu mwingine tu kisha akitaka kuongeza shot nyingine ya kumshoot staa anashindwa eidha kwa staa kujificha kukwepa au kumuwahi yeye. Sasa huwa najiuliza hilo shambulio la kushtukiza si angelielekeza moja kwa moja kwa kumshoot star
Au hata jambazi akimpiga staa akaanguka hammalizii, anamuacha amelala hapo chini yeye anaendelea kuua watu wengine. Baada ya dakika chache staa ananyanyuka na kumuua jambazi 😆
 
Back
Top Bottom